Ukweli mchungu: Watanzania huenda tunaiongoza dunia kwa utii kwa Serikali yetu

Ukweli mchungu: Watanzania huenda tunaiongoza dunia kwa utii kwa Serikali yetu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari waumini wa JF,

Uzi huu hauna maudhui ya uchechezi naomba nieleweke.

Kila serikali inapopitisha sheria mpya ambazo zinagusa maisha ya Watanzania moja kwa moja wananchi wa Tanzania huiunga mkono Serikali yao.

Iwe sheria mpya ya kodi ambayo inawaminya mbavu, wananchi wataiunga mkono, iwe sheria ya umiliki wa ardhi, sheria ya uchaguzi n.k wanachi tunakuwa upande wa Serikali.

Naweza kusema kuwa Watanzania tunaiongoza dunia kwa utii.
 
Ukweli si utiifu bali ni uoga unaoletwa na Katiba iliyopo sasa.
Katiba tulionayo imeipa serikali nguvu kubwa sana kiasi kwamba raia wa kawaida anashindwa kutofautisha baina ya haki yake na utii wa sheria. Serikali imekuwa na mamlaka makubwa kwa raia kiasi kwamba yenyewe ndio yakuamua kipi ni halali ya raia na kipi ni fadhila.
Imefikia hatua ya kwamba serikali inaamua itakalo bila ya raia kuwa na uwezo wa kuhoji kutokujua ni haki yetu kuhoji. Utofauti wetu wa Tanzania na watawaliwa kifalme ni neno demokresia tu ambalo kiukweli hakuna hata hiyo demokresia yenyewe.
Lililo halali leo kwa utashi wa walio madarakani tu wanaweza kulifanya kuwa uhaini mfano mzuri mikutano ya kisiasa kuharamishwa kwa kauli ya uraisi tu, sio katiba. Hii inamaanisha kuwa kauli ya aliyekuwa madarakani ni sheria na ina nguvu kupita hata katiba. Sasa hapo unashangaa raia kuwa "watiifu"?
 
Sisi SUKUMA GANG ndo tumegeuka wapinzani Sasa wa kukosoa serikali.

CHADEMA,WANAHARAKATI NA WAPINZANI
wanasema mama ana upiga mwingi
 
Habari waumini wa jf.
Uzi huu hauna maudhui ya uchechezi naomba nieleweke.
Kila serikali inapopitisha sheria mpya ambazo zinagusa maisha ya Watanzania moja kwa moja wananchi wa Tanzania huiunga mkono serikali yao.
Iwe sheria mpya ya kodi ambayo inawaminya mbavu, wananchi wataiunga mkono, iwe sheria ya umiliki wa ardhi, sheria ya uchaguzi n.k wanachi tunakuwa upande wa serikali.
Naweza kusema kuwa Watanzania tunaiongoza dunia kwa utii.
Tunaongozwa kuwa takataka duniani
 
Heri apendayo Mungu, si unaona mambo yetu tunapomuachia Mungu ?
 
Sisi SUKUMA GANG ndo tumegeuka wapinzani Sasa wa kukosoa serikali.

CHADEMA,WANAHARAKATI NA WAPINZANI
wanasema mama ana upiga mwingi
Mbona anaupiga mwingi tu...Kwan wew unaonaje kiwango cha hizi tozo!!!! Si km Ronaldo na Mess eeh[emoji1787][emoji1787]
Lazima tuelewane, ccm mbeleeeee kw mbeleeeee
 
Back
Top Bottom