Ukweli mtupu "Simba na Yanga zinabebwa!!!"

Nimekuuliza swali we zwazwa ila hujajibu unaendelea kuongea tu kama chizi, umewahi kuskia wao wakilalamika? Kwahiyo wewe ndio una akili sana kuliko wao? Umekazana kutoa mfano wa Azam confederation unajua msimu uliopita alichukua nani? Msimu wa majuzi alichukua nani?

Nimekwambia kuna mambo mengi ya kufanya sio lazima ulazimishe kuongelea kitu usichokijua, kwahiyo kutolewa Simba na Yanga kwenye Azam confederation ndo fair unayoongelea? Ss km huko wanaweza kuzifunga kwanini washindwe kwenye ligi? Au hao jkt wangekuwa wanacheza kwao ndo wangebeba kombe?

Stupidity katika kiwango cha lami yani hujui ata utaka nini, ruhusa kila mtu kuanzisha uzi ila uwe na uwezo wa kutetea hoja yako sio unaruka ruka tu, eti jkt washinde ligi kwa kikosi gani? Kocha gani? budget gani? Unajua kwanini Azam alishinda ligi? Unajua kwanini mtibwa alichukua ubingwa?

Nenda jukwaa la mapenzi huko, huku sio mambo yako mkuu
 

jazba kontena hoja kisoda " mapenzi km uchizi ukishapenda huoni wala huskii" msimu uliopita simba ni kweli alichukua ubingwa wa fa lakini fair ground ilikuwa haijaimarishwa km sikosei mechi za mtoano karibia zote alichezea taifa kasoro mechi mbili tu sasa hpo utaona ndyo yale yale ninayosema hta yanga msimu wa juzi mechi zote kachezea taifa kasoro mechi moja tu! now msimu huu kuchezesha draw kumekata mzizi wa fitna no mbeleko tht y wote wameangukia pua maana misimu miwili iliyopita walikuwa wanapanga ratiba kwa kuzi feva simba na yanga zicheze taifa ili wapate mapato now kuchezesha draw kumeleta fairness ambayo haikuwepo kitu ambacho ni kizuri kwa mtu anayependa maendeleo ya mpira wetu, ila kwa shabiki mandazi km wewe endelea kuleta ushabiki kwenye mambo ambayo hayaleti tija kwenye mpira wetu
 
Simba na yanga hazina uwanja, ule uwanja wa taifa kila timu inauhusu. Kila timu inaruhusiwa kuutumia kama uwanja wake wa nyumbani
 
Simba na yanga hazina uwanja, ule uwanja wa taifa kila timu inauhusu. Kila timu inaruhusiwa kuutumia kama uwanja wake wa nyumbani

ruvu shooting uwanja wao wa nyumbani unajulikana ni mabatini na timu zote za ligi kuu zinaenda kucheza pale kasoro timu mbili tu ambazo ni simba na yanga,sasa hpo utajiuliza kwanini ruvu wanapotaka kucheza na izo timu kubwa fasta wanashift toka mabatini mpk taifa? kwanini mabatini ni uwanja wao wa nyumbani wanapocheza na timu nyingine za ligi kuu kasoro simba na yanga?
 
Aisee, hivi we una hoja gani labda ambayo me sijaijibu kwa fact? Kwanini me nauliza maswali hujibu? Sasa hapo me nashabikia team gani?

Hivi hizo match mbili za simba na yanga ndio zimefanya jkt awe ile nafasi aliyopo kwenye msimamo? Anacheza na team almost 14 kwenye ligi hizo hazimtoshi angalau ata kumaliza top 4? Wakati mtibwa anachukua ubingwa team zilikuwa hazichezi taifa haya kwanini wao waliweza?

Ukweli ni kwamba huna hoja mkuu na ata kama utakuwa nayo basi umekosea namna ya kuiwasilisha, kigezo cha jkt kucheza taifa mach za Simba na Yanga haiwazuii wao kuchukua ubingwa hivo ni sababu ambayo haina kichwa wala miguu kwa sababu wao hawazuiliwi kushinda taifa kwanza wanakuwa na advantage za kushinda kwani wanatolewa kwenye kiwanja kibovu na kuletwa kwenye uwanja mzuri

Labda tu hujui Sheria za fifa ili uwanja uweze kutumika kwenye ligi unatakiwa kumit standard gani, kwa bongo hakuna namna tu ni lazima viwanja kama vya njombe, jkt, mtibwa, stand utd, nk vitumike kwakuwa hakuna namna ila vingi havijamit standard za fifa, na zote haziwezi kutumia uwanja wa taifa kwani utawahi kuchoka

Najitahd sana kukujibu kwa hoja na facts ila hutaki kuelewa umekazana tu na sababu yako, kuna njia nyingi za kubebwa kwa simba na yanga ila hiyo yako haipo kwani ina faida kwa team zote, huwezi kulalamika eti Yanga kabebwa kwa kuwaleta Njombe mji kucheza taifa utakuwa huna akili
 

Naona ushanielewa ila hutak kukubali na kinachonisikitishs zaidi huelewi kuwa timu kucheza ktk uwanja wa nyumbani mbeld ya mashabiki kuna advantage ya timu husika kupambana kupata matokeo ,....unasema sina hoja mi nishakwambia hoja yangu mimi ni fairness, kila mchezo kwenye ligi unahitajika kucheza kwenye mazingira yaliyo fair ili kuondoa hali ya upendeleo kwa baadhi ya timu.leo hii ruvu akicheza na simba kwenye uwanja wa mabatini approach yao ya mchezo itakuwa tofauti kbsa na wakicheza taifa ambapo wanakuwa wenyeji jina tu! mabatini ndyo uwanja wanaofanyia mazoezi kila siku ,ndyo kambi yao ilipo,so simba wakija wanakuwa serious wapo ugenini na sio hyo maigizo yanayofanyika taifa ruvu kuwa wenyeji wakati atmosphere nzima ya uwanja inaonesha kuwa ni wageni,......mwisho acha nimalize kwa kuuliza swali " kwanini timu 14 ligi kuu zinaenda kucheza ruvu manungu, mwadui kasoro simba na yanga? nipe sababu ambazo ni reasonable kwanini simba na yanga hazichezei ivo viwanja?
 
Dahhh kweli we jamaa mbishi sana, huo utaratibu ulipangwa tangu msimu uliopita game za jkt ruvu na mgambo game za Simba na Yanga zilikuwa zinachezwa taifa, hivo sio kitu kigeni nashangaa hukuleta huu uzi tangu msimu uliopita ila ukaleta hivi sasa

Reason sifahamu kwakuwa me sio muhusika either wa TFF, Simba, Yanga na wala ruvu ispokuwa nahisi zitakuwa ni sababu za kimaslahi zaidi kwani team za jeshi zimekuwa zikipata wakati mgumu kujiendesha ila issue kubwa ni kwamba umewahi kuskia ruvu wakilalamika?

Pia kwenye game za Simba au Yanga na hizo team ata zikiwa kwao still mashabiki wa Simba na Yanga waga wengi kuliko hizo team zingine, hivo eti kusema wakiwa nyumbani wanapata nguvu ya mashabiki sio kweli

Mzee kushinda ubingwa kunahitaji mambo mwngi na wala sio issue ya kucheza taifa, nimekuuliza kwanini mtibwa alishinda ligi hujajibu, nimeuliza kwanini Azam walishinda ligi hujajibu umekomaa na hoja yako mfu, huwezi kuchukua ubingwa kwa kuzifunga simba na yanga tu mkuu, kajipange uje uwasilishe hoja yako vizuri. Na sign out for good.

Mwisho kabisa jifunze kuandika vizuri unatupa kazi sana kusoma maelezo yako
 
very good critic indeed
 
Shikamoo Karie..penalty ya Simba Leo mmmh
 
Kwahiyo unataka manyema rangers Au Mbao FC wakacheze club bingwa Africa Acha zibebwe tu.....
 
Fair gani unazungumzia ww jombe mji, ombeni basi mechi za kimajaribio na timu za east africa tujue mko vizuri km simba na yanga zinabebwa, timu hata kula shida unakuja kubwabwaja hapa
 
Uyo shabiki maandazi atakuchosha hajui hata anaongea nn, nimemwambia km simba na yanga zinabebwa waombe mechi hata na APR ya Rwanda ili tujue wako vizuri
 
Mleta mada hujui soka, ama la hujatembea mikoani ukaona viwanja vyetu, ama la hujui ukata unaovikumba vilabu vyeti. Ficha upofu wako tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…