Ukweli ni kuwa dunia imejaa hila

Ukweli ni kuwa dunia imejaa hila

Teleskopu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
702
Reaction score
767
Huwa tunaambiwa:
Wataalamu wamefanikiwa kuondoa ndui (smallpox) duniani kutokana na dungadunga.
Je, kuna ukweli wowote?

Asilimia zaidi ya 95 ya wanadamu watakwambia NI KWELI. Ukiwaambia NI UONGO utatukanwa, utabezwa, unaweza hata kupigwa mawe, au kufanyiwa chochote kibaya MAANA HUNA AKILI WEWE! Wewe ni nani ukatae wakati dunia nzima na hata WHO wanasema hayo ni mafanikio ya dungadunga?

Lakini data zinasemaje?

Smallpox and other epidemics were largely controlled by improvements in sanitation and nutrition years before vaccination became popularized.
Source: The Poisoned Needle Suppressed Facts About Vaccination by Eleanor McBean uk 6.

Maana yake:
Ndui na magonjwa mengine ya kuambukiza yalishadhibitiwa kutokana na kuboreka kwa usafi na lishe miaka mingi kabla ya “dungadunga” kupata umaarufu.

Katika ukurasa wa 11 Eleanor anatupa data zifuatazo:

CHART SHOWING DECREASE IN SMALLPOX DEATHS AFTER DECLINE OF VACCINATION
PeriodPercentage of BirthsVaccinated Smallpox Deaths
1872-188196.53,708.3
1882-189182.1933.0
1892-190167.9436.5
1902-191167.6395.3
1912-192142.312.2
1922-193143.125.0
1932-194139.91.4

Hii inaonyesha kuwa mwaka 1872-1881 ambapo asilimia 96.5 ya watoto walipitiwa na dungadunga, vifo vilikuwa karibu ya 4000. Mwaka 1932-1941, ambapo Eleanor anasema (when the vaccinations were resisted) kiasi kwamba ni asilimia 39.9 tu ya watoto walipata dungadunga, vifo vilishuka hadi 1.4.

Ukisoma kitabu cha Virus Mania kilichoandikwa na Torsten Engelbrecht na Claus Kohnlein ukurasa wa 11, wanasema hivi:

… in England, prior to the introduction of mandatory vaccinations in 1953, there were two smallpox deaths per 10,000 inhabitants per year. But at the beginning of the 1870s, nearly 20 years after the introduction of mandatory vaccinations, which had led to a 98% vaccination rate, England suffered 10 smallpox deaths per 10,000 inhabitants annually; five times as many as before. "The smallpox epidemic reached its peak after vaccinations had been introduced," summarizes William Farr, who was responsible for compiling statistics in London.

Maana yake:

…Uingereza, kabla ya kuanzishwa kwa dungadunga za lazima mwaka 1953, kulikuwa na vifo viwili vya ndui kwa kila watu 10,000 kwa mwaka. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 1870, karibu miaka 20 baada ya kuanzishwa dungadunga ya lazima, ambayo iliwezesha kufikiwa kwa kiwango cha 98%, Uingereza ilipata vifo 10 kwa kila watu 10,000 kwa mwaka; mara tano ya viwango vya kabla. Gonjwa la ndui lilifikia kilele chake baada ya dungadunga kuwa imeanzishwa,” anasema William Farr, aliyekuwa mhusika wa kuandika data pale London.

Mambo haya hayajaanza leo.

Tunaweza kutoa mifano mingi lakini huenda wengi watachoka kusoma na isiwe na faida. Hoja kuu na ya msingi hapa ni hii: Tafuta taarifa kabla ya kuamini tu jambo - whether wewe ni mtoa taarifa au mpokea taarifa. Hata watoa taarifa wengi wanazitoa kwa nia njema kabisa, ila bila kujua ukweli wa taarifa zenyewe.

Jamii isiyotaka kujifunza historia itatumbukia kwenye shimo lililoangamiza waliopita maana itadhani inayopitia ni mambo mapya, kumbe ni marudio tu.
 
Ni kama gwajiboy anavyofanywa kuhusu chanjo za uviko na abrakadabra zake duniani. Hata mitandao na media zingine hazitaki kuona upinzani wa chanjo
 
Ni kama gwajiboy anavyofanywa kuhusu chanjo za uviko na abrakadabra zake duniani. Hata mitandao na media zingine hazitaki kuona upinzani wa chanjo
ni kweli mkuu. Waovu hutumia kutojua kwa watu kujipatia utajiri, maana wanauza takataka mbalimbali ambazo wanazipa majina mazuri na kudai zinaleta afya.
 
Back
Top Bottom