Ukweli Kuhusu Nyumba za Bei Nafuu za Malipo Kiduchu Kila Mwezi Huko Kigamboni!!

Ukweli Kuhusu Nyumba za Bei Nafuu za Malipo Kiduchu Kila Mwezi Huko Kigamboni!!

Bon-CN

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2020
Posts
1,514
Reaction score
3,000
Inakaribia mwaka mmoja sasa mshikaji wangu wa karibu kabisa alipofika home na kuniambia kuhusu JPM kutaka kujenga nyumba za bei za nafuu kwa ajili ya wavuvi huko wilayani Kigamboni!! Ndugu yangu huyu akanieleza kwamba, wavuvi hao walitakiwa kufungua akaunti benki na kuweka kiwango cha pesa kisichofika hata 300K ili wawepo kwenye huo mradi.

Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu yangu huyu, idadi ya wavuvi waliojitokeza ilikuwa chache kuchangamkia hiyo fursa adimu, na ili kufikia malengo, coordinators wakalazimika kuwaingiza hata watu wengine ili mradi tu wawe kwenye mnyororo wa uvuvi, na magumashi mengine kibao!

Ndugu yangu huyu alinijia home ili kunitaka nami niingie!! Hata hivyo, hapo hapo nikamwambia wazi kwamba siamini hilo suala hata punje licha ya kunionesha mapicha picha ya kuchora kuhusu mradi wenyewe!! Ndugu yangu hakuacha kunikumbusha kila wakati kuhusu hiyo fursa!!! Mwisho majuzi akanikumbusha tena na kudai hivi sasa walengwa wanatakiwa kutoa pesa ndogo tu!

Bado sijashawishika, ingawaje nimefikia kujiuliza ni nini hasa kinamfanya mshikaji aamini uwepo wa huo mradi!!! Namjua, wala hana nia mbaya kwangu lakini nahisi ni kama sounds alizopigwa zimemuingia hasa!! Na kwa jinsi anavyonikumbushia kila wakati nahisi ni kama another form of network marketing!!

Kwa upande mwingine, angalau kwa asilimia chache, na kwa kuangalia msisitizo wa mshikaji, wakati mwingine huwa najiuliza "inawezekana hiyo kitu ni real hata kama hainiingii akilini"?!

Swali hilo la mwisho ndilo limenifanya nije jamvini ili kudodosa!! Je, kuna mtu yeyote anayefahamu lolote kuhusu huu "mradi"?!
 
Hakuna cha bure hata kikiwa bure kwako kuna mtu analipia...

Sasa kama umeshasema ni mradi wa kuwawezesha watu basi hao wawezeshaji ndio watalipia cost za huo mradi wote.., Kwahio its possible kitu kama hiki kufanyika (affordable housing) lakini tatizo hata la affordable housing sababu wanaoingia hapo kama ni watu wa chini sana wakashindwa ku-maintain hizo housing zinaweza zikapelekea kuwa ghettos.... Miradi mingi ya Affordable Housing / Housing for All inafeli hapo....

By the way sifahamu Case yako specifically lakini naongelea kwa ujumla if such a thing is possible (unaweza kuwapa watu hata nyumba bure..., ingawa ni bure kwao ila ni gharama kwa mlipa kodi / mlipaji sehemu nyingine)
 
Jambo la affordable housing ni la kawaida lakini mimi nilitaka kufahamu ukweli wa uwepo wa huo mradi huko Kigamboni!
 
Magufuli huyuhuyu aliyetunyima watumishi nyongeza ya mishahara kwa miaka 6 ndiye alitaka awajengee nyumba wavuvi?
Kuamini huo ujinga ni upuuzi
 
Nilikuwa na mawazo kama yako wakati Bitcoin ilikuwa $500 tu 2016, na nilikuwa na uwezo wa kuzinunua hata 25. Leo hii nabakia kujinyongea tu huku roho inaniuma[emoji22] huyo mvuvi akila hio fursa huto msahau maishani kama mimi sitoisahau Bitcoin

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Back
Top Bottom