Ukweli kuhusu hali ya ajira nchini

Tanzania Norway

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2022
Posts
321
Reaction score
640
Mimi si mpenzi sana wa kuanzisha mada kwenye mitandao ila huwa nacomment kwenye mada hasa za mpira nakupita ila kuna hili la hali ya ajira nchini tunapoelekea nchi yetu itakuwa ya ajabu sana na kazi nyingi zitafanyika bila weledi na taifa litazidi kuwa na jobless na vijana wengi wa ovyo mtaani.

Binafsi nimezaliwa kwenye familia ya kawaida baba alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi sasa ni msaafu na mama ni mkulima na mfugaji(mama wa kisukuma) hivyo nayajua maisha ya chini na yakati sababu ndiyo level ya makuzi yangu kulingana na pato la familia niliyokulia.

Nimebahatika kuparangana kumaliza advnce na chuo na sasa nina kiajira cha kunipa ahueni ya maisha ila katika kuparangana nikiwa chuo had mtaani kbl ya kazi yangu ya sasa nimejifunza kuwa hali ya AJIRA NCHINI NI MBAYA SANA HASA KWETU VIJANA.

Ukiachana na hali halisi ya ugumu wa kupata ajira / kazi na vibarua ila watanzania wanatumika kwa ujira mdogo na kwa masaa mengi hata kwa makampuni na sekta binafsi ya ndan na nje ya nchi.

Nakumbuka kuna kazi ya muda mfupi nilipata kwa wachina tulikuwa kama watu kumi supervisor wetu alikuwa ni mmisri ile kazi tulikuwa tunaamuriwa kufika saa2 asubuhi hadi saa3 usiku yaani kazi unafanya muda mwingi umesimama au kumove muda wa kula ni dk45 tu saa6 na nusu had 7 na robo mchana hivo tulikuwa tunafny kaz kwa masaa 12+ hapo unatumia proffesional yako.

Siku moja nikamtolea uvivu supervisor kwenye kikao nikamuuliza kuna sheria gani ya kazi ambayo mfnyakazi anafnya kazi masaa12+ jamaa alichonijibu Ni kuwa kwani "Tanzania kuna sheria gani ya kazi akaongeza kama unaona kazi inamasaa mengi basi acha kazi wanaotafuta kazi wapo wengi kila siku tunapigiwa simu" nami nikamwambia sio kesi nilipeni siku zangu nlizofnya kazi niondoke zangu basi nikapigiwa hesabu wiki mbili nikapewa lak1.75 sababu T.salary ilikuwa lak3.5 .

Kiukweli nimefanya kazi za mtaani na ajira tofauti yaani nchi yetu haina mfumo rasmi kabisa kwa namna gani wananchi watafanya kazi zao na kufurahia ajira,si viwandani,si kwenye ujenzi,kwa watu binafsi yaani hali ni mbaya imefikia hatua shule binafsi sasa hivi tena shule kubwa tu mwalimu analipwa lak3 tena wa degreee tena hapo ni full time.

Mambo ni mengi unabaki kujiuliza nchi yetu inamifumo rasmi kweli,je,waziri wa ajira na kazi na wizara wanajua hali ilivyo,wapigania haki za binadamu je? Taasisi na wanasheria wa nchi je?

Kwa mifumo yetu Yaani kuna muda hadi wasomi wanadhihakiwa hadi na machawa,vijana wanadegree zao ila wanatamn wauze japo matikiti maji barabarani waepukane na ajira za kitumwa na kidhalimu.

Kama unatumia akili yako na elimu yako vzr ajira zetu nyingi Tanzania yetu hii ni miyeyusho.NGOJA NIISHIE HAPA MENGINE MTAMALIZIA NYIE
 
Kweli kabisa. Ni unyanyasaji mwanzo mwisho mfano Kuna kampuni la ulinzi Gardaworld( zamani kk security) aise Kuna jamaa zangu pale Kila mwisho wa mwezi wanalalamika mshahara unakatwa kuanzia elfu hamsini na kuendelea. Wakilalamika Kwa waajiri wao wanaambiwa waache kazi wapo wanaouhitaji huo mshahara na mazingira hayo ya kukatwa kiasi hicho bila sababu ya msingi. Kwa ujumla Tanzania ni kama kuku wa kienyeni tu utajua utakavyoishi. Mkipata muda mamlaka husika pitieni kwenye haya makampuni ya ulinzi hasa hasa kk security ya zamani na Sasa hivi ni Gardaworld.
 
Wa Bangladeshi wao wamejitambua.wamemfukuza rais wao na kwenda kujificha sababu ya kutoka ajira Kwa upendeleo.Wtz tu chukue hatua.
 
niliiwahi fanya kazi kwenye sekta binafsi Zanzibar aiseh nilijionea hayo yote ni hudhuni kwakweli
 
Kwahiyo suluhisho wadogo zako wakatae ajira wafanyaje bwana researcher ?
Kiukweli wizara inayoshughulikia ajira ianze kufanya kazi na iweke sheria from scratch mfano.unaweka sheria kam shule mnaajiri mwalimu wa level fln lazm mshahara wake uanze kias fln na kaz ifanyike kwa masaa 8 ya kazi sio kazi zinakuwa huria tu kiholela no value mfanyakaz anakuwa kam ng'ombe jambo ambalo sio sawa vivyo hivyo kwa vibarua
 
Kuna sehemu niliona walimu wa degree wanalipwa 160000/= aisee niliwaonea huruma sana..
 
Ajira hakuna sababu ya ujinga na aibu zetu

Mwijaku tunamuona chizi huku anaingiza mamilioni kwa kufanya upuuzi tu

Kina mc garab na wengineo wanaingiza mamilioni ya pesa sababu hawana aibu
 
Kama hauna aibu bongo fursa zipo nyingi sana


Watu wanauza mishkaki kariakoo kwenye mikokoteni wanatengeneza zaidi ya 30,000 kila siku

Na wengine wanauza matunda tu walioyakata kata na kuyapaki vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…