Ukweli mchungu Eng Hersi Said hatoshi kuongoza yanga.

change formula

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2020
Posts
729
Reaction score
1,559
Ukifatilia mtililiko wa matukio wa timu ya yanga,toka Eng Hersi Said awe pale kama mwenyekiti wa kamati ya mashindano na sasa ndie Rais wa yanga,unaona kabisa anakosa kabisa sifa na hana sifa za kuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa club hio kongwe hapa nchini.

Kuna sababu kubwa tatu ambazo zinamkosesha sifa za kuwa kiongozi mzuri,sote wenye akili tunajua yupo hio nafasi ya juu si kwasababu ya uwezo wake bali kwasababu ni mtumishi mwaminifu wa GSM,
ambaye kwa sasa ndio ameishika yanga,licha ya kuwa ni kit sponsor tu,ila amekuwa na nguvu sana ya maamuzi mpaka kufikia kumuweka mtumishi wake kwenye uongozi wa juu kabisa wa club hio kongwe.

Sababu ya kwanza ya kwanini Hersi Said hatoshi kuwa Rais wa yanga ni MAAMUZI! Eng Hersi kutokana na kuwa ni mtumishi wa GSM hawezi kuwa na maamuzi yeyote ambayo yatakuwa kinyume na msimamo wa mwajiri wake hata kama ataona maamuzi hayana manufaa kwa club ila kwakuwa yanakubalika kwa mwajiri wake ambae ni GSM itabidi hayakubali ili kulinda ugari wake kwenye kampuni,

Mfano mdogo jinsi anavyoshughulikua suala la Manara! Hawezi kuchukua hatua yeyote ya kimaadili wala kinidhamu kwa Manara hata kama Manara atafanya kosa gani!kwasababu yeye na manara wote wanamtegemea GSM
hivyo Hersi hawezi kugombana na mpambe wa bosi wake,hataishia kuumia tu lakini hawezi kuchukua hatua yeyote,maana manara yupo hapo kwa manufaa ya biashara ya bosi.

Jambo la pili ni MIEMKO ya ujana,Eng Hersi ni mtulivu ukimtizama usoni, ila ki uhalisia hana utulivu kichwani ana papala sana, hasa kutafuta popularity ili aonekane yeye ndie anafanikisha mambo mengi wakati ki uhalisia tunajua si yeye bali ni GSM ndie anakamilisha mambo mengi hapo yanga.

Jambo la tatu ni BUSARA: Hersi Said ameonyesha hana busara kabisa,kwenye maamuzi yake mfano suala dogo la kuwaweka yanga pamoja,yanga kama ilivyo timu kongwe ina misingi yake na taratibu zake,toka miaka mingi iliyopita, ni nadra sana kuona mwanachama wa yanga kwenda Simba na kupewa uongozi,au mwanachama wa Simba kwenda yanga na kupewa uongozi na kuwa na sauti kubwa kuzidi wale waliokuwepo miaka yote waliojitolea kwa nguvu zao zote!! Mfano leo Bumbuli hathaminiki hapo Yanga kama ilivyo kwa Manara!!

Ameshindwa kung'amua ujanja wa akili za manara ambae sasa hivi ameiingiza Yanga kwenye sintofahamu isiyo na ulazima na uongozi wa TFF!!na anachokifanya Manara si kwa ajiri ya manufaa ya Yanga bali ni kwa ajiri ya manufaa ya umaarufu wake,hali hii imewagawa wanachama na mashabiki wenye akili timamu wa Yanga ambao wanajiuliza uyo Manara ni nani mpaka awe juu ya mamlaka ya timu yetu,na anaetaka kuwa juu ya TFF kwa mgongo wa timu yao?

Kwasasa Yanga inatarajia kushiriki michuano ya kimataifa na ili ifanye vizuri lazima ifanye kazi vizuri na TFF,sasa kama Rais wa club anashindwa kutumia busara za kiongozi,timu inaweza kukosa ushirikiano wa karibu na mwisho kuishia kutolewa round za awali tu.

Mwisho Yanga ni taasisi kongwe ilihitaji ipate kiongozi aliekomaa kiuongozi na kibusara,wapo watu wengi sana hapo Yanga mfano kama Mh.Madega, Rais wa zamani wa TFF Mh.Tenga n.k Yanga ilihitaji vichwa vilivyotulia ila sio hawa vijana wenye miemko ya kijinga.

Yanga ni taasisi kubwa ni aibu leo mtu mmoja kutoka Simba,ambao wao walimfukuza uko, amekuja na kuwa juu ya watu wote hapo yanga kiasi kwamba kazi iliyopo sasa ni kumtetea yeye na ujinga wake!! Angekuwepo Marehemu Akilimali au mzee Ngozoma matunda na wazee wengine wenye msimamo wasingekubali timu yao kugeuzwa dekio la kupangusia matapishi ya Haji Manara.
 
Kwahiyo mama yako ndio anatosha?
 
Manara hafai kabisa. Yaani hajatulia kiakili. Nilishangaa alivyohadaiwa na Kiria eti aende mbele ya vyombo vya habari akiri na aombe msamaha. Akafanya hivyo kweli 💩. Hapa ni sawa na wale kipindi cha kukiri makosa ili walipe faini,eti wauza madawa ya kulevya nao wakakiri,matokeo yake wakala mvua za maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…