Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Kwa kweli utetezi mwingine hata hauna maana...eti kama makamu wa Rais hakuwa na chochote cha kufanya zaidi ya kuwa mtiifu kwa Magufuli!
Wapo wanaoenda mbali na kudai eti yako mengi hakuyaunga mkono ila ilibidi akae kimya ili yasimkute yaliyowakuta waliojaribu kumkosoa Magufuli!
Hata hivyo kuna wakati alidiriki kusema anayotenda Magufuli kama Rais hakosei na kwamba maamuzi anayochukua ni katika kutekeleza sera za CCM.
Kwa kifupi alikaa kimya kulinda usalama wake pamoja na kwamba baadhi ya Watanzania walikuwa wakitekwa, kuteswa na hata kupotezwa.
Kwa kweli Watanzania lazima tuanze kutafakari sana aina ya watu tunaowakabidhi madaraka makubwa ya kutulinda kama raia wa taifa hili.