Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Wakati maeneo mengi nchini wakiendelea kufaidi matunda ya kinachoitwa Elimu Bure/Elimu bila Ada, huko mkoani Singida Wilayani Ikungi kata ya Choda, Shule ya msingi Choda wanafunzi wanataabika kwa kukaa chini madarasani. Ni watoto wa wakulima na wafugaji ambao ni sehemu ya walipa kodi katika wilaya hiyo.
Hili ni tatizo la muda mrefu sana ambalo uongozi wa shule hiyo imekua ukiogopa kulisema pengine kwa kuogopa kuchukuliwa hatua na uongozi wa Wilaya ambapo viongozi wa Chama wilaya wakiongozwa na mwenyeki wa chama wilaya ndugu Mika Likapakapa ambaye amekua akiwatishia walimu ndani ya wilaya hiyo wakisema matatizo yao atawafukuzisha kazi kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.
Wananchi kwa kipindi kirefu wameamua kulisema tatizo hili wao wenyewe pengine kelele zao zinaweza kusaidia.
Cha ajabu tatizo hili mbunge wa jimbo hilo ndugu Mitaji Mtaturu analijua kwa muda mrefu, kila aliambiwa amekua akipiga chenga, diwani wa kata ya Choda analifahamu tatizo hili lakini naye awali alikua akilisemea lakini pengine kwa kuogopa kunyimwa posho na Mkurugenzi naye ameamua kupiga kimya sasa.Jimbo zima hali halisi ndio iko hivyo pamoja na jimbo kua na uwakilishi pamoja na uongozi wa wilaya.
Mpaka jicho la Fundi Madirisha linapenya kunako shule hiyo, hali. Ni mbaya sana si kwa sababu hakuna uwezo wa kushughulikia na tatizo hilo au wanafunzi ni wengi, laahasha ni viongozi wameamua kulifumbia macho tatizo ili vijana wa wakulima na fugajj waendelee kukaa chini wakati watoto wako wako English Medium.
Haya si mambo ya kuachwa yaendelee wala kufumbiwa macho wakati hali shwari hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali inajinasibu kua ni Elimu bila Ada.