Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Kwa sasa mna timu ya kawaida sana, Tshabalala, Kapombe, Bocco, Nyoni na Mkude siyo wa miaka minne nyuma, Chama aliyerudi kutoka Morocco siyo yule alieondoka, pengo la Muqquison bado halijazibwa, wachezaji wenu wa kigeni ukiwatoa Innonga karibia wengine wote ni overrated. Usajili wenu ya wachezaji kwa miaka miwili mfululizo imekuwa mbovu sana.
Hapa kati mlijisahau na kujiona wakali kwa sababu kwenye mashindano yote ya ndani na kimataifa hamkukutana na timu za kuwapa upinzani thabiti. Wale wa Malawi na Waangola ni wabovu sana, hawafiki hata nusu ya ubora wa Al Hilal
Hapa bongo napo mkapiga wachovu wa mkiani wakina Dodoma Jiji na wa aina hiyo ila Azam wamefunua ubovu wenu. Jana mlizidiwa kwa kila kitu, sioni mchezaji wenu yoyote ambaye alikosekana jana angeweza kubadilisha matokeo.
Timu yenu inahitaji ukarabati mkubwa sana kufikia ubora wa timu aliyoiacha Pattrick Aussems kuanzia kwa Madam CEO mwenyewe. Na kwa huu moto wa Azam, KMC na Singida Big Stars msimu huu, sina uhakika kama hata tatu bora mtaingia, na Jumapili ni dhidi ya Mtibwa Sugar.
Jiandaeni kisaikolojia kwa lolote!