Ukwel kuhusu biashara na bidhaa za forever living

mtaji laki saba siyo wote wanaweza kumudu
 
Fanya upembuzi yakinifu kuhusu hiyo kampuni, ulizia pia watu kadhaa ambao unajua wanafanya nayo kazi vinginevyo isijekuwa tatizo kwako baadae.

asante mkuu ndo nipo kwenye mchakato
 
Ni kampuni ya network marketing inayodili na uuzaji WA dawa za binadamu ambazo Ni nzuri Sana kiukweli hii Ina tofauti na forever living na gnld kwanza kiingilio Ni 34000 Tu na unahitaji kuunganisha watu watano Tu PIA product zao Ni bei rahis

mkuu iyo mi wala hata siijui sina reference ....
 
Ntumie namba yako pm nikutumie clip usikilze 4br yao kupitia whatsap
 
Okaka kwanza ndiyo utaweza kufanya biashara hii
 
Ningependa tu share ujuzi juu ya hii biashara ya uuzaji wa bidhaa na kampuni tajwa apo juu, Je! kuna ukweli wowote na sio utapeli jamani???

Mwenye kitu tafadhali usisite kudondosha apo chini

utapeli gani sasa wakati unaambiwa nunua bidhaa ukauze kwa faida?!! kupata kamisheni kubwa ni usuguaji wa soli yako tu, ukishinda unacharanga mitaa maofisini, au unaconvice rafiki zako wa fb kununua bidhaa huenda ukafanikiwa, mimi huwa naona ni upotevu wa muda tu, wanaojua marketing za mifumo ya piramidi wanaelewa kuwa daima wenye kufaidika ni wale wa mwanzo, kadri inavokuwa wale wa juu kazi inazidi kuwa ngumu na wanawafanyia kazi wale wa chini tu, bora hata ushike jembe ukapande mchicha utakulipa haraka!
 
mkuu usiwasikilize watu,wengi wao humu hawana information sahihi wanahukum network marketing zote kwa kutumia mfano wamoja, hii Ni biashara km biashara nyingine inatakiwa ufanye kazi kweli ndyo utaona mafanikio hakuna hela ya bure bure
Yap kazi kweli kweli ni kazi ambayo wa chini unamfaidisha wa juu,bidhaa ghali na ukikosa wa kuwaingiza kwenye chama basi we chini ndo utaendelea kusugua viatu.Walioingia mwanzo ndo walifaidi ila kwa wa sasa kama huna network imekula kwako.
 
Sio utapeli ila wa chini unataabika kumuneemesha wa juu.Mtoa post naamini wanaosapoti hii biashara wamekuja inbox ili angalau nao waongeze mteja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…