Ukristo na dini zingine zinatumia njia gani kupambana na propaganda?

Ukristo na dini zingine zinatumia njia gani kupambana na propaganda?

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
16,950
Reaction score
13,527
Wana ukumbi,

Naomba awali ya yote nisionekane kama ni mtu ambae nimekuja kwa choko choko ama ni mtu mwenye mtazamo wa ubaguz.,la hasha nimekutwa na hili wazo na naomba nilete kwenu tulijadili.

Katika karne hii ya 21 na miongo yake kadhaa sasa,suala la iman za dini limekuwa kizungumkuti kwa waumin na wafuatiliaji wa iman hizo kwa namna mbali mbali,

Dini kama tuijuavyo ni kiungo muhim sana katika jamii ambacho humuunganisha mwanadamu moja kwa moja na mola wake hususan wale wenye kuamin uwapo wa mungu muumba.

Mimi binafsi yangu ni muislam,naamin uwepo wa mungu,naamin uwepo wa siku ya mwisho ya hukumu,na naamin nitakuja hukumiwa kwa kila tendo baya na zuri ninalolifanya.

Hoja yangu iko hivi:

Mara nyingi huwa tumekuwa tunaskia watu wa mataifa mbali mbali ambao huwa kwa namna moja ama nyingine huingia kwenye tafaruku na migogoro hadi kufikia kuingia vitani na kumwaga damu,damu za watu wasio na hatia,kina mama,wazee,watoto,walemavu na watu wa aina mbali mbali,

Mimi kwa dini yangu na iman yangu,umwagaji damu kwa watu wasio na hatia na hata wale wenye hatia bila uthibitisho na uhakika wenye uwazi hairuhisiwi na ni dhambi kubwa kabisa.

Tumeona siku hiz za karibun kuibuka kwa makundi mbali mbali yanayojihusisha na vurugu na malumbano na migogoro mbali mbali ya kimaslahi ya dunia huku wakiegemea kwenye iman za dini,

Wapo watu kama alqaeda,boko haram,alshabaab na kadhalika just to mention but a few,hao huegemea kwenye uislam kufanya harakati zao.,UISLAM HAUSEMI HIVO NA WAISLAM HATUKUBALIANA NA KILA HOJA ZAO.

Pia wapo watu wengine Tuchukulie Kama Joseph Kony wa uganda anaetumia Lord Resistance army kuendesha harakati za kutaka kusimamisha dola ambayo itaongozwa kwa kufuata amri kumi za mungu,huku akitumia watoto wadogo kwenye jeshi hilo na kubaka kina mama na kusababisha vifo vya wengi wasio na hatia,UKRISTO HAUSEMI HIVO NA WAKRISTO HAWAKUBALIANA NA HICHO ANACHOKIFANYA.

Ipo migogoro ya kidini pia northen ireland ambako watu hufikia hatua ya kumwagana damu kwa kias kikubwa sana,na hiyo yote ni kutofautiana katika maandiko na wakati mwingine hata kupignia maslahi flani.

Swali nalouliza ni kwamba,

Hizi dini zingine zimewezaje kukabiliana na hila za media ambazo kwa kias kikubwa huhusisha vurugu na migogoro flan moja kwa moja na iman husika za watu?

Mfano,ni mara zote utaskia zikifanyika harakati za watu kama alqaeda,alshabaab,na kadhalika wanaolandana nao MEDIA KWA KUJUA NA KWA MAKUSUDI KABISA WANATUMIA TERMS KAMA ''ISLAMIST GUNMEN,MUSLIM TERRORIST,MUSLM MILITIA,ISLAMIC REBELS,ISLAMIC RADICALS'' na kadhalika?
Kwanin Media moja kwa moja zihusishe neno ''Islam or Muslims'' na violence?hata pale pasipokuwa na msingi huo ili hali wanafaham fika kwa kufanya hivyo wanakua wamesha associate iman flan na vitendo hivo??

Pia,mbona Media hizo hizo hatuskii zikitumia terms kama hizo kwa vikundi hivi vya kigaid kama vya LRA NA JOSEPH KONE VINAVYOTUMIA MGONGO WA DINI YA UKRISTO KUFANYA MAOVU KWA KUTUMIA TERMS KAMA ''CHRISTIAN GUNMEN?,CHRISTIAN MILITIA?CHRISTIAN RADICALS?,CHRISTIAN REBELS NA KADHALIKA?

Kwanin Media inapofikia situations kama hizo huonesha double standards kama kuripoti taarifa zake,kwa matukio ambayo kwa kias kikubwa yote yapo nje ya mafundisho ya dini na yote hayana baraka na waumin wa dini hizo wenye kuyafaham mafunzo kwa uhalisia?

Ndio,kwa maana nauliza au WENZETU WA IMAN ZINGINE HUTUMIA NJIA GANI KUPINGANA NA HIZI MEDIA PROPAGANDA ZINAHORIBU TASWIRA YA MAFUNDISHO YA IMAN ZA WATU??

KARIBUNI.
 
Ukristo sio Dini.

Ni kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.
Kufuata mafundisho yake.

Hakuna aya inayosema Ukristo ni DINI.

Zungumzia hizo dini zilizo jitambulisha kwa hilo jina.
 
Jibu ni simpo tu. Angalia magnitude ya Matukio yafanywayo kwa kivuli cha imani hiyo.

Chukua mfano mdogo juzi tu hapa Kuna kiumbe kule Alfagnistani kimejilipua na kuua watu 95 kwa imani ya kuona PEPO huku akiwa kaziba kifanyio chake kwa chuma kisiungue ili kule aendako apambane na wale Mabikra wa imani yake!

Huwezi fananisha jambo la imani hiyo na ile ya skotilandi!
 
Bado hamjamuelewa wote mliojibu hapo juu mnasukwumwa na imani zrnu kujibu
 
Taasisi za dini ya kiislam zinapaswa kuwa proactive katika kulaani vitendo vyote viovu vinavyofanywa na vikundi vya kigaidi vinavyojificha kwenye mwamvuli wa dini ya kiislam.
Ni mara chache kukuta waislamu wakiportray vikundi vya kigaidi kama ni vikundi vibaya sana hivyo waumini wake wasivifuate. Mtu kama Osama aliekuwa gaidi no. 1 duniani utakuta mnamuita Sheikh!!!??? Seriously!!!
Katika kutaka kuisafisha dini yenu kwa nini msianzishe utaratibu wa kukemea watu wanaochafua dini yenu kwa mwamvuli wa vifungu vidoogo vilivyomo kwenye Koran. Mfano huyu nabii Tito amepingwa makanisani na almost madhehebu yote ya kikristu!
Muwe mnakuwa wa kwanza kupinga na kukemea na kuportray a positive image ya dini yenu pindi mkiona kuna mtu anataka kuwachafua kwa msingi wa itikadi kali na kufikiri dunia nzima inapaswa kuwa ya kiislamu
 
Pia,mbona Media hizo hizo hatuskii zikitumia terms kama hizo kwa vikundi hivi vya kigaid kama vya LRA NA JOSEPH KONE VINAVYOTUMIA MGONGO WA DINI YA UKRISTO KUFANYA MAOVU KWA KUTUMIA TERMS KAMA ''CHRISTIAN GUNMEN?,CHRISTIAN MILITIA?CHRISTIAN RADICALS?,CHRISTIAN REBELS NA KADHALIKA?

Kwanin Media inapofikia situations kama hizo huonesha double standards kama kuripoti taarifa zake,kwa matukio ambayo kwa kias kikubwa yote yapo nje ya mafundisho ya dini na yote hayana baraka na waumin wa dini hizo wenye kuyafaham mafunzo kwa uhalisia?

Hii topic ni ya zamani sana, ila nikikaa nikawaza point ya mleta maada mstari kwa mstari naona kuna ulalamishi wa kwamba media zinawapendelea wakristo.

Inawezekana wamiliki ni wakristo ndo maana.

Kinachonishangaza kwenye hii imani ya Kiislamu, wakiwa kwenye nchi kama zetu wanalalamika kwamba wakristo wanapendelewa, wakiwa kwenye nchi zao ambazo ni full uislamu nako wanalalamika tena.

Duh!
 
Wacha dini zote zipotee tu maana hali inazidi kuwa mbaya.

Na asinidanganye mtu kuwa bila dini hatuwezi kuishi, kwani Mungu hayupo kwenye dini bali kwenye upendo wa dhati tena usio wa kulazimishana.
 
Back
Top Bottom