Ukwaju watajwa kuwa Dawa ya magonjwa lukuki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ukwaju ni tunda linalofahamika na asilimia kubwa ya watu duniani ambapo hulitumia kwa kula ama kutengeneza juisi. Tunda hili linalotokana na mti wa mkwaju ambao huota porini na unapatikana katika maeneo mengi ya nchi yetu ya Tanzania.

Watu wengi ambao hutumia tunda hili lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengenezea hasa juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha bila kujua endapo tunda hili na mti wake kwa ujumla una faida nyingi kiafya.

Lakini matabibu wengi na wataalam wa afya wamekuwa na mtazamo tofauti na kueleza kuwa mti wa mkwaju unafaida nyingi kwa binadamu tofauti na wengi wanavyodhani.

Mtaalam wa tiba asili, Dk Abdallah Mandai anasema mti huo unafaida kuanzia mizizi, magome, majani, na hata matunda yake huku akibainisha kuwa mti huo unategemewa katika tiba za magonjwa mbalimbali yanayowakabili wanadamu wengi hususani katika kizazi hiki cha sasa.

Dk Mandai anasema mizizi ya mkwaju ikitengenezwa vizuri huwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi likiwemo tatizo la mkojo mchafu (UTI) pamoja na kusaidia kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba, lakini pia humpunguzia mwanamke maumivu wakati wa hedhi au wakati wa tendo la ndoa.

Aidha, anafafanua kuwa majani ya mkwaju yanapoandaliwa vizuri husaidia sana kuzuia homa za mara kwa mara ukiwemo ugonjwa wa malaria, kuharisha damu, homa ya matumbo pamoja na vidonda vya tumbo na majani hayo yanapokaushwa vizuri kivulini kasha kupondwa na unga wake ukichanganywa na mafuta ya nazi husaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na mwasho.

Kwa wenye matatizo ya miguu kufa ganzi au kuwaka moto pia majani ya ukwaju ni tiba nzuri kwani unga wa majani haya ukichanganywa na mafuta ya nazi na kasha mgonjwa kuchua eneo husika maumivu huondoka kabisa.

Mbali na faida hizo unga wa majani ya ukwaju pia husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya pumu (athma), ambapo mgonjwa anapaswa kuchanganya unga huo pamoja na asali kisha kulamba jambo linalomsaidia kuondokana na hali hiyo pamoja na kifua kikavu.

Juisi ya ukwaju husaidia kuongeza vitamin A, B na C, lakini pia ina madini ya chuma, ‘calcium’ na ‘zink’.
Wataalam wa tiba wanasma kuwa endapo mtu ana shida ya kupata choo au tumbo kuunguruma ni vizuri kutumia juisi hiyo kwani husaidia kuondokana na matatizo hayo.

Kutokana na faida hizo watanzania wanashauriwa kuongeza juhudi za upandaji miti hii ambayo wengi wanaamini ni miti ya porini kwani inaweza kuzisaidia afya za watanzania wengi kuimarika bila kutumia gharama kubwa kununua dawa za viwandani.


hivisasa
 
Shukrani jazila

Tuyaache kama yalivyo
 
Kuna tiba nyingi za asili tunaweza kuzitumia na tukapona badala ya kutumia madawa yenye kemikali kama tiba.
Shukrani sana.
 
Ok

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…