Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Haya mazao ya kilimo ya biashara bei zake kwenye soko la dunia hupangwa na hao wakubwa (mabepari) wa dunia. Bei hizi hazipangwi na watanzania.
Ukweli ni kuwa haya mazao kila moja lilikuwa na enzi zake kwenye kinara. Kulikuwa na enzi ambayo zao la mkonge lilikuwa ni lulu kwa kutupatia fedha za kigeni. Ululu wake ulikuja kuporomoka baada ya ugunduzi wa kutengeneza kamba za synthetic materials kama za nylon viwandani.
Kuna enzi za pamba kuwa kinara kwenye soko la dunia kwa ajili ya kutengenezea nguo. Ululu wake ukaporomoka baada ya ugunduzi wa kutumia synthetic materials kama tetron na nylon kutengenezea nguo.
Kulikuwa na enzi ya zao la tumbako kutengenezea sigara, cigars na tumbako ya kuvuta kwenye kiko. Enzi zake ziliporomoka baada ya kupiga vita uvutaji wa sigara, cigars na viko baada ya kugundua kuwa uvutaji huo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Kuna enzi ya kahawa na chai kuwa kinara wa mazao ya kuingiza hela za kigeni. Ukinara wake uliisha baada ya nchi mbali mbali duniani kuwa na uwezo wa kuzalisha kahawa nyingi na nzuri zaidi ya ile ya kwetu.
Enzi za hivi karibuni korosho ilikuja kuwa kinara baada ya nchi ya China ambayo ina idadi ya watu robo moja ya dunia kupenda kula korosho. Ilifikia mwaka 2016 kilo moja ya korosho ghafi iliuzwa zaidi ya shillingi 5,000/ hadi watu wa Mtwara kuanza kuwanywesha mbuzi wao bia! Ukinara wa korosho uliporomoka baada ya muda mfupi tu kutokana na China kuweza kuzalisha korosho nyingi zake yenyewe.
Huo ndiyo ukweli. Bei hizo hazikutelemka kwenye soko la dunia kwa utashi au kwa makosa ya kisiasa. Njia pekee ambayo tunaweza kupata bei nzuri kwenye soko la dunia ni kuachana na kuuza mazao hayo yakiwa ghafi. Kama ni korosho tunatakiwa tuiuze ikiwa imebanguliwa. Kama ni pamba tunatakiwa tuiuze ikiwa imeshatengenezwa kuwa nguo. Kama ni ngozi ya ng'ombe tuiuze tukiwa tumeitengeneza kuwa kiatu au begi au sofa. Vivyo hivyo kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi mengine. Hakuna cha siasa hapa bali ni sayansi na tekinolojia tu.
Hata madini yetu hali ni hiyo hiyo. Tusiyauze yakiwa ghafi. Na hii kwa bahati nzuri ndiyo dhamira ya serikali yetu. Tunatumaini wakipewa miaka mitano mingine watatimiza dhamira hii kwani kwa mara ya kwanza serikali yetu inaongozwa na mwanasayansi aliyebobea. Tumeshuhudia manufaa ya kuongozwa na mwanasayansi katika mapambano ya kisayansi dhidi ya janga la kisayansi la COVID 19! Tusiitupe bahati hii.