Pre GE2025 Ukweli mchungu: Bila Wasanii CCM itakuwa kama KANU, Wasanii ni Injini ya CCM tangu Mfumo wa Vyama Vingi uanze!

Pre GE2025 Ukweli mchungu: Bila Wasanii CCM itakuwa kama KANU, Wasanii ni Injini ya CCM tangu Mfumo wa Vyama Vingi uanze!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ukitaka kupima nguvu ya Wasanii angalia Sugu anavyokubalika Mbeya, angalia Prof Jay anavyokubalika Kilosa, angalia Babu Tale anavyokubalika Morogoro

Lakini zaidi angalia Freeman Mbowe anavyokubalika kwenye Siasa za Nchi yetu

Wengi hawajui Kwamba Komba rip na Mbowe ndio waliaminiwa na mwalimu Nyerere kusimamia Sanaa za Vijana na Siasa ambapo Mbowe alihusika na Kizazi kipya na Komba akapewa Vijana wa Bara waliopendelea Ngoma na Kwaya

Hivyo basi siyo rahisi CCM kuwepo au kushinda Uchaguzi bila Wasanii iwe wa Dunia au wale wa Nyimbo za Injili

Kwa sasa nguvu ya Wasanii inazidi kuwa kubwa na itafika wakati watazitamani Nafasi nyeti

Kama una macho angalia tu nguvu ya akina Mwijaku, Zembeela, Diamond, Harmonize, Baba Levo, Masanja nk hawa wanazurura Ulaya na Uarabuni bila Hata kusubiri wasafiri na Rais

Tunakumbushana tu 😂😂😂
 
Leo umeongea point kuhusu chama chetu. Ila hawa wasanii kukubalika kisiasa ni aina ya jamii tuliyonayo.
 
Back
Top Bottom