Ukweli lazima usemwe

Ukweli lazima usemwe

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Kuna mambo wanakikundi ni lazima tuwekane sawa, imeniuma sana na hata jana nilitaka niwapigie wanagroup niwaeleze waangalie hili swala linaweza kukomeshwa vipi. Mimi naamini kundi liliundwa kwa nia nzuri tu ya kusaidiana katika shida na raha na hata kushirikiana kufanya maswala ya kimaendeleo tupatapo fursa, sasa inapotokea kuna mtu badala ya kujikita katika maswala haya yeye anaona atumie mda huu kuchafua watu kwa masuala ya uongo na ya kutisha na ikiwezekana kuwakosanisha watu, Lazima ifike mahala tuheshimiane na hata kama kuna mtu amekukwaza basi usimfanyie kitu kibaya kitakacho mkwaza nayeye, utakuwa hujamsaidia ni heri umweleze kwamba anachokifanya siyo kitu kizuri na hukipendi hivyo usingependa kuona anafanya tena. kuliko kumdhalilisha kwa watu, Sasa nini kimenifanya nifunguke ni kwamba siku za hivi karibuni kumetokea uvumi mbaya sana kuhusu mimi, mwanzoni nilidhani ni story tu kumbe ni habari za kweli na anayevumisha ni mwanakikundi mwenzangu na nina muheshimu sana sana na huwa najifikiria nimemkosea nini mpaka akaamua kuanza kunichafua, ni mtu wa pili sasa ananipigia simu kwamba amepata habari toka kwa mwana group mwenzangu kwamba eti mimi sili pilau, Hebu fikiria huyu mtu ni mnyama kiasi gani kunizushia jambo la kutisha kiasi hiki hasa siku kama hizi ambazo sikukuu zimekaribia.
 
ha ha ha ... kweli sio haki kabisa mtu akuzushie jambo zito kama hilo
 
Back
Top Bottom