Ukweli kuhusu hali ya Mabenki Tanzania.

Duh! mambo haya yanawenyewe hiyo hoja ya kwanza nimetoka kapa!! nasubiri hiyo tathmini uliyotabiri hapo mwishoni
 
Mkuu kama wewe unafahamu hayo si utuelezee humu na sio kumponda mwenzio.

Lete hizo takwimu unazozitaka na sio kuzodoa na kuhoroja
 
katika hali yoyote ile ya kutapatatapa either kwa boti kuzama au kuanguka kwa uchumi, kuna makundi matatu huibuka...kundi la kwanza huweka mkazo kuwa uchumi uko sawia (Optimism) na kundi la pili huwa na mtazamo hasi (Pessimism) na kundi la mwsho huwa ni wale wenye mtazamo wa kineutrolali (Neutral). Uchumi ukijakuyumba hawajamaa optimist huwa wanakuwa na hali mbaya sana kisaikologia kutokana na kuonyesha udhaifu wao wa kuchambua masuala makubwa kama haya yanayoligusa taifa (Refer Global Economic Crisis). kwa suala hili la uchumi kwenda mrama si ajabu kumuona mtu kama huyu bwana mdogo akiinuka na kusema hali ya uchumi iko sawa (kwa ufupi ni kuwa huyu jamaa yuko U.S.A na sio Tanzania), pili ni mwanachama mtiifu wa chama kinachoongoza na ni mfanyakazi wa serikali (namwita middle income person). Nenda uendako wanaoanza kuonja joto la mtikisiko wa uchumi ni hawa lower income (unstable income earners) sio wenye kaliba za watu kama martin. Ndg mafuru alieleza wazi kuwa kuna liquidity problem iliyo sababishwa na serikali kuweka hela B.O.T na vile hawajaanza kurelease kwenye projects (NB. PM kalisema hili jana Arusha). wadau wengi mtaani wanakwambia hali ya uchumi haiko OK kutokana na mdororo wa biashara na viwanda kuonyesha nia ya kufungwa/kupunguza wafanyakazi (pessimist class). Kwa ushauri wangu huyu jamaa amalize masomo yake na arudi aendelee na kibarua chake
 
Mkuu The Tomorrow People umeongeza mkangnayiko badala ya kusawazisha mambo. Mimi naomba unisaidie majibu ya maswala machache kutokana na maelezo kwamba banks zinaoperate under prudential limits:

1. Kuna hoja kwamba hakuna tatizo la liquidity kwenye mfumo wa fedha nchini. Hili naomba tutofautiane tatizo la liquidity lipo na halisababishwi na serikali kuondoa pesa pekee zipo na sababu nyingine pia. Mathalani serikali imeondoa pesa na kupiga marufuku ufunguaji wa Fixed Deposit accounts kwa taasisi zake, biashara zimedorora (hii unaweza kuangalia data zako hasa performance ya service industry) na hata watu wenyewe wamekuwa wagumu kusave pesa bank. Kitendo cha kulipa accruing tax in one lumpsum kina maana ya kutoa pesa kwenye mfumo wa kibank na kuzizika BOT. Haya yote kwa pamoja yanapunguza amount ya bank deposit kuboost liquidity.

Kukataa kwamba liquidity ni tatizo ni kukataa kukubali dalili zinazojionesha kwa uwazi. Katika kikao cha taasisi za fedha na BOT, iliripotiwa kuna tatizo la liquidity na BOT wakasema watatoa fedha kunusuru hali hiyo. Kama wangekuwa wako within prudential limits, kwa nini BOT inatoa fedha kuboost liquidity? Na unahisi kwa nini wamesitisha kutoa mikopo au wenzetu hamsomi sababu ambazo wenye mabank wametoa?
 
ww umeatoa hoja kitaalamu kabisa lakini kuna wapotoshaji hawatataka kuelewa.
 
mdau mpya

...Huyo jamaa, haongelei uchumi kuyumba. Ukisoma sentensi ya kwanza, utaona anazungumzia hoja ya mabenki kufilisika. Na hilo amelitolea hoja hizo tatu.

king kan

...Unaposema, "biashara zimedorora (hii unaweza kuangalia data zako hasa performance ya service industry) na hata watu wenyewe wamekuwa wagumu kusave pesa bank." na kuhusisha hii na Serikali kuondoa kiasi cha fedha kwenye mabenki, huoni unaleta mkanganyiko?

...Hawana hela, wata save nini?

...Well, mi ntasema kwamba, mdororo uliopo kwenye biashara, unatokana na upungufu wa kipato (cha halali, and otherwise) cha wananchi. Hili limesababishwa kwa kiasi kikubwa na Serikali kupunguza au kuondoa matumizi, mazingira ya kibiashara kubadilika, n.k.

...Je, hali hii itapelekea mdororo wa uchumi? The jury is still out!
 
Kumbe na huyu ticha wangu chuoni yuko humu. Tumekusoma mkuu maelezo mazuri, ila watu kama nyie kwa serikali ya sasa hamna maana maana mnaweza kutoka mapendekezo mazuri ila yakatupwa kapuni.
 
Brother you were the best at the university 2005/2008 tunakukubali sana kipindi kile unasoma Finance Udsm,umetoa nondo nzuri
 
Lawrence Mafuru said exactly same thing.
 
Tumekuelewa sana mkuu na hata hiyo digirii yako ukiipata ni haki. Ila, ukirudi home, angalia sana usiajiriwe na sirikali hii unayotakiwa uiweke digiriii yako pembeni ujibu ka mlevi wa gongo.
Watu wanasema kiwanda flan kinafungwa kwa sababu hii, unasimama na kubisha kuwa sio kweli bali kinatengenezwa tu. Mwingine anaenda kuinua walevi huko na kuwavalisha makofia ya mainjinia na kuwauliza tu; Mmeona mali ghafi yetu. Wanajibu, ndiyoooo.
Kesho yake mnakubali kiwanda kile kimeshafungwa. Hata mtoe sababu gani, nani tena atakuamini kwani watu weshakuona kuwa mpiga dili??
Haya uliyo yasema, yangelielezwa tu kirahisi hivi ka ulivyo eleza, si watu wangelielewa?? Lakini mnasikia tu, Fedha ya serekali haina ruksa kuwekwa benki binafsi. No explanation, no what!! Ndo maana watu wanawaita wengine, madikteta. Kwa sababu, si wewe wa kuyatamka hayo. Waache uliowapa madaraka wayaseme. Jamani, msinielewe vibaya wakuu
 
Mtoa post umeandika mengi kwa utaalam kabisa. Nakubaliana na wewe kwamba sekta ya fedha nchini haina hali mbaya ya kutisha ila pia ni ukweli usiopingika kwamba kwa mwaka huu sekta ya fedha itapata matokeo mabaya kulinganishwa na mwaka uliopita. Na pia kumbuka kama umetumia interim results za mabenki ni kwamba hazipo audited, inabidi kusubiri final results ambazo zipo audited, kila benki inatakiwa kuzikamilisha by 31 March 2017.
 
This is yet another theory...maelezo ya kwenye karatas mengi tu kama ya mafuru na wasomi wengine "wa kukariri"...tufanye nini?...tusaidie...mohamed wa bangladesh came up with brac idea...he won nobel prize..uplifted lives of not only banglas..but of many other african and asian countries..hiyo ndio faida ya mchumi na financier...kama huna msaada unaandika andika tu..hata hapa mliman we have a bunch of ur like..hiding under the "thin" forest of "academicians"...go do ur assignment and come with smthn nobler..[emoji55][emoji55]
 
ka mkubwa we wa moto...
 
Naomba nijibu paragraph yako ya kwanza, haya mabenki kwa miaka kadhaa wamekuwa na hiyo mikopo isiyo lipika ika walikuwa wakifumbia macho kwa sababu hamna mtu alikuwa akifuatilia, nakumbuka humu jf palikuwa na thread kuhusu mikopo mibovu ya crdb na nbc hata kabla Kikwete hajamaliza muda wake, kwa mfuatiliaji mzuri wa hoja atakuwa alisoma, lakini pia siku ike JPM aliposhtukiza BOT aliliongelea hilo la usimamizi wa mabank kwa sababu ni kazi ya BOT na hawakuwa wakifanya kwa uadilifu unaotakiwa.
Sasa JPM alichofanya ni kuwataka BOT watekeleze majukumu yao na ndio maana huo udhaifu ukaonekana sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…