Ukweli kuhusu jiwe la ajabu Bosnia na ukweli kuhusu kutengenezwa na binadamu au kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi (asili)

Ukweli kuhusu jiwe la ajabu Bosnia na ukweli kuhusu kutengenezwa na binadamu au kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi (asili)

Joined
Mar 15, 2018
Posts
26
Reaction score
36
Mwanaakiolojia Sam Osmanagich maarufu kwa jina la “Bosnia indiana jones" alitamka kuwa jiwe la Bosnia ni jiwe la ajabu katika Bara la Ulaya , ambapo alieleza amefanya utafiti wa jiwe kwa miaka 15 , mwaka 2016 jiwe la Bosnia liligunduliwa katika.

Jiwe hilo lina upana wa mita 3 ambapo watengenezaji wa jiwe hilo hawakujulikana waliishi miaka 1000 iliyopita ila kunasababu nyingi za kuuliza na utata wa udunduzi wa jiwe hili la ajabu.
images.jpg


Kwanini ugunduzi wa jiwe hili lina umuhimu. Kwanza kuna ushahidi wa Ulaya ya Kusini, Balkan na Bosnia kuwa ni sehemu zilizoendelea mwanzoni kabisa katika masuala mbalimbali japo hamna rekodi ya zilizoandikwa kuhusu nchi hizo, pili walikuwa washaendelea kiteknolojia ukilanganisha na nchi zingine, pia walikuwa wataalamu wazuri wa Hesabu wengi tunajua ugumu katika Hesabu ya maumbo ya kijoemetri (geometry) umbo la tufe ni mojawapo ya maumbo yenye nguvu na magumu ni kama piramidi , matukio ya tumulus yanapatikana Bosnia.

Mwanaakiolojia huyo ameshafanya tafiti katika mawe mbalimbali makubwa duniani ikiwemo costa rica , jiwe la volkano mexico na kumalizia Bosnia ambapo amekili kuwa jiwe la Bosnia ni kubwa sana kuliko jiwe la Costa Rica na kufanya jiwe hilo kuwa jiwe kubwa liliotengenezwa na Watu wa Bosnia.

Lakini kuna baadhi ya watafiti walisema jiwe ilo halikutengenezwa na Mwanadamu bali mabadiliko ya mazingira yalitengeneza jiwe hilo ambapo Sauti ya America (V.O.A) waliwahi kutangaza kuhusu jiwe ilo na kusema halikutengenezwa na Binadamu.

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Manchester alizungumza na MailOnline kuwa jiwe lenye umbo la duara ni mfano tosha wa miamha migumu, miamba hutengenezwa katika hatua mbalimbali ambapo matokeo yake mara nyingi huwa na umbo la duara.

Sio kusema kwamba hamna Binadamu amabaye amewahi kutengeneza jiwe la duara linalofanana na mpira hapa duniani kuna moja ya jiwe maarufu duniani ambalo linapatikana Costa Rica ambalo lilitengenezwa kutokana na maendeleo ya binadamu wakati wa zamani ambapo kuwa duara halikutengenezwa kiasili bali ni Binadamu wa wakati huo ndio waliotengeneza.
images (2).jpeg


Wanaakiolojia duniani wameweza kufanya ugunduzi wa mambo mengi ya kale mfano kugundulika mji wa Pompeii, Olduvai George , Mji wa kale wa Jerusalem.

Tanzania tunajivunia uwepo wa jiwe lililotokana na kuanguka kwa kimondo ambapo linapatikana Mbozi , pia maajbu ya mawe yaliyobebana mkoani Mwanza.

Tuthamini vitu walivyo viacha Babu zetu wa kale huo ndio urithi wetu na asili yetu.​
 
Daaah watu kutengeneza mawe......inafikirisha Sana hii inaonesha watu wa zamani walikuwa na teknolojia kubwa
 
Back
Top Bottom