Ukweli kuhusu 'Ndoa' ya Zari na Diamond

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kama wewe ni mmoja kati ya watu waliochukizwa au kuumizwa na taarifa kuhusu ndoa ya mastaa wawili wanao make headline kwa sasa, zarinah hassan aka zari pamoja na mpenzi wake diamond platnumz, taarifa ikufikie kuwa uvumi huo haukuwa kweli, diamond na zari "HAWAJAFUNGA NDOA"

Uvumi huo ulienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, mara baada ya mastaa hao kupiga picha wakiwa wamevaa mavazi ya harusi na kuzitundika kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa zinasema picha hizo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kuitangaza shoo kubwa ya super star kutoka uganda, ZARINAH HASSAN . Show hiyo inayotambulika kwa jina la CIROC ALL WHITE PARTY ambayo itafanyika kwenye ukumbi mkubwa pale MLIMANI CITY mei moja.

Zile picha walipiga kwa ajili ya kuitangaza show hiyo kubwa inayotabiriwa kuvunja record kwa kuhudhuriwa na mastaa pamoja na watu mbali mbali mashuhuli.
 
Zari n diamond
 
Attachments

  • 1428556228516.jpg
    53.6 KB · Views: 3,070
Hivi inakuaje mtu achukizwe au kuumizwa na ndoa ya watu ambao hana uhusiano nao??! Akichukizwa Wema au Ivan, naweza kuelewa kinyume chake ni kujitafutia stress za kujitakia!
 
Hivi inakuaje mtu achukizwe au kuumizwa na ndoa ya watu ambao hana uhusiano nao??! Akichukizwa Wema au Ivan, naweza kuelewa kinyume chake ni kujitafutia stress za kujitakia!

BInadamu tumeumbwa na dhambi ya asili, sio kila kitu wanachokifanya binadamu wewe utapenda ata kama hakikuhusu, ndivyo tulivyo binadamu ulimwenguni kote
 
Wema hataenda kwenye hiyo party
 
Hivi inakuaje mtu achukizwe au kuumizwa na ndoa ya watu ambao hana uhusiano nao??! Akichukizwa Wema au Ivan, naweza kuelewa kinyume chake ni kujitafutia stress za kujitakia!

Bora ivan ana haki ya kuumia kwa sababu ni mke wake, huyo wema si hawara tu kama walivyokuwa wanawake wote waliotoka na diamond, basi wataumia wengi
 
Wema hataenda kwenye hiyo party
Wema akiumia kwa kweli siwezi kumlaumu... we kasuguliwa miaka yote hii halafu aachwe kwenye mitaa! Anyway, nadhani Diamond alikuwa anakwepa ndoa ya mapema na Wema kwa kuhofia mambo ya pasu kwa pasu pale ndoa itakapoenda hali jojo!
 
Hivi inakuaje mtu achukizwe au kuumizwa na ndoa ya watu ambao hana uhusiano nao??! Akichukizwa Wema au Ivan, naweza kuelewa kinyume chake ni kujitafutia stress za kujitakia!

Ni kweli usemayo, ila huyu mwanamke mjanja sana atapiga sana pesa kwa kumtumia Diamond sasa taratibu naanza kuyaelewa malengo yake.
 
Bora ivan ana haki ya kuumia kwa sababu ni mke wake, huyo wema si hawara tu kama walivyokuwa wanawake wote waliotoka na diamond, basi wataumia wengi
Mpwa, hivi wewe hawala yako wa muda mrefu akaja kukupiga chini kisha akaolewa na mwingine hautaumia? Huyo Ivan nae itakuwa ni full maumivu coz' ka inavyoelekea, hata kama Ivan alimwacha Zari mwenyewe lakini alifanya hivyo huku akiwa bado anapenda... ingawaje mapenzi nayo ni ujinga mtupu... unaweza kuamua kumpiga mwenza wako chini kwa moyo mmoja lakini ukikuta mwingine anabeba, unaumia!
 
Wema akiumia kwa kweli siwezi kumlaumu... we kasuguliwa miaka yote hii halafu aachwe kwenye mitaa! Anyway, nadhani Diamond alikuwa anakwepa ndoa ya mapema na Wema kwa kuhofia mambo ya pasu kwa pasu pale ndoa itakapoenda hali jojo!

Ahahahaha apo nimekuelewa uliposema wema ataumia kwa kuwa ndiye mwanamke aliyechezewa zaidi na diamond kuliko mastaa wote, khaa!! Atajibeba, yeye si alijiachia ovyo
 
Ni kweli usemayo, ila huyu mwanamke mjanja sana atapiga sana pesa kwa kumtumia Diamond sasa taratibu naanza kuyaelewa malengo yake.

Kuna mtu aliwahi kusema, Diamond hamuwezi zari, ni mwanamke hatari sana na mwenye akili nyingi, sasa ivi anajipigia pesa tu kupitia jina la diamond, wema akili izo hakuwa nazo, tumuache zari afanye yake
 
Ni kweli usemayo, ila huyu mwanamke mjanja sana atapiga sana pesa kwa kumtumia Diamond sasa taratibu naanza kuyaelewa malengo yake.
For the time being, sioni atapiga vipi labda kama kweli kuna ndoa basi ndoa hiyo idumu kwa muda mrefu! Alipiga za kutosha toka kwa Ivan kwa sababu aliishi na Ivan kwa muda mrefu na ingawaje tangu hapo Ivan alikuwa na hela lakini ali-make zaidi alipokuwa na Zari na hivyo kuonekana kwamba utajiri wao ni kama umetafutwa na wote!

Lakini kwa hapa tulipo kuhusu Zari na Diamond, unless kama nilivyosema waende mbali zaidi, lakini kwa sasa Zari kila kitu amekikuta. Hata leo Zari akijifungua na kuthibitika kwamba mtoto ni wa Diamond kisha wakaachana, bado Zari hawezi kupata kitu... labda aombee Diamond afe, kisha Zari ale vya Diamond kupitia urithi wa mtoto! Wakiachana wakati ndoa haijafika mbali, sana sana atakachoambua ni pesa za matunzo ya mtoto! Mbaya zaidi, unless iwe vinginevyo, kwenye Uislamu hakuna "cha mali hii tumechuma wote" bila kuonesha tangible contribution kwenye mali husika unless kama ni suala la kurithi na sio ugawanaji baada ya ndoa kuvunjika!
 
Wema kinachomsumbua ni kupenda wanaume maarufu tu, apo kinachomsumbua ni kushuka kwa jina lake tu na kukosa mvuto kwenye jamii, ki ukweli sasa ivi wema hayupo kwenye line ya wema yule tunayemjua, zari ka take over everything, kama kungekuwa na mwanaume maarufu kumzidi diamond, basi wema angejiweka apo, ndicho kinachomuuma, sio kwamba ana mapenzi ya dhati na diamond ila umaarufu wake ndo unamchanganya
 
Ahahahaha apo nimekuelewa uliposema wema ataumia kwa kuwa ndiye mwanamke aliyechezewa zaidi na diamond kuliko mastaa wote, khaa!! Atajibeba, yeye si alijiachia ovyo
Hao wengine wote Diamond alikuwa anapita tu na sidhani kama yupo ambae alidumu nae kwa angalau mwaka... labda Penny lakini Wema, duh! Na ile style ya Diamond ya kutotaka kutoka na kushinda home tu, yaani watakuwa wamechakazana sana huku nikijitahidi ku-maintain heshima ya Wema coz' neno sahii hapo sio kuchakazana, bali...... atakuja kumalizia Heaven on Earth!
 
Last edited by a moderator:
Hivi inakuaje mtu achukizwe au kuumizwa na ndoa ya watu ambao hana uhusiano nao??! Akichukizwa Wema au Ivan, naweza kuelewa kinyume chake ni kujitafutia stress za kujitakia!

Wewe, hapa mtaani kwetu kuna team pwanya road alitaka kujiua kabisaa!
 
Diamond anajua kucheza na akili za watu, kashajua wabongo ni wambea, ivi diamond na zari si wote waislamu? Iweje wafunge ndoa ya kikristo? Bora ata mmoja angekuwa mkristo tungesema kamfuata mwenzie, ila wabongo sisi hatukufirikia hvyo, tukajua kushabikia tu ndoa dah kumbe changa la machp
 
Wema mjinga sana, na hata humu jamvini nimewahi kusema kwamba ni mjinga kwa kushindwa kutumia nafasi alipokuwa na Diamond! Wema kupitia nafsi yake ya uigizaji, kama angekuwa mjanja, angefanya mauzo sana ya filamu wakati yupo na Diamond! Kwa bahati mbaya, alidanganyika na maneno ya watu kwamba kuwapo kwa Diamond kunamtegemea Wema... kwamba Diamond anatembea na nyota ya Wema na mademu wengine, jambo ambalo mara zote humu nilikuwa nikipinga na leo ukweli umedhihiri... hakuna tena anayesema kwamba Diamond anatembelea nyota za Mademu bali mademu wenye akili kama Zari ndio wanatembelea nyota yake... jambo ambalo Wema alishindwa kulifanya ama kulitumia na kuishia kukatishwa maoni kwenye show!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…