Ukweli mchungu

maramojatu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
1,749
Reaction score
2,319
Hamna haja ya salamu, ujumbe tu unatosha.
Baada ya miaka 5 -10 watoto tunaowapeleka na kuwarudisha shule kwa mabasi ya njano watakuwa wanaongozwa na waliosoma shule za umma. Hii itakuwa ni kwenye nyanja zote za uendeshaji uchumi, jamii etc.
Mtoto anapakiwa getini na kurudishwa getini. Anaishi mbezi kimara anasoma ubungo, hajui sinza, buguruni, mbagala etc. anamaliza kidato cha sita hajui kubadili gari afike Mbagala. Hii ni hatari.
Mbaya zaidi hajui kuuza pipi ya shilingi 100 apate 120. Hawezi kulima bustani zaidi ya kusoma mboga darasani.
Huyu ndio aje apambanishwe na anayeishi Mbezi suka na kusoma shule ya secondary Mbagala.
Thubutu!
 
Halafu elimu ya msingi ni ya kumuweka sawa mtoto kimsingi katika hatua fulani ya ukuaji,bado malezi yanaendelea na kubadilika hadi hapo atakapokuwa mtu mzima .
Unadhani akisoma kwa tabu ndio atakuwa mpambanaji?
 
Sema kuna watoto wanalelewa kimayai sana asee.....mtoto wa miaka 12 anavaa kiuna 34
 
Watanzania hatusongi mbele due to hii mentality ya ki stupidi stupidi ya kuamini kua watu lazma wateseke as if kuna certificates zinatolewa kwa mtesekaji hodari.
Mtoto anapanda basi ili apate exposure na misingi mbali mbali kwa ajili ya dunia inayoendelea.
Kujua kuuza pipi 120 from 100 haimfanyi awe kiongozi au mtu bora bali inambakisha kwenye ile quadrant ya self employed na kuvunja mgongo.
Pia mtoto kujua mitaa mingi haimfanyi kua street smart sana sana inamfanya a adopt mambo ya ajabu kama kucheza ngoma za mchiriku na kupiga chabo.
Suala n mzazi kumtengenezea mtoto msingi wa kimaisha na kuanzisha kitu ambacho ataendeleza sio kumuacha arande rande kama kuku wa kienyeji.
Wewe mtoa mada, una chochote ambacho mwanao atakuja kukiendeleza kiwe bora zaidi au unataka azunguke mitaani ili awe na akili kubwa ya ku bet kama yako?
Hopeless!
 
kwa msio muelewa mtoa mada,

hajasema kuhusu kumtesa mtoto, muelewe kusoma shule za serikali sio kumtesa mtoto

kikubwa ni exposure, mtoto wa gari la njano anakosa exposure na mazingira yanayomzunguka , anatoka nyumbani yupo getini anasubir bus ya shule na akirudi anaachwa hapo kweny kigeti, mtoto hajichanganyi kwa lolote la nje ya getin la nyumba.
 
Kwa kukusaidia ndugu. Maisha yote yanaelekea kwenye compyuta. Watoto wetu hawatatafuta in hard way mzee ila in soft ways. Mjaze mtoto elimu na maarifa tu ulimwengu unaenda kuishia kiganjan mwako
 
Inategemea unamuandaa mwanao kuwa nani huko baadae kwenye hii dunia ianupadvance kila uchao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…