Ukumbi wa bunge maalum la katiba.

Yawezekana ila sidhani kwan tunaozijua bullet proof dah! Lakin bungen kuna nafasi za wagen kila kikao just try 2go even u ask for, nobody can sentence u!
 
Sasa hizo billet proof za nini bungeni na zinaashiria nini ina maana uaminifu na utulivu hautakuwepo!
Huo unashawishi matumizi ya hizo bulet .....!
Mmm hapo nna mashaka na hilo bunge letu inakuwa kama tuko Palestina!!
 
Yaani sijui kwa nini watanzania tunataka kufika huko. Ila ukiona hivyo ujue kwamba viongozi wetu wanatambua kuwa mambo wafanyayo si mazuri kwa jamii hivyo wanaanza kujenga uoga kwamba watu wanaweza fikia hatua ya kupigana risasi
 
Tanzania hatutapata katiba nzuri kwa vile imetayaraishwa kupitia process ya kisiasa zaidi badala ya kuwa process ya kisheria zaidi. Pesa nyingi sana zimetumika kuandaa upuuzi mtupu, tangu gharama za mchakato hadi gharama hizi za bunge maalum. Katiba hii ingependeza sana kama ingeondoa wanasiasa wote walio active au passive ndani ya vyama votena kuleta watu independent kabisa, na tena ingesaidia sana kama ingeongozwa na consultant wa kutoka nje ya nchi ili kuondoa bias.
 
Duuh ndani ya ukumbi wa bunge vioo ni bullet proof. Hii ni hatari.
Vitu vingine vinaitwa security details, huwa havisemwi!. Haya ni matokeo ya kufutwa kwa JKT, hivyo watu hawana tena uzalendo hati kutoa inje siri za kiusalama!.

Hivyo mtu akisikia kuwa zile gari za wale viongozi wakuu wa nchi na wakuu wa vyombo vya dola ni bullet proof!, atakuja humu kueleza!. Taarifa kuwa viongozi wakuu hupaswa kuvaa vest za bullet proof from time to time pia utazileta humu!.

Mwishoni utajikuta unaleta hata taarifa za shirika la posta, kuzifungua baadhi ya barua, kuziscan, kisha kuzituma zinakwenda as if hawajui kitu!. Mwisho utatoa taarifa za kampuni za simu, kuingilia mawasiliano ya baadhi ya simu, na kuyarekodi, ila kujinyamazia bila wenyewe kujua!. Hatimaye utatoa siri kwa baadhi ya mawasiliano ya e-mail kuwa intercepted through ip adress na kunakiliwa bila wenyewe kujijua!.

Vitu vingine huwa vipo ila havisemwi!.

Pasco.
 
Kwani ndugu Pasco hiyo ni kwa mujibu ya taarifa ya habari ya ITV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…