Ukweli kuhusu Gharama za ujenzi Stigler’s Gorge Power Project

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
9,710
Reaction score
2,240
Mwananchi la leo wanasema “Alisema kuwa wataalamu wa ujenzi wa mradi huo watatoka nchini Brazil na kwamba tayari makubaliano yamekwishafanyika kinachosubiriwa ni fedha na kiasi kinachohitajika ni Sh 4 bilioni.”
Wakati Daily news leo wanasema wanasema US $ 2 BILLION
MY TAKE

Daily news ndio wako sahihi as for the last 10 years tumekuwa twauongelea huu mradi ivi kweli 4 billion zingetushinda wakati ni ela za kawaida sana TZ kwa sasa ambayo ata wizi ni mwendo wa matrillion.
Gazeti la mwananchi huwa nawaamini katika facts pls kuweni makini maana hadhi yenu bado iko juu.
Wenzenu Nipashe wameona figure inawachanganya wakaamua kutoitaja.
 

Mkuu, hivi dola moja unapata madafu mangapi hivi sasa?
 
mkiambiwa tuna matatizo mnabisha na sasa ndio uanzie hapo kuona kuwa taifa zima limo katika mgogoro.
unaweza kusema Daily News wako sahihi lakini mimi nilvyoangalia tv jana usiku walisema $4 Billion, sasa unashindwa kujua kipi ni kipi.

Ila nakukumbusha kuwa Brazil sio kuwa ndio wanakuja kujenga, la, wanapewa ile sehemu na watadevelop then itakuwa kama ka-songas kengine maana wata-determine ni jinsi gani wawauzie tanesco umeme.

Na nimesikia mtu wa Mamlaka ya Bonde la Rufiji akisema kuwa hao wa-Brazil ndio walifanya feasibility study na mpaka sasa watz hawajui lolote lililomo kwenye hizo reports mpaka wakikabidhiwa mradi ndipo wata-disclose.
Na watu wa mazingira wanasema hii project itakuwa na matokeo mabaya sana kwa ecologia ya eneo lile na ukichukulia kuwa iko ndani ya mbuga ya Selous. Tusubiri tuone mwisho
 
Njowepo, umenisaidia sana kuleta bandiko hili. Baada ya kusoma MWANANCHI leo nilikuwa nataka kuja na uzi kuhusu gharama za mradi huu. Baada ya kusoma Mwananchi na gharama zao za 4 bn nikajiuliza hivi tumekuwa mabwege kiasi cha kushindwa kuwapa Tanesco hizo pesa ili gharama za umeme zisije kuwa juu sana baada ya mradi wa Stiggle Gorge kukamilika.
Jana kwenye taarifa ya habari Radio 1, walisoma USD 200! (mia mbili). Vyombo vyetu vya habari sometimes ni kichefuchefu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…