Ukweli kuhusu mgomo UDOM

UTAFITI ULIOFANYWA NA MASWAYETU BLOG KUHUSU MGOMO WA UDOM,HUU NDIO UKWELI,
MTAFITI :BLOGGER

Itakumbukwa kuwa serikali ilifanya kampeni kubwa juu ya suala hili mwaka jana 2014. Na ikasema imejiandaa vya kutosha kuwaendeleza vijana hao wa masomo ya sayansi ili wamalizapo diploma ya "chap chap" warudi kwenye shule zetu kuondoa tatizo la ukosefu na upungufu wa walimu wa sayansi.

Vijana hao walidahiliwa pale Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya programu hiyo lakini serikali haikuwa imejipanga kuwapa fedha za mahitaji muhimu kama ilivyohitajika. Taarifa kutoka UDOM zinaonesha kuwa, vijana hao wametangatanga na kuomba pesa za kula na kujikimu kutoka kwa wale "wakubwa zao" wanaosoma Digrii hadi imekuwa kero.

Unakuta kisichana cha miaka 17 au 16 kinasoma programu hii na hakijapewa pesa za vitabu, chakula na malazi. Kinazunguka kuwaomba wakaka wa digrii ili kiishi, nani kakipeleka kitoto hiki Dodoma? Baada ya vijana hao wanaotokea mikoa mbalimbali ya Tanzania kutaabika bila kupata msaada huku hawana pesa kwa muda mrefu, waliamua kuongozana kwenda kwa Waziri Mkuu na ama Mawaziri na viongozi wengine wa serikali ili suala lao litatuliwe. Wamekutana na ukatili wa kutosha kutoka kwa polisi, wengine wamevunjika na kuumia vibaya.

Mimi ambaye nimepitia misukosuko zaidi ya hiyo wakati naongoza UDSM na TAHLISO, nachoweza kusema ni kuwa vijana wa sasa na wazee wetu wa sasa, hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu. Tuna serikali isiyo na mipango na isiyo na haja ya kupanga na kutekeleza chochote "unresponsible government".

Iweje tupange kusomesha vijana kwa programu za dharura huku hatuna fedha za kuendesha program hiyo na hasa kutosheleza mahitaji ya gharama za maisha ya wahusika? Ni hivi karibuni tu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kwamba imeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi zaidi ya 20,000 kwa mwaka huu peke yake.

Nikukumbusheni pia kwamba, bunge la bajeti lililokamilisha kazi yake mwezi Juni 2014 tulijionea ripoti za aibu zikionesha kuwa kuna wizara nyingi tu ziliishia kupata 40% - 50% ya bajeti iliyopangwa. Haya yote ni dalili tosha kuwa tunaishi kwenye "taifa linaloangamia" (a failed state). Kwamba hatuna uwezo wa kupanga na kutekeleza mipango yetu.

Kwamba hatuna kipaumbele kwa yale tunayoyafanya. Watoto wa watu tumewadanganya, wameacha kwenda kidato cha tano na sita kwa nia njema ya kulisaidia taifa lao kutokana na vipaji na elimu yao, badala ya kuwalipa neema na mipango thabiti tunawalipa ubabaishaji, ukatili, nia ovu na jeuri. Vijana hawa wanaoteseka leo kwa ajili ya haki zao wanapata mafunzo makubwa sana.

Idadi ya vijana watakaoendelea kuichukia CCM inaongezeka kama mchanga wa baharini maana "Colonialism planted the seeds of its own destruction" – Hakika, hata CCM inapanda mbegu ya kujimaliza wenyewe.

Poleni sana wadogo zetu, poleni sana wana UDOM maswayetu blog
 
utafiti au maono tu? ila nawapa pole wadogo zetu na mungu awazidishie hasira za kuwachukia ccm wakati wote wa maisha yenu na vizazi vyenu amina.
 
Habari ndugu zangu wana JF?

Hivi jamani naomba kueleweshwa juu ya hili. Maana fupi ya serikali ni mimi, wewe na yeye kama ni kweli je serikali mambo iliyoyafanya UDOM ni sahihi? na kama sio sahihi basi serikali sio ya watu.

Msaada wa mawazo jamani.
Ahsanteni nyote.
 
Jamani wanachuo wenzangu wa UDOM hiv tumesahau ile kauli ya Mh. waziri mkuu PINDA? Ya WAPIGWE TU? MAANA TUMECHOKA SASA......... MY COUNTRY TANZANIA WHERE IS YOUR PEACE?????
 

Attachments

  • IMG-20150116-WA0004.jpg
    35.6 KB · Views: 294
  • IMG-20150116-WA0008.jpg
    117.9 KB · Views: 286
  • IMG-20150116-WA0003.jpg
    28.5 KB · Views: 274
watavuna walichopanda BAVICHA

Jitahidi kuimarisha uwezo wako wa kufikiri nje ya siasa kwa kufikiri mambo kwa kina.vijana waliahidiwa kupatiwa pesa za kujikimu na hawajatimiziwa mpaka kuamua kufuatilia haki yao wanaambulia mateso halafu wewe unangiza siasa hapa.vijana wamekosa majibu sahihi kutoka kwa waliohusika kutokana na nchi kushindwa kuwa na mpango mzuri wa kusimamia uwabikaji wakaamua kufuatilia kwa ukaribu ili kuwakumbusha wenyedhamana;vijana wakaishia mateso na wengine kupata vilema vya maisha.wakati huo huo waliosababisha vijana kuandamana hawaulizwi wala kujadiliwa halafu wewe mwenzetu unahusisha mambo haya na siasa.THINK BIG FRIEND
 
Kama maandamano hayasaidii mbona wametoa majina ya mkopo ambayo yanaonyesha yamefanyiwa malipo tangu tarehe07/01/2015
Mnao mpinga Mwakibinga mpingeni ila mungu anajua mchango wake ni upi katika kutetea haki za watoto wa masikini
 
Msilalamike Ovyo, chukueni hatua! Hapo inatakiwa ni mwendo wa kutoingia darasani hadi viongozi wenu warudishwe!
 
Kama maandamano hayasaidii mbona wametoa majina ya mkopo ambayo yanaonyesha yamefanyiwa malipo tangu tarehe07/01/2015
Mnao mpinga Mwakibinga mpingeni ila mungu anajua mchango wake ni upi katika kutetea haki za watoto wa masikini

Nachukia hawa wanaojiita watoto wa maskini. Kwanzia nasoma chuo nilikuwa nachukia mara eti ooh mi mtoto wa mkulima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…