swaumu mohamedi
New Member
- Jun 21, 2024
- 3
- 2
Akili bandia ni nini? Huu ni mchoro wa ujasusi au roboti ambayo inajaribu kuiga kazi za binadamu zenye ubongo kwa kutumia aligorithms data iliyojifunza, kutokana na ukuaji wa technolojia akili bandia inaweza kutumika katika programu za kumpyuta ambazo zinaweza kufanya maamuzi ya kibinadamu au kutekeleza kazi ambazo hufanywa na binadamu, kwa mfano akili bandia ina uwezo wa kuiga sauti, pia inaweza kufanya kazi za kuzalisha vipindi katika tasnia ya habari na kusaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoitajika hivyo basi hakuna budi kuikubali katika sekta ya habari.
Picha kutoka kwa mkurugenzi wa ushauri wa teknolojia katika EPAM system inc
Kutokana na uwepo wa ukuaji wa technology nchini inatulazimu kuweza kuikubali hii technolojia ya kutumia akili bandia hasa upande wa habari na mawasiliano kwa umma
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UTUMIAJI WA AKILI BANDIA KATIKA SEKTA YA HABARI
# Nyumba za habari maarufu kama (media house) ziweze kuweka sera nzuri zitakazowezesha waandishi wa habari waweze kujifunza mbinu mbalimbali za kutumia akili bandia, kulingana na teknolojia iliyopo hatuna budi nyumba za habari ziweze kuweka matumizi ya akili bandia iwe moja ya sera katika zoezi zima la uendeshwaji wa vyombo vya habari, kwa kufanya hivyo husaidia kukusanya kwa taarifa kiurahisi hasa huwezesha kupata taarifa za kiuchunguzi katika tasnia ya habari
# Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA )iweze kurasimisha matumizi ya akili bandia katika sheria za utangazaji na kuweza kutoa njia salama zitakazowezesha matumizi ya akili bandia pasipo ubadhilifu wa taarifa au habari, kulingana na technolojia iliyopo endapo akili bandia itaweza kutumika vizuri katika uzalishaji wa habari pasipo taarifa za kugushi au kuingia usiri wa mtu itawezesha kazi za habari ziweze kwenda kuendana na teknolojia husika kwa sababu hatuna budi kuitumia
Picha kutoka BBC Swahili
# Pia TCRA iweze kutengeneza mitambo mbalimbali kwenye vyumba vya habari itakayowezesha kunasa taarifa sahii zilizoandikwa kwa kutumia akili bandia ambazo si sahii au zinaweza kuleta mtafaruko kwa watu, kupitia hii itasaidia kutumia hii teknolojia pasipo na shaka kwa sababu kutakuwa na uwezo mzuri wa kuangalia taarifa zitolewazo kwa usahii zaidi pasipi kuwa na uongo
# Pia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA iweze kuweka sheria nzuri zitakazomtetea wananchi na waandishi wa habari endapo litatoke tatizo kama hilo la ubadhilifu wa taarifa kutokana na matumizi ya akili bandia, kupitia hii itasaidia kwa pande zote mbili hasa kwa waandishi wa habari kuwa makini katika matumizi ya akili bandia na kuweza kuhakiki taarifa zake kwa mfano kuweza kwenda kwa muhusika mwenyewe ili kuweza kupata taarifa fasaha pia kuweza kuwafanya wananchi wawe huru katika utoaji wa taarifa zao
Picha kutoka BBC swahili
UMUHIMU WA AKILI BANDIA KATIKA TASNIA YA HABARI
Hurahishi kazi katika uaandaaji wa vipindi, hii hutoke pale waandishi wa habari wanapotafuta habari hasa zile habari za uchunguzi na habari za takwimu huwezesha kuweza kupata taarifa kwa urahisi kupitia kusearch katika mifumo mbalimbali ya akili bandia kama vile chatgpt na kadhalika pia akili bandia hutumiza katika kuzalisha kazi mbalimbali za video kwa kutumi capcut inakuwezesha wewe kuhariri video yako kwa matumizi zaidi
Pia akili bandia huwezesha kukua kwa tasnia ya habari, endapo itaweza kutumika vizuri akili bandia ina uwezo wa kuendesha shughuli za habari ambapo kutakuwepo na watu watakaowezesha kuendesha hiyo mitambo ya akili bandia na kuweza kupelekea ongezeko kubwa la ajira katika tasnia ya habari kupitia hivyo watu wataweza kujifunza kwa wingi teknolojia mbalimbali zitakazowezesha katika kufanya kazi za uandishi wa habari na kupelekea maendeleo katika sekta ya Habari
Pia akili bandia husaidia kukua kwa teknolojia katika tasnia ya Habari , hii hutoke pale waandishi wa habri wanapoweza kuchukua au kujifunza njia mbalimnali kutoka katika vyanzi vingi vya akili bandia na kuwawezesha kuweza kupata vitu mbalimbali vipya vitakavyowezesha katika utendaji wa kazi za uandishi wa Habari kutoka kwa wadau mbalimbali wanahusiana na mambo ya uandishi wa Habari
Pia katika vyuo mbalimbali vinavyowezesha kutoa mafunzo yanayohusiana na uandishi wa Habari husaidia wanafunzi waweze kutafuta mambo mbalimbali yatakayowawezesha wawe mahiri katika tasnia ya Habari na kuweza kuendesha masomo yao ya uandishi pasipo kuwa na shaka
HITIMISHO,
Palipo na maendeleo hapakosi kuwa na changamoto kama wasemavyo wahenga, kuwepo kwa akili bandia kwa upande mwingine husababisha baadhi ya nafasi za waandishi wa habari kuchukulia na kuweza kuendeshwa kulingana na uwepo wa mitambo ya akili bandia ingawa hatuna budi kuikubali kulingana na uwepo wa ukuaji wa sayansi na teknolojia nchini

Upvote
4