Ukweli kuhusu mgomo UDOM

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
Itakumbukwa kuwa serikali ilifanya kampeni kubwa juu ya suala hili mwaka jana 2014. Na ikasema imejiandaa vya kutosha kuwaendeleza vijana hao wa masomo ya sayansi ili wamalizapo diploma ya "chap chap" warudi kwenye shule zetu kuondoa tatizo la ukosefu na upungufu wa walimu wa sayansi.

Vijana hao walidahiliwa pale Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya programu hiyo lakini serikali haikuwa imejipanga kuwapa fedha za mahitaji muhimu kama ilivyohitajika. Taarifa kutoka UDOM zinaonesha kuwa, vijana hao wametangatanga na kuomba pesa za kula na kujikimu kutoka kwa wale "wakubwa zao" wanaosoma Digrii hadi imekuwa kero.

Unakuta kisichana cha miaka 17 au 16 kinasoma programu hii na hakijapewa pesa za vitabu, chakula na malazi. Kinazunguka kuwaomba wakaka wa digrii ili kiishi, nani kakipeleka kitoto hiki Dodoma? Baada ya vijana hao wanaotokea mikoa mbalimbali ya Tanzania kutaabika bila kupata msaada huku hawana pesa kwa muda mrefu, waliamua kuongozana kwenda kwa Waziri Mkuu na ama Mawaziri na viongozi wengine wa serikali ili suala lao litatuliwe. Wamekutana na ukatili wa kutosha kutoka kwa polisi, wengine wamevunjika na kuumia vibaya.

Mimi ambaye nimepitia misukosuko zaidi ya hiyo wakati naongoza UDSM na TAHLISO, nachoweza kusema ni kuwa vijana wa sasa na wazee wetu wa sasa, hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu. Tuna serikali isiyo na mipango na isiyo na haja ya kupanga na kutekeleza chochote "unresponsible government".

Iweje tupange kusomesha vijana kwa programu za dharura huku hatuna fedha za kuendesha program hiyo na hasa kutosheleza mahitaji ya gharama za maisha ya wahusika? Ni hivi karibuni tu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kwamba imeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi zaidi ya 20,000 kwa mwaka huu peke yake.

Nikukumbusheni pia kwamba, bunge la bajeti lililokamilisha kazi yake mwezi Juni 2014 tulijionea ripoti za aibu zikionesha kuwa kuna wizara nyingi tu ziliishia kupata 40% - 50% ya bajeti iliyopangwa. Haya yote ni dalili tosha kuwa tunaishi kwenye "taifa linaloangamia" (a failed state). Kwamba hatuna uwezo wa kupanga na kutekeleza mipango yetu.

Kwamba hatuna kipaumbele kwa yale tunayoyafanya. Watoto wa watu tumewadanganya, wameacha kwenda kidato cha tano na sita kwa nia njema ya kulisaidia taifa lao kutokana na vipaji na elimu yao, badala ya kuwalipa neema na mipango thabiti tunawalipa ubabaishaji, ukatili, nia ovu na jeuri. Vijana hawa wanaoteseka leo kwa ajili ya haki zao wanapata mafunzo makubwa sana.

Idadi ya vijana watakaoendelea kuichukia CCM inaongezeka kama mchanga wa baharini maana "Colonialism planted the seeds of its own destruction" – Hakika, hata CCM inapanda mbegu ya kujimaliza wenyewe. Poleni sana wadogo zetu, poleni sana wana UDOM maswayetu blog
 
Huku TPA wakipeana posho za 500,000 kwa siku.

Huku wengine wakibembelezwa kulipa kodi ya fedha ya ufisadi wa escrow.

Na wengine wakiwa na flight hours nyingi utafikiri ni Marubani!
 
Inasikitisha kwa kweli, poleni waathirika ukombozi upo njiani.
 
Mume anpoana mke aliyenaye ni matatizo humrudisha kwao.
Mke kadhalika anapoona Mume matatizo hujirudisha kwao. Ya nini mapambano.
Sasa hasara kwa nani?
Siasa za hadaa na kumwaga damu kila mwaka wa uchanguzi Mkuu.
Hakuna zaidi ya fitina tu.
CCM inaingiaje hapo!!!!
Aliye anzisha vurugu nani.
Kunatatizo Chuoni rudini makwenu shida ikipungua rudini Chuoni.
Kijana tetea fani yako achaneni na Siasa sio kimo chenu.
 
Inaumiza Sana

Vijana hao walidahiliwa pale Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya programu hiyo lakini serikali haikuwa imejipanga kuwapa fedha za mahitaji muhimu kama ilivyohitajika. Taarifa kutoka UDOM zinaonesha kuwa, vijana hao wametangatanga na kuomba pesa za kula na kujikimu kutoka kwa wale “wakubwa zao” wanaosoma Digrii hadi imekuwa kero.

Unakuta kisichana cha miaka 17 au 16 kinasoma programu hii na hakijapewa pesa za vitabu, chakula na malazi. Kinazunguka kuwaomba wakaka wa digrii ili kiishi, nani kakipeleka kitoto hiki Dodoma? Baada ya vijana hao wanaotokea mikoa mbalimbali ya Tanzania kutaabika bila kupata msaada huku hawana pesa kwa muda mrefu, waliamua kuongozana kwenda kwa Waziri Mkuu na ama Mawa
 
Hao walimu bila shaka hasira zao wataenda kumalizia darasani kwa watoto wetu. Poor my country
 
Dah... Nchi isiokuwa na mipango thabiti...ni shida ,hapa (udom) humanity Leo kuna kikao cha kawaida cha bunge la wanafunzi na tumeombwa wanafunzi kuhudhuria....too bad wameleta askari wanala landa kututishia amani badala ya kwenda kumweka Seth Singh chin ya ulinz ***shame on you mafisadi papa
 
watu ni wabishi wakiambiwa chama tawala kimechoka hawaelewi haya ndo matokeo sasa
 
Hakika,hizi ni siku za mwisho za CCM,matumizi makubwa ya vyombo vya dola,mauaji,ufisadi,uroho wa madaraka,...eee MUNGU OKOA TAIFA LETU!
 
Halafu viongozi wanafukuzwa, Philipo Mwakibinga,Rais wa chuo na spika wa UDOM wote wamefukuzwa,nini maana yake?
Umoja wetu vijana ndo nguzo kwetu ktk kuiondoa ccm mwaka huu ili vijana wapate elimu wanayoitarajia.
Mungu simama katikati yetu dhidi ya mashetani yanayotuangamiza ccm na serikali iliyo kandamizi na isiyojali utu wa binadamu.
 

Daaaaaah poleni sana. Fanyeni kama Yale ya cive mwaka 2011.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…