Ukweli ni huu, hakuna usawa kwenye ndoa za kikristo wala ki-islam. Kama huwezi masharti nenda bomani tu

Ukweli ni huu, hakuna usawa kwenye ndoa za kikristo wala ki-islam. Kama huwezi masharti nenda bomani tu

pakamwam

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
516
Reaction score
654
Niande tu kwa kusema mkataba na maagano ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuangalia katika maisha kabla hujaingia

Kwa kiswahili sanifu agano ni tokeo la kukubaliana au kuwekeana ahadi au mapatano

Mapatano ni maafiiano, makubaliano ,agano na ahadi

Mapatano au maagano huzaa mkataba

Mkataba ni makubaliano yaliyofikiwa kwa kuandikiana baina ya watu au vikundi viwili kufanya jambo au kazi fulani

Leo nazungumzia mkataba wa ndoa

Hii mikataba imegawanyika kwenye makundi mbali lakini makuu ni matatu

Aina ya kwanza mkataba wa ndoa inayoambana na mlengo wa dini fulani kama ukristo au uislam. Kwa kawaida huu mkataba huwa unajali sana vipengele na misingi ya dini husika. Katika dini zote mbili zinafanana kwa maana ya kuwa mwanamke ni msaidizi wa mwanaume na hayuko sawa na mwanaume kimaamuzi. Ni kama rais, makamu ni msaidizi wake na inamaanisha rais anaweza kumtuma lakini sio makamu kumtuma rais zaidi ya kumshauri. Tofauti ya dini hizi mbili ni idadi ya wanawake wa kuoa.

Matatizo mengi tunayoyaona sana kwenye ndoa za hasa sisi vijana ambao huwa tunaingia kwa hisia pekee bila kujua undani zaidi inakuwa shida. Ndoa za wazazi wetu zilidumu maana walijua maana ya mkataba na dini waliyoingilia huo mkataba.


Matatzi yalikuja pale tulipoanza habari za usawa. Kwa ukristo haki ya mwanamke ni kupendwa tu na kupewa mahitaji ya msingi. Wajibu wa mwanamke ni utii kwa mume wake na hilo halina mjadala. Hili ndio limekuwa kero kwenye ndoa sana. Wengi hawajui kutii na kunyenyekea inamaanisha nini.

Mambo ya kukosa utii yameleta habari ya usawa ambao sasa unatafuna mataifa kama japani. Wanawake hawataki kuzaa tena maana wako busy kutafuta. Sasa japan in dying population mpaka imefikia wakati ukizaa unalipwa

Kama wewe ni mkristo na umefunga ndoa ya kikristo inamaanisha umeingia mkataba wa kuishi ndoa ya kikristo au kiisilam ambazo hazitambui usawa. Kazi yako wewe ni kutii mume wako. Usifurahia sherehe kubwa bila kuelewa mkataba ulio ndani yake

Mkataba wa pili ni ndoa za bomani. Hizi ni ndoa za zisizoambana na mlengo wa dini yoyote. Hizi huwa zinakwenda kwa shera za nchi. Huku kuna usawa mwingi maana mbele ya sheria wote sawa. Lakini kwenye dini nafasi zetu ni tofauti sana. Mtazamo wangu kwa kuangalia mataifa yalioyoendelea aina hii ya ndoa ni hatari kwa ustawi wa jamii kabisa. Angalia mfano wa japan na italia

Mkataba wa tatu ni ndoa za kimila ambao zinafanana na za kidini ila zenyewe huwa zinaendeshwa na mila za kabila husika. Ili ufurahie ndoa hii ni vyema kuoa mtu wa kabila lako anayejua mila za kwenu vizuri

Haya mambo mengine tunajipa shida maana tunakengeuka masharti ya mikataba na maagano tuliyowekaa. Mara nyingi zipo shida nyingi sana za kuvunja mikataba na maagano

Jumapili njema
 
Back
Top Bottom