UKWELI MCHUNGU (GEN Z Hawataki Kusikia Lakini ni Ukweli 100%)

Home tutor Dar

Senior Member
Joined
Feb 23, 2025
Posts
126
Reaction score
156
1. School Won’t Make You Rich — But School Is NOT a Scam

Shule haikubuniwa kukufanya uwe tajiri.
Shule ilibuniwa kukufanya uwe mtu wa kawaida mwenye nidhamu, uwezo wa kusoma, kuandika na kufikiri.
Kufanikiwa ni kazi ya skills, mtaji wa mawazo, na maamuzi ya kiuchumi, sio tu cheti.
Cheti ni tiketi ya kuingia uwanjani, si ushindi wenyewe.

2. Wengi Hawana Pesa Sio Kwa Sababu ya Serikali — Ni Kwa Sababu ya Maamuzi Yao

Ukweli mchungu:
Watu wengi hawana pesa kwa sababu hawatoi muda kusoma vitabu, kujifunza market skills, au kutatua matatizo ya watu.
Wengi wanataka pesa ya haraka bila skills.
Hakuna shortcut.
Shortcut ni kufanya kazi kwa akili.

3. Kazi Uliyoisomea Haikuhakikishi Ajira

Ajira ni product ya:

uwezo wako,

ujuzi wako halisi,

attitude yako,

na uthubutu wako

Soko halijaapa kuajiri kila aliyehitimu.
Soko linaajiri anaye tatua problem.

4. Life Won’t Reward You because You Are “A Good Person”

Being good is NOT an economic skill.
Soko halina huruma.
Soko lina value.
Unalipwa kwa thamani unayoleta — sio tabia nzuri tu

5. Hustling Without Strategy Is Poverty in Costume

Kuamka mapema pekee haitoshi.
Kukimbia bila direction ni kama treadmill: unachoka lakini husogei popote
Strategy > Effort

6. Hakuna Mtu Atakusaidia Kama Hujajiendesha

Hakuna mjomba, hakuna shangazi, hakuna boss, hakuna mentor atakubeba kama mzigo.
Watu wanasaidia wanaoonyesha kujisaidia

7. Social Media Ikikupotezea Muda, Itakupotezea Maisha

Mtu wa TikTok 24/7 hana uwezo wa kushindana na mtu anayejenga skills 24/7.
Watu hawataki kusikia hivi — lakini ndicho kinachowatenganisha maskini na waliofanikiwa.

8. Mapenzi Hayalipi Bili

You can love, but you must also work.
Huwezi kutegemea emotions kukulipa rent.
Hata ndoa ina runs vizuri zaidi ukiwa na fedha.

9. Marafiki Wewe Unaochill Nao Leo—Watakucheleweshea Maisha

Ikiwa marafiki zako hawafanyi kitu cha maana, hakuna namna uta-develop speed.
Environment ni destiny

10. Huwezi Kuwa Tajiri Kwa Kufanya Ile Ile Inayofanywa na Kila Mtu

Ukitaka ordinary life → fanya ordinary things.
Ukitaka extraordinary life → jenga skills ambazo watu wachache wanazo.
 
Hayo yote hayawezekani kwenye taifa linalonuka rushwa,damu na ukandamizaji,CCM lazima watiwe adabu kwanza
 
Mna-copy and paste hizo lecture za wazungu bila kufikiria kwamba kule watu wamestaarabika kuanzia ngazi ya familia mpaka serikali na mifumo yao ipo well-organized.

Wapo watu ambao shule imewatajirisha. Anayofanya Elon Musk akujifunzia mtaani, alienda shule tena shule zinazoheshimika.

Upande wa serikali ina mkono wa moja kwa moja kukushusha kimaisha. Leo hii binti mdogo kama Niffer biashara zake zikifa utasema serikali haihusiki? . Unafikiri wale machawa wanaojizima data ni matahira? Wanafanya vile ili wasiguswe au wapate upendeleo na serikali.

Afrika inajulikana suala la mtu kufanikiwa ni randomly, sio systematically. Kwaiyo ukitoboa na wewe washike mkono kuwainua walio chini yako especialy ndugu zako. Mdogo ako yupo nyumbani ada ya shule imekosekana halafu usisaidie chochote eti "life won't reward you because you are a good person", totally bullshit.
 
Umemjibu vizuri sana vingine yupo right ila vingine huwezi toboa hata siku moja. Skills hazimtoi mtu ila uthubutu
 
Hayo mambo waambie watu wa miaka ya 80 huko, hawa Gen Z wengi wanachuma pesa nje ya elimu zao.

Sasa huu ukweli mchungu sidhani kama unawahusu sana.
 
Hayo mambo waambie watu wa miaka ya 80 huko, hawa Gen Z wengi wanachuma pesa nje ya elimu zao.

Sasa huu ukweli mchungu sidhani kama unawahusu sana.
Hawa motivational speakers michosho sana. Madogo wa gen z wanapambana katika mazingira ambayo hakuna kitu kilichoachwa kwa ajiri yao. Ajira, rasimali na njia za kiuchumi zote zimeshikiliwa na kizazi cha 80's kurudi nyuma. Dogo wa Gen Z bila connection hatoboi.

Kilichowashinda hawa madogo ni suala la maadili na mahusiano. Ila kwenye mapambano ya ku-survive madogo wanafight sana, especially madogo wa kiume.
 
"Home Tutor Dar" naona unafuata ushauri wako mwenyewe. Ila hautoaminika mpaka siku ukifanikiwa kwa kutumia njia zako hizo.
 
Kwa hayo maneno ntatoboa kweli nakata tamaa😔😢 siku zile zile maisha yake yale
 
Wanataka Samia awagawie Hela Kila mwezi
Sidhani na sijawahi sikia wakisema hivyo. Wanachotaka hao vijana ni equal opportunity most if haki.

Sio wanatafuta ajira halaf wanaona viongoz wanaweka familia zao position za juu huku wenye vigezo halisi wakibaki mtaani.

Wanajiona kutengwa nchini huku mamlaka ziki ignore sauti zao
 
It is easy said and written down kama ukivyofanya hapo wewe, than done.Umeassume everything is constant -
But in reality it is complex na ngumu.
Cha msingi ATAKAYEWEZA KUVUMILIA MPAKA MWISHO NDO ATAKAYESHINDA
 
Wanataka Samia awagawie Hela Kila mwezi
Hapana. Wanataka kuwe na mazingira mazuri ya kujiajiri katika sekta binafsi. Utitiri wa kodi za TRA. Tozo. Rushwa kila kona. Mtu unaanzisha kibiashara chako kinakufa maana mazingira siyo rafiki. Ajira hakuna. Na umesoma. Huku ufisadi wa mabilioni ukiendelea. Ukisema unatekwa na kuuwawa.

Vijana hawa siyo wajinga. Wasikilizeni. Wana hoja za msingi na kuwaua tu haisaidii maana hamuwezi kuwaua wote milioni 30+.

Samia yeye ale kwa urefu wa kamba na mafisadi wenzake lakini vijana hawa wanataka mazingira rafiki na uhuru kamili wa kuendesha maisha yao.

Is this too much to ask Miss Warda? 🤔
 
Sawa, maandamano yawe ya amani si mabomu tena mtatuua Kwa presha.
 
Sawa, maandamano yawe ya amani si mabomu tena mtatuua Kwa presha.
Wewe si uko Zenj ama? Huko si mnakula urojo tu kwa raha zenu huku mkifaidi utajiri wa wajinga wa Tanganyika?

Kwenye msafara wa mamba na kenge wako hivyo hooligans huwa hawakosekani. Na polisi wana mbinu nyingi kukabiliana nao mf. Risasi za mpira, maji ya Pilipili, mabomu ya machozi n.k..
 
I'm
Kuweni Walpole,mtaenjoy😃
 
Sasa hivi unavyotumia mfano JF app na tovuti ulijua vinatoka BAKWATA
 
Ww ni lijinga sana na kwa point zako za kijinga ndo zina zihirisha ujinga wako

Wanafunzi wanao anza darasa la kwanza 100,000 na katika hai wanafunzi 100,000 ni wanafunzi 30,000 ndo hufika vyuo vikuu na kumaliza elimu ya juu

Na unapoongelea ajira huwa kuna aina mbili za ajira Expert na ajira za kawaida
Sasa leo hii unataka expert akafanye kaz za kawaida sasa je hawa wengne wa ajira za kawaida watafanya nn

Leo hii unataka msomi wa degree akawe dreva boda, lori, fundi welding, sasa hawa ambao hawajafika elimu ya juu wakafanye kaz gan
80% ya wanafunzi wanaofika chuo kikuu husoma kwa mikopo kutoka serikalini afu mtu uyo anamaliza chuo unamwambia akajiajiri sasa km alikosa milion5 ya kusoma chuo atapata wap pesa ya kwenda kujiajiri

Kwa lugha ndogo 80% ya wasomi wa vyuo vikuu wametoka familia maskini wamesoma shule za serikal ambazo ni free na vyuoni wamesoma kwa mikopo afu wakimaliza wakija mtaa mnataka wajiajiri na km hawawezi kujiajiri bas wajishushe afanye kaz yyte ile sasa kurikua na umuhimu gan wa kumkopesha pesa za kusoma degree
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…