Ukweli & historia ya Muungano. Ni muhimu kujua. Soma hapa.

Ukweli & historia ya Muungano. Ni muhimu kujua. Soma hapa.

T.Mwambungu

Senior Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
198
Reaction score
43
MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR:26-04-1964

>Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 09-12-1961,
Zanzibar 12-01-1964.

>Mwl.J.K.Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume walitiliana saini ya Kuukubali muungano tar. 22-04-1964.

>Mkataba uliidhinishwa tar.26-04-1964 na Bunge la muungano na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

>Viongozi kutoka pande zote 2 walikutana ukumbi wa Kalimjee Dar es salaam na kubadilishana hati za Muungano.

>Jina la muda la nchi undwa lilikuwa "JAMHURI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR"

>tar.28-10-1964 jina likabadilishwa na kuwa "JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1964, no.61

>tar.26-04-1964 sheria za Muungano zilipipishwa na Bunge likiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

>tar.27-04-1964 Wajumbe 7 wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge la Jamhuri ya Muungano.
Nao ni:Sheikh Abeid Aman Karume,Sheikh Idris Abdul Wakil,Sheikh Hasni Makame,Kassim Abdallah na Abdulrahaman Mohamed Babu.

>mwaka 1965 katiba ya muda ya Muungano ikapatikana na kuainisha mambo 11 ya muungano

MAMBO 11 YA MWANZO YA MUUNGANO.

~Katiba ya serikali ya muungano.
~Mambo ya nchi za nje.
~Ulinzi.
~Polisi na mamlaka yahusuyo kutangaza hali ya hatari ya nchi.
~Uraia
~Uhamiaji
~Mikopo na Biashara ya nchi za nje.
~Utumishi ktk Jamhuri ya Muungano
~Kodi binafsi ilipwayo na mashirika na watu binafsi
~Usafiri wa anga,posta na simu.
~Bandari
~Ushuru wa forodha,Ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini unaosimamiwa na Idara ya forodha.


>Katiba ya muda ya 1965 ilitambua mfumo wa chama kimoja yaani, TANU kwa Tanganyika na ASP Kwa upande wa Zanzibar.
Ilimtambua Rais wa Zanzibar kama Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya muungano, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano.

ONGEZEKO LA MAMBO 11 YA MUUNGANO NA KUFIKIA MAMBO 22

~1965, Mambo yote yanayohusu sarafu na fedha

>1967,kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikapelekea kuongezeka kwa mambo 3 ya muungano ambayo ni:
~Leseni za viwanda na Takwimu.
~Elimu ya juu
~Usafiri wa anga
~1968,Mambo ya Maliasili ya Mafuta na Mafuta yasiyochujwa.
~Bidhaa ya gesi asilia iliongezwa pia.
N.k

>Mwaka 1977,kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukafanya kuongezwa kwa mambo yaliyokuwa chini ya Jumuiya hiyo na kuwa chini ya Serikali ya muungano na kufikisha mambo 21 ya muungano.

>1992, Baada ya kuingia ktk mfumo wa vyama vingi, kukapelekea Jambo la 22 kuongezeka ili kuendana na mfumo mpya wa vyama vingi.

NINAWATAKIA SHEREHE NJEMA ZA MUUNGANO KWA WATZ WOTE WALIOMO NCHINI NA NJE YA TZ
 
Uhuru wa Zanzibar ulikuwa Disemba 1963 labda kama unamaanisha mapinduzi ndo yalikuwa 12 Januari 1964. Kwa maneno mengine serikali iliyochaguliwa kwa kura halali ilipinduliwa na kikundi cha watu wachache ambao wala hawakuwa na ridhaa ya Wazanzibari wengi.
 
Uhuru wa Zanzibar ulikuwa Disemba 1963 labda kama unamaanisha mapinduzi ndo yalikuwa 12 Januari 1964. Kwa maneno mengine serikali iliyochaguliwa kwa kura halali ilipinduliwa na kikundi cha watu wachache ambao wala hawakuwa na ridhaa ya Wazanzibari wengi.

HABARI YAKO TUYUKU?

>Unachokisema nikweli kabisa kwamba Zanzibar ilipata uhuru mwaka 1963.

>sikupenda kujikita sana ktk historia ya Zanzibar kwa sababu tunaongelea juu ya muungano.

>Lakini sinabudi kurekebisha pale unapoona pamekosewa licha ya kuwa ninaamini tukianza kuujadili uhuru wa Zanzibar na mapinduzi yake hatutamaliza leo.

KWAKIFUPI:

>Historia inasema kuwa waarabu wa Oman walianza kuingia Zanzibar mnamo mwaka 1832 na walipofika waliwakuta waafrika wakiwa na utawala wao chini ya Mwinyimkuu.

>Tangu mwaka 1832-1964 yaaminika kwamba kumepita takribani Sultan 11 baada ya kuuangusha utawala wa muAfrika wa Mwinyimkuu.

UHURU WA ZANZIBAR:

>tar.09-12-1963 Zanzibar ilipata uhuru (chini ya serikali ya mseto) iliyoundwa na vyama vya ZPPP na ZNP Ikiongozwa na waziri mkuu kwa misingi ya makubaliano ya "LANCASTER HOUSE"

>Hivyo basi Zanzibar huru haikuwa Jamhuri hadi pale yalipofanyika mapinduzi tar.12-01-1964 yaliyoing'oa serikali ya kisultan ya Jamshid bin Abdullah.
.
.
.
.
>(naomba niishie hapa kwa leo kwani dhamira yetu ni kuujadili muungano na ukweli wake)

>Kama kunamahara nimekosea turekebishane kwasababu hii ni historia ambapo kunamengi yata andikwa na kusimuliwa kwa namna mbalimbali.
 
Kuna kitu nilitaka niandike ila Basi nimeahirisha tu.. !

>Kitu gani hicho Mkuu??
Kukaa kimya ilihali unaukweli wenyemsaada haitosaidia.
>Hii nchi ni yetu sote, na ni wajibu wetu kuuweka ukweli bayana kwa manufaa yetu na kizazi kijacho.
 
::
Hivi kuna ukweli kuwa Karume alikuwa hapendi Muungano?
=
 
Back
Top Bottom