Ukweli na Uaminifu wa Maalim Seif

Ukweli na Uaminifu wa Maalim Seif

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MOHAMED GHASSANI AMEZUNGUMZA UKWELI NA UAMINIFU WA MAALIM

Nami naweka ushahidi wangu wa mapenzi waliyokuwa nayo watu Visiwani na Bara kwa Maalim.

Bahati mbaya sana mimi Allah hakunijaalia kipaji cha utunzi wa mashairi wala sauti ya kuyasoma mashairi asomavyo yeye.

Hatuchoki kumsikiliza, ''The Poet.''

Laiti ningekuwa na kipaji kama chake haya niliyosema ningeyatia katika beti na kuyasoma kama yeye.

Bila ya ukweli na uaminifu huwezi kufuatwa na umma ule uliokuwa nyuma ya Maalim hadi umauti ulipomfika.

Maalim seif hakujilimbikizia mali wala hakupenda vitu vya watu wala hakujivutia kwake kimiasha.

Amekufa akiwa hana hata nyumba ya kuishi ya kwake mwenyewe aliyojenga kwa pesa zake.

Bali maalim seif sijui hata kama alikuwa na Account ya Savings ya Bank yake binafsi.

Lakini alikuwa tajiri kwa vile alikuwa na watu nyuma yake, na walikuwa wanamtii na kmusikiliza Hakuwa na shida ya chochote, bali hakufikia kueleza shida yake ila wapenzi na wafuasi wake walimtatulia.

Aliishi maisha ya Utajiri huku akiwa ni Mnyonge asiye na chchote binafsi.

Kwa maana hiyo ndiyo maana alichukua myoyo za wengi, masikini na matajiri.

Maalim alijitolea maisha yake kutetea haki za Zanzibar, lakini wasaidizi wake baadhi walijaa unafik na undumila kuwili.

Uchaguzi wa 2010. kuna wasaliti katika Jimbo la Bubu waliuza fomu za matokeo ambayo kama zingalipatikana fomu zile kwenye uhakiki wa matokeo basi Maalim angelipewa nchi na kuwa Raisi wa kwanza wa serikali ya Umoja wa kitaifa Mpinzani.

Mwaka 2015 kuna namna ilifanyika ,na hatimae jecha akafanya unyama wake.

Na baada ya mazungumzo kufanyika, hali ilionesha kuwa mbaya zaidi, lakini Maalim alikubali Amani na kukosa kila kitu kuliko kuwa mshirika wa maovu.

Maalim alikwa na Moyo wa Chuma
 
Maalimu alikuwa mjanja mjanja,hakutaka kuwa Rais hata hao unaosema walificha fomu walikuwa na baraka zake

Maalimu angeamua kuwa Rais angekuwa,tena kitambo tu

Sema kila baada ya uchaguzi alikuwa akiitwa ikulu wakanywa gahawa na wale CCM akitoka huko amesalimu amri anaweka silaha chini, watu wamekufa na kuoata ulemavu kwa ajili yake ila hakuwa ngangari, hakuwa na msimamo.

Sijui walikuwa wanamtisha na nini
 
Maalimu alikuwa mjanja mjanja,hakutaka kuwa Rais hata hao unaosema walificha fomu walikuwa na baraka zake,
Maalimu angeamua kuwa Rais angekuwa,tena kitambo tu,
Sema kila baada ya uchaguzi alikuwa akiitwa ikulu wakanywa gahawa na wale ccm akitoka huko amesalimu amri anaweka silaha chini,watu wamekufa na kuoata ulemavu kwa ajili yake ila hakuwa ngangari ,hakuwa na msimamo.
sijui walikuwa wanamtisha na nini
Mdukuzi,.
Historia ya Zanzibar baada ya vyama vingi imetawaliwa na Maalim hadi anafariki.

Nimesoma hayo uliyoandika kuwa Maalim alishiriki katika njama za yeye kushindwa uchaguzi.

Lugha za ''gahawa,'' si mahali pake katika mjadala mzito kama huu.
Nimesoma kuwa Maalim ''alisalimu amri anaweka silaha chini.''

Nimesoma kuwa ''watu wamekufa na kupata ulemavu kwa ajili yake.''
Nimesoma Maalim hakuwa, ''ngangari hakuwa na msimamo.''

Unasema Maalim alikuwa ''anatishwa.''
Unasema hujui walikuwa wanamtisha na nini.

Tuanze na hili usilolijua kwani ni muhimu nikufahamishe hili usilolijua kwanza kisha tuingie hayo unayajua.

Dhima kubwa ya kiongozi ni kuwavusha watu wake kwa salama.
Si kuwaangamiza.

Kuuangamiza umma ni kitu kinachomtia hofu kila kiongozi makini.

Hakuna asiyejua historia ya Zanzibar na damu ambayo imekuwa inamwagika katika kila uchaguzi ukiondoa uchaguzi wa 1995.

Kuna faida gani kuwa chembelecho ''ngangari,'' damu ikamwagika.
Kuna starehe gani kukikalia kiti cha urais kilicholowa damu ya wananchi wasio na hatia?

Soma Macbeth William Shakespeare ujifunze hatari ya kuvaa taji linalovuja damu.

Hapakuwa na mtu yeyote wa kumtisha Maalim Zanzibar ila yeye akiwatisha wote.
Haingii yeyote na Maalim katika uchaguzi akamshinda.

Mtokeo ya chaguzi zote sita alizoshiriki Maalim ni nakala ya uchaguzi wa kwanza wa 1995.
Hayo mengine nimeyakalia kimya kwa kuamini kuwa haya niliyoandika yanatosha.

Nataka ujue kitu kimoja kuwa wote waliouiwa na kupata ulemavu hayakuwakuta hayo kwa ajili ya Maali,

Yamewafika yote hayo kwa kuipigania nchi yao Zanzibar.
Tusimame hapa.

Ikiwa una mengine Ahlan Wasaalan.
 
Mdukuzi,.
Historia ya Zanzibar baada ya vyama vingi imetawaliwa na Maalim hadi anafariki.
Nimesoma hayo uliyoandika kuwa Maalim alishiriki katika njama za yeye kushindwa uchaguzi.

Lugha za ''gahawa,'' si mahai pake katika mjadala mzito kama huu.
Nimesoma kuwa Maalim ''alisalimu amri anaweka silaha chini.''

Nimesoma kuwa ''watu wamekufa na kupata ulemavu kwa ajili yake.''
Nimesoma Maalim hakuwa, ''ngangari hakuwa na msimamo.''

Unasema Maalim alikuwa ''anatishwa.''
Unasema hujui walikuwa wanamtisha na nini.

Tuanze na hili usilolijua kwani ni muhimu nikufahamishe hili usilolijua kisha tuingie hayo unayajua.

Dhima kubwa ya kiongozi ni kuwavisha watu wake kwa salama.
Si kuwaangamiza.

Kuuangamiza umma ni kitu kinachomtia hofu kila kiongozi makini.

Hakuna asiyejua historia ya Zanzibar na damu ambayo imekuwa inamwagika katika kila uchaguzi ukiondoa uchaguzi wa 1995.

Hapakuwa na mtu yeyote wa kumtisha Maalim Zanzibar ila yeye akiwatisha wote.
Haingii yeyote na Maalim katika uchaguzi akamshinda.

Tusimame hapa.
Ikiwa una mengine Ahlan Wasaalan.
Mimi naamini maalim alishinda chaguzi karibia tatu au nne au zote kabisa,angesimama imara leo CCM ingekuwa chama cha upinzani Zanzibar, kuna vyama bila kuwa ngangari havitoki madarakani, lengo la chama nikushika dola, raia walikuwa tayari kwa lolote ili mradi haki ipatikane.

Kwa sasa juhudi zake, uadilifu, vimekwenda nae, sioni CCM ikikosa tena usingizi kipindi cha uchaguzi. Maalim angetaka kuwa Rais angekuwa. Usipokuwa aggresive huwezi kufikia malengo yako ya kisiasa
 
Mimi naamini maalim alishinda chaguzi karibia tatu au nne au zote kabisa,angesimama imara leo ccm ingekuwa chama cha upinzani zanzibar,kuna vyama bila kuwa ngangari havitoki madarakani,lengo la chama nikushika dola,raia walikuwa tayari kwa lolote ili mradi haki ipatikane
Kwa sasa juhudi zake,uadilifu,vimekwenda nae,sioni ccm ikikosa tena usingizi kipindi cha uchaguzi.Maalim angetaka kuwa Rais angekuwa .usipokuwa aggresive huwezi kufikia malengo yako ya kisiasa
Mdukuzi,
Ahsante sana.
Naamini wako walionufaika na haya maneno yako.
 
Mdukuzi,
Ahsante sana.
Naamini wako walionufaika na haya maneno yako.

..hili la Maalim Seif kushindwa kutetea ushindi wa chama chake hata mimi linanishangaza.

..Na kwanini mara zote kulipotokea matatizo ya uchaguzi Maalim Seif alikwenda peke yake kujadiliana na viongozi wa Ccm?

..Kwanini Maalim kuwashirikisha viongozi wenzake wa Cuf kujadili matatizo ya uchaguzi kama ambavyo Ccm walikuwa wakifanya kila wakati?

..Na hoja kwamba Maalim Seif hakutetea ushindi wa Cuf kwasababu alidhamiria kuepusha madhara na umwagaji damu inanipa ukakasi kuikubali.

..Kama suala lilikuwa kuepusha madhara kwa wananchi basi Maalim Seif na Cuf walitakiwa wasishiriki kabisa uchaguzi, au hata siasa.

Cc mdukuzi
 
  • Thanks
Reactions: Ilu

Kabisa mkuu inatafakarisha sana,historia ya zanzibar ikuwa inaenda kuchange ila alituangusha sana, watu waliitikia ombi lake la kupiga kura, yeye akalegea kusimamia ukweli wa matokeo ya uchaguzi akiwa kiongozi,yaani na hivi hayopo CCM itatawala milele Zanzibar, kwanza kura za upinzani zimeshagawanywa baina ya ACT na CUF
 
Kabisa mkuu inatafakarisha sana,historia ya zanzibar ikuwa inaenda kuchange ila alituangusha sana,watu waliitikia ombi lake la kupiga kura,yeye akalegea kusimamia ukweli wa matokeo ya uchaguzi akiwa kiongozi,yaani na hivi hayopo ccm itatawala milele zanzibar,kwanza kura za upinzani zimeshagawanywa baina ya ACT na CUF

..Na kitu kingine ni kama vile hawakuwa na mpango wa kujenga chama huku TANGANYIKA.
 
Maalim alifukuzwa CCM kwa usaliti
Laki...
Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir alikamatwa mwaka wa 1968 usiku akarudishwa kwao Zanzibar kwa tuhuma za kutaka kupindua serikali.

Salum Abdallah babu yangu alikamatwa mwaka wa 1964 kwa tuhumu za kutaka kupindua serikali na akawekwa Jela ya Uyui.

Sheikh Mselem bin Ali na masheikh wenzake waliwekwa jela kwa miaka 8 kwa tuhuma za ugaidi.
Hizi ndizo siasa za Afrika.

Haishangazi kuwa Maalim alifukuzwa CCM kwa, ''usaliti.''
Unaamini utakacho - ''kupindua serikali, ugaidi,'' ''usaliti'' nk. nk.
 
Ndio kitaondoka nae
Mdukuzi,
Hili ni tawi la CUF mtaani kwangu tukisheherekea ushindi wa viti vyote serikali ya mtaa mwaka wa 2015.

Wagombea wetu kama wakiruhusiwa In Shaa Allah tutachukua ushindi bila shida.
Naamini umenielewa.

1644698227879.png

1644698093344.png
 
Back
Top Bottom