Ukraine: Wanaume waliokwepa kujiunga na programu ya Jeshi wa anza kukamatwa

Ukraine: Wanaume waliokwepa kujiunga na programu ya Jeshi wa anza kukamatwa

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanaume waliokwepa kujiunga na programu ya Jeshi na kwenda klabu kula bata huko Ukraine wamekutana nacho baada ya Jeshi la Nchi hiyo kuanzisha msako wa kuwakamata Wanaume wote waliokwepa programu hiyo kwenye kumbi za starehe, matamasha ya Muziki, sehemu za manunuzi, migahawa na maeneo ya Umma.

Video ya Mwanaume mmoja aliyehudhuria mapema wikiendi hii kwenye tamasha la bendi ya Muziki ya Okean Elzy katika Jumba la Michezo la Kyiv imesambaa mitandaoni ikionyesha akiwa anakamatwa na Maafisa watatu wa Polisi baada ya kukagua hati zake na kuonekana kuwa na kasoro.

Kitu ambacho inawezekana hukijui ni kwamba kulingana na Sheria za Ukraine, Wanaume wote wenye umri kati ya miaka 25 hadi 60 wanastahili kujiunga na programu maalum ya Jeshi na Wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 60 pia wamepigwa marufuku kuondoka Nchini humo hivi karibuni.

Soma Pia: Ukraine kapigwa na kitu kizito wapoteza zaidi ya wanajeshi 600

Hii ni Kutokana na uhaba mkubwa wa Wanajeshi ambao Taifa hilo linakabiliana nao wakati vita dhidi yake na Urusi vikipamba moto, Ukraine ilipunguza umri wake wa Watu kuhama kutoka miaka 27 hadi 25 na kufunga mwanya wa Watu kuondoka Nchini humo tangu April mwaka huu.

Takwimu za Huduma ya Walinzi wa Mipakani Nchini humo iliripoti mwezi April kwamba takribani Wanaume 30 walifariki wakijaribu kukimbia Nchi hiyo tangu kuanza kwa vita, mara nyingi wamekufa kwa kuzama walipokuwa wakijaribu kuogelea kwenye mito yenye baridi kali.
 
Wazungu vichwa maji tu wanajidai Wana akili alafu wanshindwa kusuruhisha matatizo yao
 
Wazungu vichwa maji tu wanajidai Wana akili alafu wanshindwa kusuruhisha matatizo yao
Ukraine anatumika kama chambo tu; ile vita ni kati ya USA na Russia; communist world Vs Capitalists. Kimsingi hi vita ilitakiwa kupiganwa wakati ule wa Vita baridi duniani yaani before 1988. Ukraine bila kujitambua, kaingia mkenge
 
Lazima wabaki watu watakaokua busy kuzalisha vinginevyo nchi itaangamia
 
Wakati wa amani wanajeshi wanakula salary. Wakati wa vita watu wote wanaswagwa.
 
Bado ripoti nyingine zinasema hata walio mstari wa mbele vitani wamechoka vita,imefika wakati wanaacha kutii amri za makamanda,wengine wakizidi kujisalimisha kwa majeshi ya Russia!
 
Back
Top Bottom