Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 993
Sidhani kama kuna mtu hajui ukimwi nini,ishu ipo kwenye namna ya kuuepuka
Ishu zingine jukwaa la biashara linahusu!
Hivi na kampeni zote hizi kuna mtu ambaye haufahamu ukimwi na VVU? Sema sikio la kufa halisikii dawa!!!! Tunajua mambo yote sana ila sasa ile starehe yake watu tunajisahau sana. Gonjwa limekamatwa pabaya, pale watu tunapenda!!!
Mkuu, nime-edit post yangu maana nimegunduwa jana hamukuweza kunielewa vizuri.
Dah sikihitaji maana kitakuwa na lengo la kupotosha jamii, kama kinapingana na dhana kuwa V.V.U ndiye msababishi wa UKIMWI basi si kitabu chema.
Ukweli Kuhusu UKIMWI ni kitabu kinachotoa maelezo yanayoipinga dhana inayosema ugonjwa wa UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (V.V.U) kupitia maandiko kadhaa ambayo yameshaandikwa na wanasayansi wengine duniani kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika mfumo kwa kieletroniki na kusomwa katika kompyuta, tablet na baadhi ya simu zenye uwezo wa kusoma vitabu katika mfumo wa kieletroniki.
Nunua kitabu hiki sasa na upate majibu ya maswali hayo hapo juu. Ili kukinunua kitabu hiki bonyeza hapa.
Mkuu kirahisi hivyo? Nilidhani ungeeleza mwandishi wa hicho kitabu Ana sifa zipi, elimu yake, amewahi kufanya nini na wapi .
Pia ingekua vizuri kuonyesha kama kitabu kimepitishwa na Nani.(approved) hapo ndiyo Mtu anaweza akatoa 5000 yake kununua!
Kwa kifupi.
Mtazamo wangu.
Ni kawaida kabisa scientific process zote kupita michujo ya akili na test za wanasayansi wengi vizazi na vizazi.
Tunajua wote.
Na hakuna kati ya wanasayansi wote waliotajwa kwny hiko kitabu anaeinga ukweli rahisi. Au fact.
-UKIMWI hauna tiba
-HIV huambukizana kwa majimaji ya mwili hasa damu
-Uwepo wa HIV hupelekea ugumu wa kupona magonjwa ya kawaida kuwa mgumu zaidi
-kuwa na HIV sio terminal disease wala any disease by the way.
Asante kwa kitabu japo msome wale wenye interest ya kujua migongano ya kawaida ya wanasayansi katika kutafuta ukweli hadi chembe ndogo ili kujibu maswali yote. Kwa sasa bado haujapatikana.
Wote tujichunge tusiambukizwe hivyo virui au kama tunavyo tusiambukize wengine hasa vizazi vijavyo.
Ni kirusi ambacho kwa lifestyle yetu ya lishe ndogo, kupata na kuishi na maambukizo mengi ya kila aina km tb pneumonia nk inakuwa ngumu sana kupona. Ndio sababu unatupukutisha. Kwa kupata kinachojulikana kama UKIMWI.
Wewe acha kudanganya watu mkuu, wee fanya biaashara yako polepole tu.