JamiiCheck
Member
- Nov 3, 2023
- 98
- 122
Upotoshaji hufanyika kwa njia nyingi ikiwemo kusambazwa kwa jumbe zinazodaiwa kuwa ni zawadi zinazotolewa na Mashirika ya kimataifa kama vile UNICEF na mengine.
Ukutanapo na taarifa za aina hii hakikisha unathibitisha kuona kama ni kweli imetolewa na chanzo husika ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi na kujiepusha na upotoshaji.
Mathalani JamiiCheck tulifuatilia madai aliyoyaleta mdau akitaka kujua iwapo taarifa iliyokuwa ikisambaa kuwa shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na masuala ya watoto (UNICEF) inatoa pesa kwa watu ila ili kupata pesa hizo unapaswa kuchangia pesa kidogo.
Baada ya ufuatiliaji tulibaini kuwa si kweli na shirika la UNICEF hlikuwa linatoa pesa kwa watu na kuwaonya watu kuwa makini dhidi ya Taarifa hizo. Tazama hapa