Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Unapokopa unawekeza katika miradi inayozalisha zaidi kuliko ile gharama ya kukopa(cost of borrowing), miradi mikubwa tuliyoiona ni ile iliyoanzishwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli, miradi wa SGR, Bwawa la Umeme la Julius Nyerere, mradi wa mabasi ya mwendokasi, mradi wa barabara njia nane toka Dar hadi Morogoro, Ununuzi wa ndege Mpya 15, Ujenzi wa Meli za kisasa Ziwa Victoria,Z iwa Tanganyika, na kuhamisha makao makuu toka Dar hadi Dodoma, je, mikopo hiyo ndiyo inakwenda kwenye miradi hiyo muhimu kwa Taifa la Tanzania?,
Unapokopa na ukachezea au ukahamisha hela ya mkopo kwa kitu kisichokusudiwa unaingia kwenye utumwa wa madeni.
Debt is like any other trap, easy enough to get into, but hard enough to get out of.Some debts are fun when you are acquiring them, but none are fun when you set about retiring them, Wars in old times were made to get slaves, the modern implement of imposing slavery is debt.
Hofu ya wananchi ni kwamba, je ni kwa asilia ngapi pesa zinazokopwa zinaenda kufanya lengo lililokusudiwa pasipo kuwa na upotevu wa pesa yoyote.
Hii mikopo kama inafanya mambo ya maana angalau ila kama ni haya mambo yakununua V8 SUV, nimeona kamanda wa Burkina Faso amewekeza kwenye miradi yenye tija badala ya hayo ma V8 kanunua tractors na kupunguza mishahara ya mawaziri huku akiongeza mishahara ya wafanyakazi kwa 50%, ni kiongozi wakuigwa kwa tunakoelekea hili deni si rafiki hata kidogo na hili kwa % kubwa ni haya mambo ya uchaguzi.
Kwa ukubwa wa hii nchi tungewekeza kwenye kilimo, viwanda na kumalizia viporo vya miradi yenye tija, hayo mapikipiki na magari yanatuongezea madeni zaidi, tukumbuke kodi zetu ndizo zitakazolipa hayo madeni, mapato yanayokusanywa ndio yanalipa hilo deni, tukishindwa tujiandae shilingi yenu kuporomoka zaidi kwa sababu ya hilo deni, tuitizame Kenya deni la taifa linavyowaumiza.
Kwa sasa wanakopa deni lenye masharti nafuu kulipa deni lenye masharti magumu, deni likifikia above 45% ya GDP sio himilivu tena, hii ina athari mpaka kwa raia mitaani rejea majirani zetu.
Kwa nini tusiishi kama enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Ali Hassan Mwinyi, katika awamu zao tulikuwa hatukopesheki walikuwa, tulikuwa hatufungamani na upande wowote na mikopo kwa wakomunist ilikuwa marufuku, tulipata mikopo midogo midogo tuu na grants from British government na Scandinavian countries, kwa mikopo hiyo midogo tuliweza kuishi bila madeni, shida ipo kwenye ulazima wa kukopa, ni kweli tunahitaji kukopa? Je, tungejinyima tungeweza kupata hela?
Alipoingia madarakani Hayati Rais John Pombe Magufuli, deni la taifa lilikuwa ni shilingi 35 trillion, kwa mujibu wa taarifa rasmi za bunge la Tanzania, deni likaendelea kukua na kufikia shilingi 60.7 trilioni mwezi April 2021 "Ongezeko la deni la Serikali katika Awamu ya tano ya CCM iliyoongozwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli lilitokana na kupokelewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji, na kulipa malimbikizo ya riba ya deni la nje"Awamu ya sita ilipoanza, April 2021 deni la Serikali lilikuwa sh 60.9 trilioni hadi kufikia machi 2024 deni la Serikali lilikuwa trilioni 91.7.
Shida ni nini? Je ni kushuka kwa thamani ya shilingi yetu ndio maana deni la Taifa linaongezeka au mikopo tunayoendelea kuchukua? rekodi ya kushuka kwa thamani ya shilingi yetu ipo kama ifuatavyo ;- Mwaka 2020. 1 Dollar -Tshs 2,314.8
Mwaka 2021. 1Dollar -Tshs 2,314.3
Mwaka 2022. 1Dollar- Tshs 2,326.1
Mwaka 2023 1Dollar- Tshs 2,419.6
Mwaka 2024 1Dollar- Tshs 2,463.5(Jan -June)
Sasa hivi June 2024 1Dollar -Tshs 2,627.5 sasa kwa nini hela yetu inashuka sana thamani? Je, Devaluation ya local currency pia ni mbinu ya uchumu ku-promote export na ku-discurrage import, tuna import mno.
Inatakiwe tuzalishe wenyewe na vingine tuanze kuexport nje ndio tutabalance trade, Dollar rate inakua determined na balance of trade i.e imports vs exports tanzania has imbalance terms of trade kila kitu tuna import na sie tuna export kidogo, Mama aongeze nguvu kwenye tourism inaweza kutuokoa.
-Nini lifanyike;-
Serikali ijikite kuongeza uzalishaji na mauzo ya nje, Serikali ivutie zaidi miradi ya uwekezaji, Serikali iongeze juhudi kwenye kuzalisha bidhaa ambazo tunaagiza nje ya nchi kama ngano, mafuta, maziwa, furnitures na bidhaa za mifugo.
Nimalizie kwa kusema kwamba hata mtaani mtu anapokuwa na madeni mengi unaona anavyoangaika, maisha yake hayawi sawa tena, anakuwa mtumwa, pengine vitu vyake nyumbani vitapigwa mnada, mkopo si mzuri, na hasa hii mikopo ya siku hizi yenye jina la "kausha damu" damu ni uhai, ikikauka maana yake ni kifo, kwa nini tufe na madeni!??
====
Pia soma: Prof. Mkumbo: Deni la Taifa lafikia Trilioni 92.7
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.