Ukwel kuhusu biashara na bidhaa za forever living

Avatar

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
11,128
Reaction score
11,921
Ningependa tu share ujuzi juu ya hii biashara ya uuzaji wa bidhaa na kampuni tajwa apo juu, Je! kuna ukweli wowote na sio utapeli jamani???

Mwenye kitu tafadhali usisite kudondosha apo chini
 
Tafuta biashara nyingine achana na hiyo, ni ushauri tu.
 
Hao wazinguaji mambo yote Ni bf suma Ni pm km unahitaj kujiunga
 
Ushauri wngu:
Tafuta mtu ambaye anaifanya hiyo biashara kwa angalau mwaka mmoja. Muulize maswali/wasiwasi wako wote. Hpo ndo uamue kama inakufaa au la.
 
hii biashara inafanana sana kama siyo kabisa na hadithi ya kusadikika! ni sawa kabisa na kujirisha upepo! fanya ya kwako mkuu achana hao jamaaa kwamwe huwezi timiza ndoto zako bora ingia kwenye kilimo nk!
 
nimeangalia watu wanayo ifanya naona wamefanikiwa kweli eti..... wananunua magari seriously
 
Tafuta biashara nyingine achana na hiyo, ni ushauri tu.

katika moja ya semina zao waliitaja hii kuwa ni moja ya changamoto kubwa sana..... kukatishwa tamaa
 
jiunge uone.... mimi haya mambo ya kusadikika ndo simo kabisa... wewe lima green house utajirike
 
jamani hii biashara ya mtandao ni nzuri sana nimeanza kuifanya nilipomaliza shule mwezi 5, mpaka saiv wananiingizia si chini ya laki tano kwa mwezi kama bonus, pamoja na faida ninayoipata kwa kuuza bidhaa, nasubiria kwenda chuo na biashara yangu hii na sitegemei kuchukua mkopo wao, hapa naweza kuendesha maisha yangu vizuri, na kama upo dodoma nitafute nikupe details zaidi. Usikubari kusikiliza maneno ya watu walioshindwa maisha.
 
Fanya upembuzi yakinifu kuhusu hiyo kampuni, ulizia pia watu kadhaa ambao unajua wanafanya nayo kazi vinginevyo isijekuwa tatizo kwako baadae.
 
bf ni nini? mkuu

Ni kampuni ya network marketing inayodili na uuzaji WA dawa za binadamu ambazo Ni nzuri Sana kiukweli hii Ina tofauti na forever living na gnld kwanza kiingilio Ni 34000 Tu na unahitaji kuunganisha watu watano Tu PIA product zao Ni bei rahis
 
katika moja ya semina zao waliitaja hii kuwa ni moja ya changamoto kubwa sana..... kukatishwa tamaa

mkuu usiwasikilize watu,wengi wao humu hawana information sahihi wanahukum network marketing zote kwa kutumia mfano wamoja, hii Ni biashara km biashara nyingine inatakiwa ufanye kazi kweli ndyo utaona mafanikio hakuna hela ya bure bure
 
Ni kampuni ya network marketing inayodili na uuzaji WA dawa za binadamu ambazo Ni nzuri Sana kiukweli hii Ina tofauti na forever living na gnld kwanza kiingilio Ni 34000 Tu na unahitaji kuunganisha watu watano Tu PIA product zao Ni bei rahis

lakini forever haiitaji kiingilio,mtaji wako ndo kiingilio na faida ya kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…