KWELI Ukungu unaweza kusababisha magonjwa kwa mazao au mimea na kudhoofisha mazao shambani

KWELI Ukungu unaweza kusababisha magonjwa kwa mazao au mimea na kudhoofisha mazao shambani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu wa JamiiCheck naomba kufahamu uhalisia wa hili kwamba ukungu unaweza kuathiri mazao na kupunguza kiwango cha uzalishaji. Huwa naona shambani majani ya mimea inaungua nikuliza wenzangu wananiambia ni ukungu je, ni kweli?
Screenshot 2025-01-30 100008.png
 
Tunachokijua
Ukungu kwa maana rahisi ni hali ya unyevu kwenye angahewa. Mara nyingi ukungu hutengenezwa wakati hewa yenye joto inapokutana ghafla na ubaridi kwenye uso wa ardhi na kupelekea kutengeneza matone madogo ya maji yanayoning'inia hewani na wakati mwingine matone huwa makubwa yanayoonekana, hali hii ya unyevu inawawezesha viumbe hai wanaojulikana kama kuvu (Fungus) kukua na kuzaliana kwa kasi na kiwango kikubwa.

Kuna hoja kwamba ukungu ni ugonjwa au huchochea magonjwa kwenye mazao na mimea mbalimbali


Utafiti uliochapishwa katika jarida la Agricultural and Forest Meteorology ukihusisha mimea iliyolimwa kipindi cha uwepo wa ukungu na kisichokuwa na ukungu ulibaini kuwa hali ya mimea kujitengenezea chakula chake (Photosynthesis), upitishaji wa hewa kupitia stomata vilipungua kwa asilimia 30% katika siku zenye ukungu ikilinganishwa na siku zisizokuwa na ukungu, hali iliyosababishwa na kupungua kwa mionzi ya mwanga inayofaa kwa usanidimwanga na halijoto ya chini wakati wa ukungu.

Tafiti zinabainisha juu ya kuongezeka kwa magonjwa ya fangasi endapo siku zenye ukungu zitadumu kwa muda mrefu. Pia, hali hii inapunguza kasi ya ueneaji wa wadudu wenye manufaa (wanaochochea uzalishaji) kwenye mazao, na hivyo kubadilisha muda wao wa kawaida wa uchavushaji. Ukungu huathiri kupenya kwa mionzi ya jua, ambayo ni muhimu kwa usanidi mwanga, na hivyo kupunguza viwango vya uvukizaji wa maji (evapotranspiration) na kasi ya usanidi mwanga kwa mazao mbalimbali.

Ukungu husababisha unyevu kujilimbikiza kwenye majani ya viazi, jambo linaloongeza hatari ya maambukizi ya fangasi na magonjwa. Endapo patakuwapo na theluji pia itasababisha seli za mmea kuganda, hali inayosimamisha ukuaji wake. Katika zao la viazi majivu kutoka jikoni yanaweza kutumiwa kama njia ya asili katika kulinda mazao dhidi ya ukungu na theluji. Majivu yanayotokana na kuni au kinyesi cha ng’ombe yana sifa asilia zinazosaidia kuweka mazao yakiwa na joto na kuyakinga dhidi ya magonjwa. Kunyunyiza majivu kwenye majani ya mmea huunda tabaka la ulinzi, hivyo kupunguza athari za ukungu na theluji.


Back
Top Bottom