ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Muinjilisti na Msomi wa dini bwana Sylvanus Ngemera amesema anatarajia kuasisi Dini Mpya ya kikristo yenye msingi wa utamaduni na mila za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara itakayoutwa "African Orthodox Derekh Church" Ili kuachana na Ukristo wa Mzungu ambao umejikita kutetea utamaduni wa mzungu na kuhimiza ukoloni mamboleo Kwa mtindo wa utoaji Fedha au sadaka.
Mwinjilisti huyo amesema watatumia biblia hii hii ila yenye tafsiri ya Kiebrania badala ya kiyunani(Rumi).
Aidha amesema Dini hii inalenga kupambana na ukoloni wa dini,mmomonyoko wa maadili na italeta Nguvu za Kimungu za kupambana na uovu ikiwemo uchawi,waganga na utapeli unaoendelea kwani Ukristo huu wa Mzungu ni vigumu kutambua ikiwa ni Imani halali au utapeli na kwamba Ukristo unaonekana kama mzaha.👇
=========================
Wakati dini ikihusishwa na utamaduni wa kule ilipotoka, Mwinjilisti Silvanus Ngemera (67) ameanza mchakato kuanzisha madhehebu ya Ukristo yatakayorejesha utamaduni wa Mwafrika.
Madhehebu hayo yatakayoitwa Derekh yanalenga kupambana na mmomonyoko wa maadili, kuachana na dhambi, pamoja na kuuishi utamaduni wa asili ya Mwafrika.
Mwinjilisti Ngemera amesema Waafrika wanapaswa kutambua kuwa, yapo madhehebu yao, ambayo kila mtu mwenye Mungu ndani yake ana uwezo wa kutenda kwenye dhehebu la Derekh na si watu maalumu kama ilivyozoeleka.
Ameyasema hayo leo Ijumaa ya Septemba 6, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
"Ukristo huu mpya hauna ngazi ndani yake, unamuhusu Mwafrika mwenyewe. Hakutakuwa na mahubiri ya fedha na hatutakuwa na nyimbo wala vyombo vya Kizungu kwenye masinagogi yetu tutakuwa na nyimbo zetu za asili za makabila.
Mwinjilisti Ngemera ambaye ni mkereketwa wa maendeleo ya Waafrika weusi ambao anawaona ni watu wa kubaki nyuma katika mambo mengi hivyo ameamua wa dhehebu hilo kwa ajili ya kuleta mapinduzi kwao.
My Take
Kama dini hii itaondoa masharti ya kipuuzi ya Kuoa Mke mmja yaliyowekwa na Wazungu Kwa lengo la kudhibiti uzazi Afrika nitakuwa wa kwanza kujiunga.
Wasambaza haraka hiyo biblia na Muongozo wake tuusome.African Religion and Churches zimekuwepo kabla ya ukoloni kuja.
Naunga mkono vision hii ya Muinjilisti.👇👇
Soma Pia: Athari za ukoloni na dini mpya kwa jamii ya kiafrika