Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UKRISTO NI UDAKTARI BINGWA" KWAAJILI YA MAGONJWA SUGU NA WAGONJWA MAHUTUTI"
Anaandika, Robert Heriel
Yule Shahidi, Kuhani katika Hekalu Jeusi.
Nami ni shahidi, mwonaji, Mtibeli ambaye ninayashudia haya. Wala sio kwaajili yangu Bali kwaajili yao watafuta Njia, Njia iliyochongwa na watangulizi, mashahidi wa Yule aliyehai. Na katika yeye nasi tu hai. Nasi tutakuwa hai katika yeye.
Kwa maana kila Jambo linasiri zake, na kila Siri inawakati wake wa kuwekwa wazi. Ipo Siri zilizowekwa mihuri na kufichwa maana zake.
Haya ninyi watafuta Njia, msioiona Njia. Tazameni. Kila kitu ni chema Kwa waliowema. Kila MTU ni Mwema Kwa waliowema. Yeyote apendaye Wema huyo ataona Wema. Kwa maana Wema huishi katika Nafsi ya wapenda Wema. Naye aliyemwema hawezi uona ubaya hata akifanyiwa ubaya. Kwa maana yote ni Mema ikiwa ni mapenzi ya Mungu.
Yule Shahidi, Mkombozi wa Njia iliyotekwa. Ndiye Yesu Kristo aliyekuja Kwa ajili ya Wokovu, akaikomboa njia. Njia ya uzima. Na uzima ni kumjua Mungu wa kweli, Muumba wa yote. Aliyehuru na akatufanya kuwa Huru kupitia ukombozi Kwa wale waliokuwa mateka.
Yule Yesu hakuja Kwa wote isipokuwa Kwa Waliokuwa utumwani, naam waliopotea katika njia. Wenye magonjwa SUGU na waliomahututi, na waliokufa.
Ukristo ni kwaajili ya waliotengwa, waliomahututi, Maskini na ambao hawana tumaini. Mayatima na Wajane. Ukristo sio kwaajili ya Watakatifu, sio kwaajili ya Makuhani wenye kumcha Mungu, sio kwaajili ya Watoto wa wachungaji, masheikhe, Walawi, maaskofu na wale wote wajionao ni Wema. Ukristo sio kwaajili ya Wayahudi, au Watibeli. Hapana.
Ukristo uliletwa kwaajili ya wale waliodharauliwa, Wadhambi, wazinzi, wachawi, walawiti, mashoga, wasagaji, walevi, wafiraji, watukanaji, na waliokufa Kiroho.
Hao ndio waliokuja kukombolewa na Shahidi Yesu Kristo, Ukristo ni uspeshalisti Kwa wagonjwa waliokwisha Kufa, wenye Hali Mbaya, waliopo ICU.
Nami Taikon, Mtibeli nikasema yakuwa Mungu wa Tibeli ni Mungu wa wote. Mungu wa Watakatifu wanaozishika amri na sheria zake Kwa mkono wa Torati ya Musa, tena ni Mungu wa Walioasi, wenye dhambi, waliomahututi Kwa mkono wa Shahidi Yesu Kristo, tena ndiye Mungu wa Usafi na unyenyekevu Kwa mkono wa Muhammad.
Yeye ndiye ajuaye yote, amilikiye yote katika yote. Yeye ndiye mwenye Hekima na mjuvi wa kukomboa Watu wake waliopotoka katika Uhuru aliowapa(kwani kupitia upendo Nafsi zote zi huru kujiamulia) hiyo ndio HAKI. Kwa maana Mungu wetu ni Mungu mwenye HAKI.
Basi Taikon nasema, wewe uliyemsafi na mnyenyekevu usimkaripie na kumhukumu aliyemchafu na mwenye Kiburi. Kwa maana ninyi wote ni Watoto wa Mungu. Nasi tu Watoto wa Baba mmoja.
Yesu alikuja Kwa sababu ya Watoto waliozaliwa katika dhambi. Embu fikiria mtoto aliyezaliwa na kukulia katika mazingira ya umalaya na ulevi. Bila Shaka mtoto huyo automatically atakuwa Malaya na mlevi. Basi Kristo ndiye Shahidi aliyekuja kwaajili ya Watu wa namna hiyo ili kuwapa Ile Zawadi na tunu ya Neema ya Mola wetu Mlezi, Mungu mwenye Nguvu.
Nawe ujapojikwaa na kuangaka, ukaharibiwa na Matendo yako ya dhambi na uasi. Walimwengu na dunia ikakuona wewe haifai. Basi tambua Mungu anakitengo maalumu kwaajili yako, nacho ni kupitia Ukristo, naam kitengo cha magonjwa ya dharura, SUGU na wagonjwa MAHUTUTI.
Usiukimbie USO WA Mungu wako. Kwa maana yeye ndiye chanzo cha yote. Wala hataki yoyote apotee..wale Watakatifu wafuate utakatifu kupitia Torati na Quran. Na wale watakaoanguka mara Kwa mara basi upo mlango wa rehema kupitia Kristo.
Hayo nayo niliyasema Kwa Watibeli, na Wayahudi, na Wakristo, na Waislam, na wabudha, na wahindu, na wapagani. Na kila Mwanadamu mwenye uhai. Mwenye kusikia na asikie.
Wala simhukumu yeyote, kwani hiyo sio kazi yangu, Kwa maana kwenye upendo hakuna Hukumu.
Mungu mwenyezi awe pamoja nanyi. Amani yake iwe pamoja na wote mumtafutao. Amina!
Ni yule Shahidi Kutoka Nyota ya Tibeli.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam