SoC03 Ukweli uliojificha na maumivu yake

SoC03 Ukweli uliojificha na maumivu yake

Stories of Change - 2023 Competition

Bulali Mt

New Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
1
Reaction score
2
Katika jamii zetu za Kiafrika hasa Tanzania elimu ni kitu ambacho kimepewa umuhimu tangu mtoto anapofikisha miaka miwili anapelekwa shule za chekechea kuanza kusoma. Wazazi wengi wamekuwa na dhana halisi kwamba mtoto anatakiwa asomeshwe na lengo kuu la kuwapeleka watoto shule ili baadaye awe msaada kwa familia, kwa kuwa wanaamini baada ya kusoma ataajiriwa Serikalini na kupata mshahara mnono ambao utawanufaisha familia kwa ujumla. Kama zilivyo familia nyingi za hapa Tanzania na Mimi nilipelekwa shule pamoja na changamoto nyingi za kukosa ada, mavazi na vifaa vya darasani kutokana na familia yetu kuwa duni kiuchumi nilianza darasa la kwanza na kuendelea na masomo.

Kiukweli niliipenda elimu ya darasani sana hakuna ambaye aliweza kunipita katika masomo yote darasani. Niliendelea hivyo hadi darasa la Saba. Baada ya mtihani wa kumaliza darasa la Saba na Mimi nilipelekwa shule za Kata. Kwa kuwa nilikuwa nimetoka katika familia duni nilichelewa kwenda shule kutokana na kutokidhi mahitaji ya shule. Baada ya miezi mitatu nilifanikiwa na Mimi kwenda shule japokuwa nilikuta wenzangu wamesoma vitu vingi bado nilijipa tumaini kwamba na Mimi nitaongeza bidii ili niyajue yale ambayo wamefundishwa kabla sijaja.

Baada ya wiki moja nikawa sawa na wao. Tulifanya mtihani na nilifanya vizuri zaidi ya wanafunzi ambao walinitangulia. Siku moja Mkuu wa shule alikuja darasani kwetu akiwa na daftari akaanza kusoma majina ya wanafunzi ambao hawajalipa ada. Kwa kuwa na Mimi ni miongoni mwao jina langu lililosomwa. Kati ya siku siwezi kuisahau ni ile nilichapwa fimbo sita na kuamuriwa kwenda nyumbani kuleta ada. Kiukweli niliumia sana.

Niliondoka kuelekea nyumbani, nilipofika nilimweleza mama yangu na akaniambia kama ni hivyo kaa tu Mwanangu nyumbani kwa kuwa nafahamu hela hazipo nyumbani. Nakumbuka ilikuwa jumatatu nilienda tena shuleni sasa hii siku haikuwa nzuri kwangu baada ya usafi wa mazingira ya shule, kengele iligongwa na tukaenda paredi kama ilivyokuwa desturi ya shule ile. Mkuu wa shule alikuja tena pale paredi na akaanza kwa kufoka sana, akasema kama unajua hujakamilisha ada pita mbele nilipita mbele na alianza na Mimi nilipigwa kama vile Mimi ni mtuhumiwa, aliamuru tuende nyumbani kufata ada. Niliondoka na sikwenda nyumbani maana ningeenda nyumbani mama yangu angelia sana kuniona na maumivu yele. Nilikaa barabani pembeni mwa shule. Lakini Cha ajabu Mkuu wa shule alikuja tena na kutufukuza tuondoke.

Kwa ufupi niliendelea kuishi maisha ya kupigwa kama Mkuu wa shule yupo akisafiri ni furaha kwangu. Lengo langu linitaka hata kama sitafaulu huo mtihani angalau nipate elimu ambayo itanisaidia hapo baadaye.
Baada ya maisha yale ya mateso nilifanikiwa kufanya mtihani wa KIDATO CHA NNE na kuondoka Mkoa ule ambao nilisoma na kwenda Mkoa mwingine. Nilianza kujishughilisha na kazi za mikono ili maisha yaende.

Nilianza kwenda chuo cha computer kwa mkopo na baada ya mwezi Mkuu wa shule akaomba ada nikawa Sina kwa wakati huo akanifukuza. Kwa kuwa nilikuwa tayari nimejua computer kiasi fulani kwa kufahamu program kama vile Microsoft word na Microsoft publisher nikaamua kuanza kazi za mikono na baada ya muda nilifanikiwa kununua baaddhi ya mashine za kufanyia kazi kama vile computer moja na printer moja. Nikaamua kufungua kiofisi kidogo ambacho kilinipa mahitaji yangu. Kupitia Ile ofisi nikaanza kuwatunza wazazi wangu na nikafanikiwa kulipia mahari na kuoa mke wangu ambaye kwa sasa tayari tuna mtoto mmoja.

Pamoja na KUFELI KWANGU KIDATO CHA NNE naamini sana katika biashara. Nimeona wafanyabiashara wengi hawana elimu sana hapo elimu pia ni nzuri. Nadhani sisi ambao tulifeli serikali inatuchukia sana maana haiweki mazingira mazuri kama kwa wenzetu ambao wanafaulu maana wao baada ya Kidato Cha sita wanapewa mikopo. Hakuna kitu sipendi kama wanaofeli kuonekan wajinga na hawawezi kitu chochote jambo ambalo sio sahihi.

Nadhani serikali na wadau wa maendeleo warudi waone namna Bora ya kuwasaidia wanaofeli Kidato Cha nne. Sisi ndio nguzo ya uchumi hawajui tu kinachohitajika na kupewa kipaumbele kwa kupewa mitaji ili tuweze kufanya biashara maana naamini sana katika biashara. Wahitimu wengi wa elimu ya juu kwa sasa hawana uwezo wa kufanya kazi na hata kusimamia biashara kwa kuwa akilini mwao wanawaza ajira. Nadhani turudi kama nchi kwa ujumla tumuone aliyefeli darasani anaweza kufaulu vizuri zaidi nje ya darasa.

Naamini kupitia andiko hili japo ni kama simulizi lakini naamini nimefikisha ujumbe mahali husika.
Simu: 0621 044 216
 
Upvote 2
Back
Top Bottom