Ukweli Kuhusu Dragons


kuna siri ambayo hakupendezwa uijue kwa kuonesha udadisi wako.
 
Hapo itabidi usome agano la kale lote ufanye calculation kama nilizofanya mimi. Halafu unganisha na miaka ya sasa. Maana Yesu alizaliwa 4.BC, miaka ikiwa imeanza kupanda juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa mkuu... ila hiyo elimu ya calculation yako iko wazi au umebuni tu mkuu wangu!? Sidhan kama kunae anaejua mwanadamu wa kwanza aliumbwa lini kwamaana hata ukiifuata historia bado utapewa idadi ya miaka ya fuvu (predicted from death date) lakin haijasemwa ni lini mwenye fuvu alianza kuishi, sidhan kama uwazi ungekuwepo juu ya hilo mambo ya calculation yasingehusika hapa... Hesabu za kutafta x tuziache shule tuu. Bado ukihusisha vitabu vya dini vinasema
Mwanzo:1.:26-27
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Haikusemwa ni tarehe ipi, mwezi wala mwaka bali mwanadamu aliumbwa siku ya sita (6). Tusibuni taarifa. Ahsante
 
Ipo wazi mkuu inacheza miaka hiyo hadi karibia na 7000, hatujafikisha miaka 7000 mpaka sasa according to Bible.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
kujazia nyama kidogo..

kujazia nyama kidogo..

Your browser is not able to display this video.
 
Hapo ndio changamoto inapokuja, huko angani hakuna ramani tujue uelekeo mkuu. Ila ukifuatilia kwa umakini utagundua eneo ni bara la Asia.

Wanawafahamu sababu ya ile milima mikubwa kua mingi sana upande wao.
Ngoja na mm ntafuatilia nione

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahaihi, ni kweli kuwa hawa viumbe wamewahi kuwepo lakini kwa bahati mbaya wakawa extinct kabla ya binadamu wa kizazi chetu hiki cha sasa, kuanza kuishi. Kuna mmoja mifupa yake iliwahi kupatikana huko Tengaduruna Tanzania na watafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Idara ya Jiolojia, na sasa mifupa hiyo iko Ujerumani imehifadhiwa kwenye museum ya Berlin, kama sikosei.

Tukirudi kwenye Maandiko Matakatifu Biblia, ni kwamba Biblia inasema tangu Adam na Eva kuumbwa ni takribani miaka 6000 hadi leo, lakini Biblia hiyo hiyo ndiyo inayokiri kuwa Mungu hakuumba Ulimwengu siku ile ile alipowaumba Adam na Eva bali alikuwa tayari ameshaaumba kipindi kirefu huko nyuma, kama vile udong na miamba, katika muda ambao Biblia haitaji urefu wake. Alichofanya kipindi kile cha siku saba ambamo aliwaumba pia Adam na Eva, ni marekebisho ya kile alichokuwa tayari ameumba huko nyuma kama vile:

1. Kutenganisha maji na nchi kavu (maji na nchi kavu vilikuwepo tayari, hakuviumba siku hiyo

2. Kutenganisha anga na mbingu---hivi navyo vilikuwepo kipindi kirefu nyuma

Kwa hiyo ni sahihi kuwa kuna ulimwengu ulikuwepo kabla ya Adam na Hawa, na wana-Sayansi wanaofanya utafiti na kupata matokeo ya umri wa vitu ambavyo ni zaidi ya miaka 6000 wako sahihi na hawapingani na maandiko matakatifu ya kwenye Biblia
 
Gud[emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwenye mwanadamu kuumbwa siku ya Sita (6). Pana leta shida hasa ukisoma Biblia kwa intergration. Maana mungu alimuona Adam mpweke, siku Moja unaweza kujiita mpweke, tena ndiyo umetoka kuumbwa.

Adam alilala usingizi mzito, kuamka anamkuta Eva.(Hawa) siku hiyo hiyo ameumbwa, analala usingizi, analetewa Eva, Mungu anawaita Adam, siku alipowaumba.

Hapa huwa nakubalialiana kuwa kwa mungu miaka 1000 Ni siku Moja.

Kumbuka usiku na mchana uliumbwa na wenyewe, kabla ya usiku na mchana kuumbwa tulikuwa na giza tu, na nchi ilikuwa na vilindi vya maji ambapo giza ilikuwa juu yake.

Kumbuka pia Mungu kabla hajafanya uumbaji wa hii dunia alianza kuweka misingi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…