Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
Iwapo ufahamu wako ndiyo kitu pekee kinacho-exists basi tambua ya kuwa wewe ni kila kitu na kila mtu. Katika nyakati fulani za wakati usiosemekana ulikuwa kila kitu unachokitambua. Ulikuwa jua, ulikuwa mwezi, ulikuwa nyota nakadhalika.
Wanasayansi wanakwambia kuwa ukubwa wa ulimwengu ni bazilioni, gajilioni ya miaka mingi isiyoesabika ya kasi ya mwanga... kivyovyote vile, hivi ndiyo ukubwa wa ulimwengu ulivyo, simamia vidole vyako vya miguu na jaribu kunyoosha mikono yako, na vidole vyako kuelekea angani usawa wa kichwa chako. Utabaini ukomo kuwa ni urefu wako na siyo ulimwengu. Maana yake nini kusema hivyo? Ukubwa wa ulimwengu unaoufikiria ni sawa na urefu wa mwili wako. Hivyo ndiyo ilivyo. Ndiyo tambua hivyo, daima ni kitu kilichopo mbele yako, mbali na upeo wako. Ndiyo ni mbali kabisa na matarajio ya mafikio yako.
Lakini huwezi kujua vyema jambo hili pasipo kujua kwanza juu ya UPALIZO na ngazi za ufahamu ambazo unapitia kama mwanadamu katika kuelekea kwenye hatua ya utambuzi halisi.
NINI MAANA YA UPALIZO (ASCENSION)?
Tunapotumia neno upalizo ni kama rejea ya namna ya kuupandisha/kuinua (elevating) ufahamu wa mwanadamu katika masafa na uhalisia wa mwelekeo (dimension) wa juu zaidi. Tunaweza kulitizama hili katika misingi ya madaraja ya kiufahamu katika mtiririko ufuatao; 3D, 4D, na 5D. Ubinadamu umekuwa ukiendelea kufanya kazi katika ufahamu au ulimwengu wa 3D kwa mamia ya miaka. Kadri jinsi ubinadamu unavyozidi kupokea mabadiliko ndivyo tunavyopanda kuelekea katika ufahamu wa juu wa 5D.
UFAHAMU WA 3D, 4D, 5D (CONSCIOUSNESS)
3D
Ufahamu wa 3D uundwa na daraja la chini, lenye masafa (frequencies) yenye mitetemo mizito (dense) na ufanya kazi katika njia mbili ya uwili(duality) na utengamano (separation). Watu wanaoishi katika ulimwengu wa 3D uwa na mtizamo finyu katika muktadha wa vitu vinavyowatokea na kuvitenda. Na uelewa wao huwa tu katika vile wanavyoweza kuvishika na kuviona kama vitu pekee vilivyo halisia kwao. Na maisha kwao huwa na muundo wa "The survival of the fittest" na katika ulimwengu huu unatambulika tu kwa jinsi ya mwonekano wako wa nje, kazi inayofanya, na gari inayoendesha. Katika daraja hili la ufahamu kuna programu nyingi ambazo ulazimisha/kushurutisha akili ya mwanadamu kutenda kwa namna zinavyotaka.
4D
Ufahamu wa 4D ni malango ya kuingilia ufahamu wa 5D lakini bado ni daraja ambalo ufanya kazi yake katika uwili (duality). Ni mwanzo wa kuanza kutambua kuwa nje ya kuwa wewe kuna la zaidi. Ufahamu wa 4D unaanza kukuamsha na kukujengea dhana ya kutambua kuwa kumbe sisi wote ni wamoja/tumeunganika (connected) na kuna la zaidi katika maisha na si tu katika yale yaonekanayo tu kwa macho. Na hapa ndipo tunapoanza kuwa wadadisi juu yetu wenyewe na kuianza safari ya kujigundua na hapo ndipo tunapoanza kuungana na kitu kingine nje ya sisi. Mara nyingi kitendo hiki ujulikana kama UAMSHO (Awakening).
5D
Ufahamu wa 5D uruhusu UPENDO na KUTOEGEMEA UPANDE WOWOTE (neutrality). Katika daraja hili la ufahamu hakuna uwili (duality) na hakuna jema (good) au baya (bad). Katika 5D hakuna ushindani wa chochote kile na sote utambua kuwa kuna vya kutosha katika ulimwengu kwa kila mmoja wetu. Unajihisi kujawa/kuijiliwa na hisia za upendo na huruma juu ya maisha, dunia na nyota. Katika daraja hili la ufahamu tunaishi huru pasipo masharti na tunaishi katika umoja "oneness" na sisi binafsi na wengine. Hatua hii ujulikana kama kujitambua "self mastery" na itatengeneza dunia iliyo na amani.