nimeshapangiwa tayari sasa nilipe yote au nilipe nusu?
nimeshapangiwa tayari sasa nilipe yote au nilipe nusu?
Kulipa au kutolipa yote kunategemea na huyo anayetakiwa kulipa hiyo mahari km ana huo uwezo kwa wakati huo. Km mahari siyo kubwa( una uwezo wa kulipa) lipa yote .
Kuna kisa cha bwana mmoja alifiwa na mkewe wazazi/wakwe wakataka mahari imalizwe kwanza ndipo marehemu azikwe au wakazike kwao. Usingoje yakukute.
Kwetu sisi, mahari hulipwa yote kama mhusika anaweza na kwa awamu kama hawezi kulipwa yote kwa pamoja,ila kuna makabila hii wanaona si sawa (ya kulipa kwa pamoja), wanaona kama kujionyesha fulani na visababu vingine vingi....!
Ndo maana nimekushauri uulize zaidi namna ambayo inakubalika,mbona rahisi tu mwambie mchumba wako aulize shangazi zake... au baba wadogo/wakubwa!
Habari wana jf,kuna jambo natatizwa nalo khs mahari,wengine wanasema mahari huwezi kulipa yote unapolipa lazima ubakishe na wengine husema mahari unaweza kulipa yote uliyopangiwa na hakuna tatizo,nipo njia panda katika hili naombeni ukweli kutoka kwenu wana jf.