Ukraine yafurahia shehena ya mabomu haramu, wako tayari kuyatumia

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kamanda wa vikosi vya ardhini wa Ukraine Colonel General Olesksandr Syrskyi amekiri kupokea shehena ya mabomu haramu yanayoripuka kwa kuchawanyika na kwamba wataanza kuyatumia siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo waandishi wa habari wameiona mizinga aina ya American M777 howitzers karibu na maeneo ya Bakhmut ambayo ndiyo yenye uwezo wa kurusha mabomu hayo.

Kamanda Syrkkyl aliyasema hayo hapo jana Julali 18 alipokuwa akizungumza na kituo cha habari cha BBC.Moja ya faida ya kutumia mabomu hayo alisema ni kwamba yataweza kuwauwa askari wa Urujsi kwa wingi na hiyo itakuwa ni salamu itakayowafikia familia za askari hao waliobaki majumbani.

Ikulu ya Marekani kwa upande wake imesema imetoa msaada huu kwa Ukraine kuwawezesha askari wa Ukraine kuzipenya ngome za jeshi la Urusi kwani bila hivyo Ukraine hawatoweza ng'o kupenya ngome hizo.Kwa upande mwengine uamuzi huo umekuja wakati ambapo Marekani imepungukiwa mno na silaha za kuipa Ukraine kuendelea na mashambulizi yake ya kurudisha maeneo yaliyotekwa na Urusi.

1689756728926.png

Yahoo News
 
View attachment 2692913

Yahoo News
Russia kayatumia pia haya mabomu hapo Ukraine, so siyo kitu cha kipekee. Jambo ambalo sijajua maana yake ni hii ya Ukraine kuweka matangazo ya silaha anazotarajia kutumia kwenye vita, mbona asizitumie kimya kimya?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kijeshi haipo hivyo neno kuishiwa haina maana hiyo kabisa. Stock yao ipo kama ilivyo kwendana na lolote litakalo jitokeza.
Maana hiyo ni ya kwako kinyume na raisi Biden na ikulu ya Marekani
 
Wanaropoka halafu baadaye wanaanza kulalamika.
Wanapenda propaganda ya kutishia.Vile vifaru vyote walivyoviomba kwa miezi kadhaa kama kwamba wakivipata ndio ushindi hatimae wameamua kuviacha na kutembea kwa miguu na vingi vimeshaharibiwa katika vita.
Silaha ya mwisho wanayobembeleza sana wapatiwe ni ndege za F16.
 
Ogopa sana mrusi yeye ni ngumi nyingi maneno kidogo
 
Russia kayatumia pia haya mabomu hapo Ukraine, so siyo kitu cha kipekee. Jambo ambalo sijajua maana yake ni hii ya Ukraine kuweka matangazo ya silaha anazotarajia kutumia kwenye vita, mbona asizitumie kimya kimya?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Hata Mimi Huwa nashangaa sana aisee,yahani mpo mnagombana na mtu alafu unamwambia mtesi wako kwamba dakika chache zijazo nitakupiga ngumi ya sikio!

Hii ndio imesababisha long anticipated counteroffensive kuwa na mwendo wa kinyonga
Vinginevyo hii michezo inachezwa kimakusudi Ili kurefusha vita

Tofauti na hapo basi wazungu wamekuwa vilaza kupita kiasi!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Kama USA IMEISHIWA SILAHA URUSI IENDE KUIVAMIA MAREKANI BASI
yanini kufanya uchokozi. Ukitaka daima ushinde katika vita pigana baada ya kuchokozwa. Mrusi atampiga kidogo kidogo hapo Ukraine mpaka ataisha.
 
Maana hiyo ni ya kwako kinyume na raisi Biden na ikulu ya Marekani
Bro uko serious kabisa kwamba silaha ambazo wao watahitaji pindi unapoingia katika vita ziwe kidogo? Producer yoyote wa silaha duniani huwezi kuta ana kitu kama hicho ndiyo maana huwa wanazalisha zaidi kwendana na mahitaji ya mshirika pindi naye anapopata uhitaji hivyo yawezekana kiwango hicho ndicho kimepungua. Vita ina mambo mengi sana achana battlefield tu pale.
 
Kuna unga wa kutengenezea risasi ili ikamilike unapatikana Urusi pekee na wamemuwekea vikwazo.
SOMA MAKALA HII UTAFAHAMU
 
Kuna unga wa kutengenezea risasi ili ikamilike unapatikana Urusi pekee na wamemuwekea vikwazo.
Hayo mambo yapo hivyo nadhani siumeona hata kinachoendelea kati ya USA na China kuhusu manunuzi ya hizi Semiconductor devices.

Kwasababu hata Russia naye kuna baadhi ya spare alikuwa anategemea zaidi Europe hasa katika ndege.
 
Back
Top Bottom