Ukuaji wa Teknolojia husababisha Upweke kwa watoto wadogo

Ukuaji wa Teknolojia husababisha Upweke kwa watoto wadogo

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Ukuaji wa Teknolojia ni Mzuri kama ukitumika vizuri. Kwa nini nimeleta hoja hii kwenu?

Unakuta wazazi wote wanachart karibu siku nzima watoto wanaolelewa humo ndani wanabaki kuzunguka zunguka tu. Mama hajali kuhusu watoto wala Baba labda akilia kidogo ndio washtuke kuangalia nini kimetokea.

Dada wa kazi nae anambembeleza mtoto huku akiwa na simu yake Mkononi. Mtoto anakuwa Mpweke kutwa nzima ama nae awekewe katuni. Wazazi tuamke kwa kuweka kipaumbele katika malezi kwanza.vingine baadae.

Zungumza na watoto wako kaa karibu nao,wasikilize na uwape muongozo wa maisha.
 
Kweli kabisa,majukumu wamepewa mabeki 3 siku hizi,yaani mtoto anamuona beki 3 ndio baba na mama yake
 
Back
Top Bottom