SoC02 Ukweli uongo ama dhamira ya kujenga?

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 28, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Dhamira Dhamira Dhamira
Marudio ama msisitizo huakisi juu ya umuhimu wa jambo,dhamira ni hitaji kuu na lengo katika kila hatua ambayo kijana huichukua katika kuyaendea mafanikio.

Je, ni ipi dhamira yako kwako,kwa familia yako na kwa nchi yako?

Je ni ukweli? Uongo? Ama dhamira ya kujenga ndiyo inaiendesha nafs yako?

Vijana Vijana Vijana
Je sisi ni kesho ya taifa?

Je, ni kweli makala nzuri ni ile inayojenga fikra kwa kuuliza maswali bila kutoa majibu? Ama ni ile yenye kutoa majibu bila ya kutafakarisha mbongo zetu. je? kiongozi bora ni yupi, Yule mwenye kufikiri jana na kuitaka kesho njema ama ni yule mwenye mipango ya kuijenga kesho kwaajili ya mtondogoo njema.

Je, Uongozi bora ni kuonesha uovu wa viongozi na washirika wako kwa kuwazalilisha ili uwe bora miongoni mwao? Ama nikupandikiza mbegu ya uongozi bora kwa vijana na msingi imara kwaa uongozi uliopo? Lakini tujiulize tena je?

Ni vipi kama hatupati nafasi ya kuleta mawazo mapya ,nivipi kama kila tunapojaribu kuleta hoja mpya tunakandamizwa kwa makosa yetu madogo madogo na kuididimiza dhamira yetu kubwa ya kujenga taifa?

Je, Uongozi bora unaanza na nan?

Na je? Ubora wa kiongozi lazima uanzie ngazi fulan?

Lakinii je? Wewe ni kiongozi bora katika ngazi yako ya uongozi?

Kwa muda nimechunguza juu la swala hili la vijana kujihimiza katika uongozi bora wengi wetu tumekuwa ni watu wa kupenda uongozi ili tujipatia vitu fulani fulani kama kuheshimika na kuwa na maisha ya juu kwa kupata mishahara minono tunayoitarajia tutakapokua viongozi, Huu ni mtazamo wa vijana wengi wa kitanzania je?

Hii ni sahihi,HAPANA mimi nakataa nawewe unakataa lakini bado mawazo haya hayatapotea kirahisi tusipokumbushana,vijana ndiwo taifa la kesho na dhamira ya kijana kuwa kiongozi yapaswa kuwa ni kujitoa na kutumia kipaji ama elimu aliyonayo kuwatumikia walioko chini ya uongozi wake kwa maslahi ya taifa na si binafsi

Hii inanifanya nifikiri yakwamba sisi vijana tunamzigo mkubwa wakuzitafakarisha mbongo zetu juu ya misingi bora ya kiuongozi ambayo itaishi ndani ya kila mtanzania karne na karne baada ya vichwa vyetu kugeuka mafuvu ardhini na majina yetu kubakia historia inayofunza na kuadabisha katika sekta hii tukufu ya uongozi na kizazi kijacho wataipamba kwa kuwa viongozi bora wenye kuzingatia maslahi ya nchi.

Hivi ni kweli sisi vijana si waoga?
Tunaweza kujipiga kifua tukisema sisi ni wenye mapenzi ya dhati na nchi yetu?
Kama majibu ya haya maswali yakiwa ndiyo naapa kwa jina la taifa 'Tanzania ewe nchi yangu' hakika tutaondokana na umaskini kwani taifa lenye vijana wenye maono chanya na kujitoa juu ya nchi yao ndilo taifa kubwa lielekealo katika mabadiriko chanya katika kila sekta kwani vijana ndiyo nguzo ya taifa vijana ni tunu vijana ni tunzo ya taifa.

Nimetumia muda kusoma historia za nchi nyingi zilizoendelea duniani kabla ya kuandika makala hii na nimekuja kufumbuka juu ya umuhimu wa vijana katika taifa na ndio maana sitaki kuuacha ufumbuzi huu upotee mithiri ya pamba kwenye upepo mkari, katika historia zote za duniani nilizojifunza kuhusu nchi zilizoendelea nimepata kitu kikubwa pale nilipokutana na historia ya nchi ya China iliyoko bara la Asia iliyosemekana kuwa na uchumi duni kuliko baadhi ya nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania katika miaka elfu iliyopita, Maisha ya nchini humo hayakuwa hata kiwango cha kuridhisha, Maisha yalikua mabaya ya taabu yaliyowafanya wachina kuona dunia ni adhabu kubwa waliyopewa na mwenyez mung, je? Unajua ni vipi china iliweza kuwa taifa kubwa lililo na uchumi mkubwa na mazingira yake kuonekana kama pepo ndogo iliyoshushwa na mungu. !?

Katika historia nyeti kabisa iliyofichwa katika makabati makubwa yanayotunza historia huko katika ardhi ya china kuna vitabu mbalimbali vinavyoonesha mbinu za kitaaluma zilizopelekea mabadiriko ya kiuchumi mbaka kufikia hali ya sasa tunayoiona nnchini humo ,hii ni siri "HII NI SIRI"
Na siri hazitoki bure! Na mimi sitoitoa siri hii bure kwa mtu yoyote yule isipokua yule anaelenga kuwafunza vijana juu ya kulikomboa taifa lao.

Nasas kwa majina ya wazalendo wetu wapenda haki Mwl. Nyerere baba wa taifa, Dr ally hassan mwinyi,jemedari B,william mkapa,mheshimiwa kikwete,Dr john,p,Magufuri,Mama samia suluh hassan (Mama jasiri malkia wa nguvu) nakwenda kuitoa siri hii.

Na hii siri kubwa yenye kuletamabadiriko chanya ya kijamii ni 'ELIMU YA UZALENDO' Silabi (15) zimetosha kabisa kueleza juu ya siri hii kubwa, Kwa haraka haraka unaeeza kuichukulia siri hii kama mzaha ngoja sasa nikujuze, Huko nchini china enzi za umaskini na ulala hoi vijana wa kichina walikosa ajira na walishikilia ya kwamba viongozi wao ni walaghai,waongo na wasaliti na wakawa wanaamini msemo uliosema "Serikali inapesa raia twateseka" Hali hii ilipelekea serikali iliyokuwa madarakani kuchukua hatua ya kutoa elimu ya uzalendo ambapo wazo hilo lilipingwa na baadhi ya viongozi wakisema kwa hali ya lawama iliyopo elimu ya uzalendo ingeweza kuwachochea wananchi kupigana na serikali yao licha ya upinzani hiyo elimu ya uzarendo ilitolewa kwa mbinu mbalimbali zilizopelekea vijana kutambua ya kwamba nchi yao ni jukumu lao wanapaswa kuipambania na si kulaumu serikali iliyoko madarakani na si kuilaumu na kuipa wakati mgumu kufanya maendeleo, sas hapo kila kijana akaamua kujitoa wakaweza kuungana na kuwa wamoja na kuchukuliana kam ndugu na kuamua kujenga taifa na hii ndio inayosemekana sababu ya wachina kuonekan wakifanana fanana kwani vijana wao waliuvaa uzarendo kiasi miradi ya kitaifa ilijengwa kwa mtindo sawa na wanajeshi wawndapo vitana 'familia yangu mnitinzie napigana nnchinyangu iendelee' vijana walifanya kazi asubuhi na jioni serikali iliwagalamia chakula, mavazi na makazi walio na nguvu walifanya kazi za nguvu, Wenye kushughulisha akili walifanya kazi za akili na kuunda bidhaa nyingi zilizoleta ushindani, kwani wewe si shahidi
1) Hukuona mchina akitoa copy za bidhaa zote za kimarekani na kijerumani
2) Hukuona bidhaa zikiwekwa umiliki kwa watu wa china kwa pamoja, mfano(cherehani ) hukuona zikiandikwa "Made by the people republic of china"
3) Hakika uliona na tumeona na huu ndiwo mzizi wa mafanikio yao

UZALENDO NCHINI
Enzi za ukoroni uzalendo ulikua juu na kuunganisha mababu zetu na wakamshinda mkoloni na kuwa huru lakini angalia sasa jinsi uzalendo umepungua baina ya vijana wa kitanzania, Unakuta kijana hajui hata beti mbili za nyimbo za kizalendo si "Tanzania Tanzania" wala "Tazama ramani" Aibu! Aibu kubwa tutaweza kujitoa kwa mambo makubwa ya kizalendo kama kunakiri beti chache vichwani mwetu kunatushinda? Tujiulize na kujitafakari, Huu si uozo na ukosefu wa uzalendo mtanzania mwenzangu?Hapa pia nikatambua misingi bora ya uongoz tunayotakiwa kuisimamisha yote inaanzia na ujenzi wa mapenzi ya dhati kwa nchi yetu na huo ndio unaoitwa uzalendo, uzalendo ndio jiwe la mwanzo katika msingi wa uongozi bora nchini, Hakuna mahala patakatifu kwa mtanzania isipokua nchini kwake yote si ya maana ila yale yanayomuhusu mtanzania na nchi yake, Ifikie kipindi uzalendo ushamili nchini mbaka Tuonane kama ndugu hata kama hatujuani ilhali tukijua sote ni watanzania popote pale tukutanapo sisi ni ndugu na tutalindana na kulinda heshima ya taifa letu lililobarikiwa kwa ardhi nzuri na madini, Wananchi na viongozi tusiwe wenye kufanya mashindano kwa kuumbuana na kudharirishana kwa kuufumbua ukweli na uongo wa bandia hilo halitusaidii sifa ya mtanzania mmoja ikiharibika sifa ya nchi yetu inadhorota tujenge dhamira ya kujijenga kuwa bora hilo ndilo dhumini letu sisi ni Watanzania tulinde heshima yetu, Mtanzania ndilo liwe jina letu kabla ya jinalolote tulopewa na wazazi wetu kwani Tanzania nchi yetu ndiye mama na mzazi wa koo zetu na huyu mtanzania wa kuyatekeleza haya ni wewe na mimi, 'Hakika ni wewe na mimi mtanzania mwenzangu'

Je?nikuelekezana ama kukasirikiana,kuzungushana,kukunjiana sura,kupeana wakati mgumu katika kuelewa,kudharirishana na kutiana unyonge humfanya mtu kuonekana kiongozi mwenye msimamo? Si vyote hivyo sisi vijana viongozi bora wa kesho yatupasa kusimamia uungwana,uadilifu na kujitoa ili kuwa viongozi bora wennye misimamo

Tanzania, Tanzania
Mungu awe nawe daima

Sitamani kusema mbaka mnichoke namimi si mwingine bali ni kilio cha vijana wakitanzania wenye maono chanya juu ya taifa lao
 
Upvote 2
Asante ndugu yangu unaweza kunisaidia kushare kwa wengine ili ujumbe umfikie kila mmoja wetu kwa ujenzi wa fikra chanya
Lengo haswa ni kujipa changamoto vijan ili tuwez kupambana kuwa viongozi bora zaidi na zaidi kwa msaada wa viongozi bora wasasa ambao ni kam wazaz wetu katika swala zima la uongoz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…