Ukubwa wa madirisha ya nyumba

Ukubwa wa madirisha unatakiwa uwe asilimia 25 ya eneo la sakafu (floor) mfano kama chumba kina urefu wa mita 3 kwa mita 3, floor area yake itakuwa ni 3m×3m = 9m²

25% ya 9m² ni 25/100×9m² ambayo ni sawa na 2.25m²

Kama utatumia dirisha la urefu wa futi 5 (1.5m), basi upana utakuwa ni 2.25m²/1.5m ambayo ni sawa na 1.5m

Conclusion
Chumba cha mita 3 kwa mita 3, dirisha moja la futi 5 kwa 5 linatosha kabisa au kama utapenda madirisha yawe pande mbili za kuta unaweza ukaweka mawili yenye upana wa futi 2.5

Kwa mahitaji ya ramani au makadirio kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Umepiga picha nyumba ya Khartoum ila ukashindwa kupiga nyumba yako wala ya huyo unayeita jamaa yako, umekusudia tujadili nini…. au tuchukue tu hilo hitimisho lako?
Hii ndio jf mzee kila mtu ana nyumba kila mtu ana mchongo wa maana kiufupi kila mtu humu mambo safi ila ya kufikirika
 
Banda apige nani? Sisi ni watu wa misonge tu. Onesha neno upana kwenye ile thread yako OG.
Comments za jokes zote zilizotangulia hukuona kosa lolote ila hii yangu ambayo nimewapa jawabu unanianzishia ligi...anyway umeshinda wewe, mi ndio nilikosea
Wakati mwingine ndio mana watu hawachangiagi mada sio kwa sababu hawajui, ni kwa sababu ya kuepuka vitu kama hivi
 
mkuu kwaiyo chumba cha 5 kwa 4 nikiweka madirisha mawili ya futi 5 kwa 6 hapo imekaaje
 
mkuu kwaiyo chumba cha 5 kwa 4 nikiweka madirisha mawili ya futi 5 kwa 6 hapo imekaaje
Ni sawa tu, chumba cha 4m kwa 5m kina 20m² ambapo 25% yake ni 5m²...madirisha mawili ya 5ft kwa 6ft yana jumla ya surface area ya 5.4m²..kumbuka hiyo 25% ni minimum, kwa hivyo inatakiwa ianzie 25% na kuendelea kutegemeana na mazingira yalivyo (joto sana/baridi n.k)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…