Uzuri wake Congo ishajiunga EA,matatizo yake yatatafutiwa ufumbuzi wa kina.
Ingawa hayatoisha yote.
M23 hawana ubavu wa kuivamia DR Congo na hata Rwanda peke yake haina uwezo huo pia, hii ni kama Ukraine isivyokuwa na uwezo wa kuibwekea Russia. Hii ni wazi kuwa rasilimali za DRC zinaporwa na wazungu kupitia Rwanda, tuwe makini na huu mgogoro, tusiuchukulie poa. Inawezekana kabisa mali za DRC ndizo zinazogharamia vita ya Ukraine, you never know.Cha kujiuliza hapa inakuwaje vurugu za Mkoa wa Kivu zinahibuka sambamba na vita inayo endelea huko Ukraine,je,hii ni co-incident tu au kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia - msichikulie tatizo hili kimzaa mzaa hata kidogo.
Binafsi naona members wa EAC wanaoneana aibu hakuna anaye weza kumfunga paka kengere!! Nchi ambazo zinaweza kumaliza mgogoro huu kati ya Congo DRC na Rwanda ni nchi za SADC na majeshi yake - haya mambo ya kusema sijui EAC inaweza kumaliza mgogoro huu hilo sahau kabisa ie tutakuwa tuna jidanganya tu na kupoteza muda.
Kumbukeni kwamba hawa wanao jiita eti "M23" pamoja na mfadhili wao mkuu wote wako determined kweli kweli kuumega Mkoa wote wa KIVU na kulazimisha uungane na nchi jirani kwa kisingizio kwamba wana onewa na kubaguliwa na Wacongoman huo ni uongo mtupu - narudia kusema kwamba annexing KIVU ndio ulikuwa mpango wao mkuu wa miaka mingi tu - hivi sasa wanapata kiburi zaidi kwa kuwa wanajua kwamba akina: Tony Blair,Bill Clinton,Bush Jr, Boris Johnson nk watawakingia kifua kwenye taasisi za kimataifa kwa madai kwamba Congo DRC is too big a country hivyo iwe divided kama ilivyo kuwa Sudan etc hilo ndilo linalo kuja - don't you underrate the resolve of the so called Banyamulenges na mfadhili wao mkuu - ambaye ndiye the brains behind all these on going turmoil in North Eastern Congo DRC specifically KIVU Region, as I said lengo kuu ni ku-annex KIVU mengine ni geresha tu.
Sasa hivi Rwanda ni sehemu ya Uingereza, inapokea wakimbizi na wageni wa UK, ona hata Mkutano wa jumuiya ya madola ulifanyikia Rwanda, Sio rahisi Rwanda kuweka tangazo lake kwenye timu kubwa kama Arsenal wakati Rwanda hakuna demokrasia, rais Kagame yuko madarakani milele lakini EU na bwana mkubwa Marekani vinara wa kuhubiri demokrasia wako kimya.Nikifanikiwa kuwa Rais, East Africa itaitii Tanzania.
Sijajua why Rwanda atusumbue zone hii.
Ila ya Sudan ,yatatokea DRC ,Kivu yote itakuja kuwa nchi, ni suala la muda tu .maana kuna DRC zones tatu, ya Kinshasa, Kivu(goma) na Lubumbashi.
Kivu ataondoka, mkataba wa Lemela kuna siku utatimia.
M23 hawana ubavu wa kuivamia DR Congo na hata Rwanda peke yake haina uwezo huo pia, hii ni kama Ukraine isivyokuwa na uwezo wa kuibwekea Russia. Hii ni wazi kuwa rasilimali za DRC zinaporwa na wazungu kupitia Rwanda, tuwe makini na huu mgogoro, tusiuchukulie poa. Inawezekana kabisa mali za DRC ndizo zinazogharamia vita ya Ukraine, you never know.
Nchi za Magharibi zimezigeuza nchi nyingine shamba lao,Uwezekano huo upo, niliwahi kushangaa nilipo fahamishwa kwamba madini yaliyo tumika kwenye majaribio ya kwanza ya nuclear bom kwenye jangwa la Nevada new Mexico in 1945 kumbe yalitoka Belgian Congo (now Congo DRC)-vile vile na mabom mawili yaliyo dondoshwa Hiroshima na Nagasaki nayo yaliuudwa na madini ya Uranium kutoka Congo DRC lakini Wamerikani na Waingereza wakawa wanazuga Dunia kwamba madini yali chimbwa huko Canada, kumbe ni ulaghai mtupu.
Nchi za Magharibi zimezigeuza nchi nyingine shamba lao,
Akili halisi inayomfaa mtu na majirani zake ni Ile ya kuzaliwa nayo, hawa ni wachumia tumbo.Binafsi kinacho nisikitisha sana sana mimi ni pale nionapo baadhi ya waswahili/wabantu wenzangu waki husudu kupindukia baadhi ya mataifa ya magharibi, wakati mwingine kichukulia moja ya mataifa hayo ya magharibi kama ni Mungu wao wa hapa Duniani, uwambii kitu wakakuelewa hata kidogo - mnaishia kubishana usiku kucha. Inatia simanzi sana sana.