Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Katika Kitabu cha Matendo ya mitume 13:6 tunasoma;
"Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro (Cyprus) Walipofika Salama walihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Kiyahudi. Yohane alikuwa msaidizi wao.
Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo (Paphos) upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii....."
Huu mstari
ndio Key yangu sasa nianze tembea nayo
Sasa hapo tunaona Mwamba Paulo na Barnaba na Marko walikuwa sasa wametumwa Rasmi kuanza maisha kama wainjilishaji. Wakaenda mpaka kisiwa kinaitwa Kupro mjini Paphos
Kisiwa cha Kupros Kinapatikana Bahari ya Mediterranea unaweza kiita Kuprosi au Kipro, kwa Kiingereza Hutajwa kama Cyprus jina hili lilitokana na uwingi wa upatikanaji wa madini ya shaba wakati huo miaka ya Milenia ya 10 Kabla ya Kristu, Shaba Kikemia huitwa Kupri ndio maana na nchi ikajipatia jina hapo.
Mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji yote, mwaka 1570 waturuki Waosmani walifanikiwa kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya wenyeji, Na
Mwaka 1878 Uingereza ilianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914.
Sasa Tarehe ya 16 Agosti mwaka 1960 Kupro ilijipatia uhuru kutoka kwa Uingereza japo kulikuwa na utata wa Either Kupro kujitawala au kuungana na Ugiriki au kugawanywa kati ya kaskazini iliyo na utamaduni wa Kituruki na kusini yenye utamaduni wa Kigiriki, Mpaka leo hii Asilimia ya wakazi wa Kupro wanaongea Kigiriki na Kituruki, na asilimia 78 ni WA Orthodox.
Sasa Katika Historia na Maandiko safari ya kwanza ya Mtume paulo ilikuwa ni Kuelekea katika kisiwa hiki, Na Alipofika aliteswa katika mji wa Paphos na mahali alipoteswa iliwekwa nguzo ambayo ipo mpaka leo hii (St Paul Pillars)
Ndio ukumbusho uliopo kisiwani hapo karibu na Basilica la Agia Kyriaki, Na katika Site hiyo ndio panapatikana Mosaic ya mfano wa Sura ya Mtume Paulo, Kutembelea hapo ni Bure kabisa.