Ejolisi
Member
- Aug 26, 2022
- 57
- 87
Tanzania kwa kiwango cha uchumi tulichopo kuna haja kubwa ya kufungua na kutoa uhuru kwa wananchi kujishughulisha na kazi yoyote ilmradi haigharimu taifa kiuchumi.
Kiu kubwa ni kuwepo kwa mianya ya uzalishaji na mazingira rafiki kati ya wananchi na serikali hasa katika utengenezaji wa mazingira rafiki ya utendaji kazi na ukusanyaji wa kodi.
Andiko hili fupi litaangazia zaidi katika makundi ya hasa wanawake wanaojiuza maarufu kama “dada poa” na watu wengine wanaokamatwa Kwa makosa ya uzembe na uzururaji nguvu kazi inayotumika katika kushughulikia mambo haya ni kubwa ilihali haiongeze faida yoyote kiuchumi.
Ukuaji wa maendeleo wa nchi yoyote inategemeana na uhuru uliopo kiuchumi shughuli za uzalishaji zinazofanyika kama hayana athari hasi kiuchumi zifanyike. Kwa kuanza na biashara ya umalaya. Kwanza biashara hii inahusisha mambo mengi ikiwemo sheria, Uchumi, afya na haki za binadamu. Kwa maana hiyo jambo hili halizuliki kwa namna linavyozuiliwa sasa njia inayotumika haitaleta suluhu ya kudumu.
Sheria ya uzembe na uzururaji (penal code) katika vipengele vya 176 na 177 vinaelezea kitendo cha mwanamke kuuza mwili wake kujiingizia kipato ni kosa kisheria. Je kukamata hawa wanawake na kupeleka jela kutapunguza jambo hili au maadili yatakua mazuri? Je hii ni namna sahihi ya kutatua tatizo hili? Je kukamata dada poa na kupeleka jela ni suluhu ya muda mrefu? Je mifumo ni wezeshi kwa mwanamke kupata kipato baada ya kuacha hiyo biashara?
Kwenye kipengele cha afya ni wazi ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya UKIMWI haupo kwa wingi kwa watu wanaojiuza wanajitahidi kuzingatia matumizi ya kondomu wanapokua na wateja wao pamoja na ugumu wa kazi zao. Kwenye kipengele cha afya wanaojihusisha na biashara hii hawaongezi mzigo kwa taifa kwa kusababisha ongezeko la magojwa kwa asilimia kubwa.
Suala la ukamataji na usambazaji wa picha za watu wanaofanya biashara ya umalaya ni udhalilishaji. Licha ya biashara hii kuwa haramu nchini watu hawa wana haki ya msingi na utu. Wengine wanafatwa katika nyumba za kufikia wageni na kupumzika “lodge” swali la kujiuliza Je kuna uhakika gani kuwa wanawake wanaokutwa kwenye hayo mazingira wote wanajiuza?
Katika upande wa Uchumi, takwimu za idadi ya watu walioko jela na mahabusu ya mwaka 2023 imepitiliza uwezo wa gereza kubeba watu. Wanaokamatwa kama ombaomba na wazururaji wanaongeza gharama ya kushughulika na jambo hili, gharama na nguvu kazi inayotumika zingewekwa kwenye mambo mengine ya kimaendeleo.
Uchambuzi wa wakaguzi kutoka magereza mwaka 2023 uliochapishwa na (TRT Afrika Swahili) umeonyesha jinsi baadhi ya Magereza nchini yalivyozidiwa uwezo kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa. Magereza yenye idadi kubwa ya wafungwa;
i.Ruanda (Mbeya) uwezo wa gereza ni wafungwa 400, idadi ya wafungwa waliopo ni 972.
ii.Mkuza (Pwani) uwezo wa gereza ni wafungwa 70, idadi ya wafungwa waliopo ni 165.
iii.Kongwa (Dodoma) uwezo wa gereza ni wafungwa 120, idadi ya wafungwa waliopo ni 158.
iv.Mahenge (Morogoro) uwezo wa gereza ni wafungwa 50, idadi ya wafungwa waliopo ni 62.
v.Ukonga (Dar es salaam) uwezo wa gereza ni wafungwa 945, idadi ya wafungwa waliopo ni 1157.
vi.Idete (Morogoro) uwezo wa gereza ni wafungwa 200, idadi ya wafungwa waliopo ni 231.
vii.Magu (Mwanza) uwezo wa gereza ni wafungwa 134, idadi ya wafungwa waliopo ni 140.
Takwimu hizi zinaonesha jinsi magereza ilivyolemewa hivyo ukamataji wa watu kwa kesi ya uzembe,uzururaji na umalaya ni upotezeaji wa muda na nguvu kazi ambayo ingetumika kuzalisha zaidi na kukuza uchumi tofauti na kwenda kurundika watu magereza ambao wanachokifanya hawaathiri Uchumi zaidi kuwafunga ni kuongeza mzigo kwa taifa.
Takwimu ya hali ya uhalifu ya January – Desemba 2020 iliyotolewa na ofisi ya taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha idadi ya watu 1472, wanaume 1336 na wanawake 136 hii ni idadi ya watu waliokamatwa kwa kesi ya uzembe na uzururaji. Mifumo na mazingira wezeshi yanahitajika ili kusaidia hawa watu kupata shughuli itakayosaidia kujikimu.
Ikifikia hatua watu wanatoa miili yao ili kupata kipato kwa ajili ya chakula hili linakua sio jambo tena la kutatua kwa kihisia libebwe kwenye upande wa kiuchumi kwamba huyu mtu ana njaa/ uhutaji usiovumilika. Mfano; Mwanamke anaejiuza maeneo kama za Buguruni, Mwananyamala au Sinza katika mkoa wa Dar es salaam kwa mtazamo wa haraka pesa anayopata ni kwa ajili ya kujikimu Na sio kwa ajili ya starehe.
Kuna haja kubwa ya kubadilisha sheria na kanuni hii kulingana na hatua ya kiuchumi tuliyonayo. Kwa kuzitambua changamoto wanazokutana nazo wanawake na kuweka mikakati ya kuwasaidia badala ya kuwanyanyapaa, kuhamasishaji elimu yenye mikakati ya kuwasaidia wanawake hawa kupata elimu na ujuzi wa kazi nyinginezo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Hivyo kama wataondolewa kwa nguvu kwenye biashara yao kuwe na namna mbadala ya kusaidia wao kupata kipato kujikimu kuendelea na Maisha yao.

Upvote
2