Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,051
- 461
Jamani wana MMU hapa mwenzenu yamenikuta kujifanya mkweli kwa kila jambo....Jana jioni mama karudi toka kwenye mihangaiko yake, kama kawa nikamhug kimahaba, tukakissiana kama, tukavutana kuelekea MANSION kwetu, sasa hapo kiama kikaja baada ya kumwambia..."Mama kaoge kwanza maana jasho limekupiga sana", mwenzenu kusema tu hivyo mama kaja juu, mie nanuka au sio? nenda katafute wasionuka na maneno kibao tu...Nikajiuliza, mbona nikimwambia leo nimepata hiki hufurahia, nikimwambia jana fulani kanitextia ujumbe huu usome anafurahi....Je, ni vitu gani tuambiane ukweli na vipi tusiambiane? niko Dilema jamani....