Fantasia
JF-Expert Member
- Nov 19, 2017
- 1,071
- 832
DIWANI YA MZUKA
(Fantasma)
UKURASA WANGU
Uukumbuke ukurasa wangu
Eeh Bwana ukanirehemu
Kama mama na Baba yangu
Mwenye mamlaka chini na mbingu
Siijui kesho yangu
Huzuni nikimwangalia mwanangu
Nakuomba umsahifu
Tena ukumuafu
Katika kizazi hiki kichafu
Baada ya kuondoka kwangu
Mashetani wamevaa miili ya watu
Wanaabudiwa kama Mungu
Wamelinajisi hekalu lako takatifu
Na kuwaua Makuhani wako marahimu
Bwana
Katika Bibi na Babu zangu
Nimeomba kwa ajli ya Hawa ndugu
Nchi na Bara langu
Nchi nyeusi nchi ya miungu
Nchi takatifu
Tumefungwa makufuli katika vichwa vyetu
Bwana ukayafungue macho yetu
Nakurudisha ufahamu wetu
Tukakutane Tena kama ndugu
Katika hekalu lako tukakuabudu
Imhotep
Amenhotep
Menkaure
Amenehet
Ukatuondolee laana yetu
Ukaibariki nchi yetu
Kwa ajili ya Bibi na Babu zetu
Walioziweka Nadhiri nadhimu
Amenhotep
MOYO UKIVUJA DAMU
Siku fanya mambo machafu
Hasha! Nikawaudhi miungu
Bibi na mababu
Lakini moyo wangu umeumia
Kama umechomwa na miiba
Vile nimeingojea siku
Siku ya kufunguliwa kwangu
Kama ndege toka kwenye kifungo
Kuruka na kuchanua mbawa zangu!
Moyo umeuma
Umevuja Kama uzazi wa mtoto
Nimekulilia Mungu
Uitunze mimba yangu
Nisimpoteze mtoto huyu
Kubeba mimba ya uchungu
Kuja katika kuwa kwangu
Kuja katika kutokuwepo
Hata milele Ni chembe ndogo
Wala miungu haikuwepo
Nilipofanyika kuwa neno langu
Katika majeshi ya MIUNGU
Na huyu Ni Mungu mdogo
Na Amen wa Siri
Kuhani na wakili
Mwenye kuzishika funguo
Na Ameunet msema ukweli
Shahidi wa kweli na wa Haki
Nimeingojea Sana Alfajiri
Na mionzi dhaifu ya jua lako takatifu
Katika njia isiyo ncha
(Fantasma)
UKURASA WANGU
Uukumbuke ukurasa wangu
Eeh Bwana ukanirehemu
Kama mama na Baba yangu
Mwenye mamlaka chini na mbingu
Siijui kesho yangu
Huzuni nikimwangalia mwanangu
Nakuomba umsahifu
Tena ukumuafu
Katika kizazi hiki kichafu
Baada ya kuondoka kwangu
Mashetani wamevaa miili ya watu
Wanaabudiwa kama Mungu
Wamelinajisi hekalu lako takatifu
Na kuwaua Makuhani wako marahimu
Bwana
Katika Bibi na Babu zangu
Nimeomba kwa ajli ya Hawa ndugu
Nchi na Bara langu
Nchi nyeusi nchi ya miungu
Nchi takatifu
Tumefungwa makufuli katika vichwa vyetu
Bwana ukayafungue macho yetu
Nakurudisha ufahamu wetu
Tukakutane Tena kama ndugu
Katika hekalu lako tukakuabudu
Imhotep
Amenhotep
Menkaure
Amenehet
Ukatuondolee laana yetu
Ukaibariki nchi yetu
Kwa ajili ya Bibi na Babu zetu
Walioziweka Nadhiri nadhimu
Amenhotep
MOYO UKIVUJA DAMU
Siku fanya mambo machafu
Hasha! Nikawaudhi miungu
Bibi na mababu
Lakini moyo wangu umeumia
Kama umechomwa na miiba
Vile nimeingojea siku
Siku ya kufunguliwa kwangu
Kama ndege toka kwenye kifungo
Kuruka na kuchanua mbawa zangu!
Moyo umeuma
Umevuja Kama uzazi wa mtoto
Nimekulilia Mungu
Uitunze mimba yangu
Nisimpoteze mtoto huyu
Kubeba mimba ya uchungu
Kuja katika kuwa kwangu
Kuja katika kutokuwepo
Hata milele Ni chembe ndogo
Wala miungu haikuwepo
Nilipofanyika kuwa neno langu
Katika majeshi ya MIUNGU
Na huyu Ni Mungu mdogo
Na Amen wa Siri
Kuhani na wakili
Mwenye kuzishika funguo
Na Ameunet msema ukweli
Shahidi wa kweli na wa Haki
Nimeingojea Sana Alfajiri
Na mionzi dhaifu ya jua lako takatifu
Katika njia isiyo ncha