Ukubwa na udogo wa mishahara ni sababu ya rushwa

Ukubwa na udogo wa mishahara ni sababu ya rushwa

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Watu wengi tumekuwa tukiamini udogo wa mishahara ni moja ya chanzo au Sababu kubwa ya rushwa Jambo hili halihitaji akili kubwa kulielewa wewe vuta picha tu maisha ya leo alafu unakuta mtu analipwa laki tatu au nne mpka saba jumlisha ana watoto na mahitaji ya kila siku hapo ukikutana na mtu akakupa rushwa ni ngumu kukataa.

Sasa tuje upande wa mishahara mikubwa, Hapa nitatoa mifano Kuna kazi zinajulikana kuwa na mishahara mikubwa Kama ubunge , maofisa wa bandari, TRA n.k

Chukua mfano wa mbunge anayelipwa sio chini ya milioni tisa + sitting allowance n.k , Mshahara huu unapelekea mtu kutamani kuwa mbunge sio kwa sababu ana kiu na nia ya dhati ya kusaidia Jimbo lake bali ni kwa sababu ya tamaa ya mshahara mkubwa +uwaziri na ndio utaona wakati wa kampeni rushwa zilivyozagaa nje nje ili tu mtu apate nafasi ya mshara mkubwa nakama huamini embu leo hii itangazwe mishahara wa wabunge ni laki 9 au 8 as teacher au nesi anaye pambana kuokoa maisha ya watu kila siku uone hio fujo ya wabunge na idadi itakayo rudi 2025 kugombea.

Mwisho niseme suala la rushwa ni pana na lina Sababu nyingi, Kwani Kuna masala ya rushwa ya ngono, Ahadi ya cheo, pesa n.k unaweza toa maoni yako jinsi gani tunaweza punguza rushwa nchini. Asanteni
 
Mwenyewe nikifanikiwa Kuwa mke wa mtu tu,ubunge lazima niukomalie....ualimu unanididimiza...Kaz ngumu hela hasara hata kama Kuna Watu wanatafuta Kaz kama hii lakini nami ndo msiba wangu kiukweli.Mwanamke kijana ukiingia bila ndoa bungeni nasikia unakuwa KITAFUNIO😜
 
🤣🤣 vipi Kama ingekuwa wanalipwa laki 7 ungetamani kugombea
 
Muda ndio huu unasubiri nini mkuu

Back
Top Bottom